Hijabu

Egypt's Dar Al-Ifta

Hijabu

Question

 Aya ya Qur`ani:
Mwenyezi Mungu Anasema:
{Na mnapo wauliza wakeze haja waulizeni nyuma ya mapazia. Hivyo ndio usafi zaidi kwa nyoyo zenu na nyoyo zao} [AL AHZAAB 52]

Answer

 Na akasema tena:
{Hapana ubaya kwao (wake za Mtume) kuonana na baba zao, wala watoto wao, wala ndugu zao, wala watoto wa ndugu zao wanaume, wala watoto wa ndugu zao wanawake, wala wanawake wenzao, wala wale waliyo wamiliki mikono yao ya kulia. Na enyi wanawake, mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kushuhudia kila kitu} [AL AHZAAB 55]
Mwenyezi Mungu Amesema:
{Na waambie Waumini wanawake wainamishe macho yao, na wazilinde tupu zao, wala wasioneshe uzuri wao isipokuwa unao dhihirika. Na waangushe shungi zao juu ya vifua vyao, wala wasioneshe uzuri wao ila kwa waume zao, au baba zao, au baba wa waume zao, au watoto wao, au watoto wa waume zao, au kaka zao, au wana wa kaka zao, au wana wa dada zao, au wanawake wenzao, au iliyo wamiliki mikono yao ya kuume, au wafwasi wanaume wasio na matamanio, au watoto ambao hawajajua mambo yaliyo husu uke. Wala wasipige chini miguu yao ili yajuulikane mapambo waliyo yaficha. Na tubuni nyote kwa Mwenyezi Mungu, enyi Waumini, ili mpate kufanikiwa} [AN NUUR 31]
Mwenyezi Mungu Amesema:
{Ewe Nabii! Waambie wake zako, na binti zako, na wake wa Waumini wajiteremshie nguo zao. Hivyo nikaribu zaidi kuweza kutambulikana wasiudhiwe. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu} [AL AHZAAB 59]
Anasemaje mwenye kudai:
Al-Baidhawy amesema: Imepokelewa kuwa Omar amesema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu anakuja kwako mtu mwema na hata mtu muovu, lau utawaamrisha Mama wa Waumini kuvaa hijabu, ndipo ikateremka Aya…. “Hapana ubaya kwao (wake za Mtume) kuonana na baba zao, wala watoto wao, wala ndugu zao, wala watoto wa ndugu zao wanaume” wakiondolewa wale wasiopaswa kujihifadhi kwa ajili yao.
Na imepokelewa kuwa baada ya kuteremka Aya ya amri ya kuvaa hijabu akasema ni mbele ya baba watoto na ndugu wa karibu: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu pia tuzungumze nao nyuma ya pazia? Ikateremka Aya. Lakini hakutajwa baba mdogo wala mjomba kwa sababu wanazingatiwa ni sehemu ya wazazi wawili, au ni kwa sababu inachukiza kuacha kuvaa hijabu mbele yao kwa kuhofia kuwasifia kwa watoto wao, wala mbele ya wanawake wenzao kwa maana ya wanawake waumini, wala mbele ya wale wanao wamiliki kwa mikono yao ya kiume miongoni mwa watumwa na wajakazi na ikasemwa ni wajakazi maalumu.
Tunauliza: Je hijabu ya mwanamke inazuia jicho la muovu kutotamani? Kwani jicho la muovu linaona kwa mtazamo wa hisia, kwani Injili imezungumza kuhusu kuzaa upya na mabadiliko ya moyo kwa matendo ya roho mtakatifu ambaye matokeo yake “Mvue kwa habari ya mwenendo wa kwanza utu wa zamani unaoharibika kwa kuzifuata tama zenye kudanganya. Na mfanywe wapya katika roho ya nia zenu. Mkavae utu mpya, ulioumbwa kwa namna ya Mungu katika haki na utakatifu wa kweli”. Waefesso 4: 22 – 24 ( ).
Akasema kuna shaka katika Aya ya mia moja na sitini: Kilemba ni uwingi wa vilemba nacho ni kile mwanamke hujifunikia kichwa chake, na kushusha nguo zao inakusudiwa ni kusitiri shingo zao kwa kuanzia kufunika vichwa vyao.
Tunauliza: Ni namna gani mwanamke anawekwa ndani ya hijabu kunakofanana na jela? Kwani hijabu kwa mwanamke inauwa ari ya kufanya kazi kuendesha harakati na uhuru binafsi, na kurudisha ubinadamu kwenye zama za utumwa ( ).
Faida ya shaka:
1. Hijabu ya mwanamke haizui mtazamo wa mwanamme mwenye maradhi ya nafsi.
2. Hijabu inafanana na jela na kukwamisha kufanya kazi na harakati.
3. Hijabu inarejesha ubinadamu kwenye zama za utumwa.
Kuondoa shaka:
Kwanza: Hijabu kama inavyoonekana haimkwamishi mwanamke kwa chochote bali inahifadhi dini yake usafi wake na nguvu zake kutotawanyika katika kushuhurika na mapambo, na kumuwezesha nguvu hii kufanya vizuri katika maeneo mengine ya kazi na harakati zingine za kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu na kulinda utashi huu wa kupenda kujipamba kwenye sehemu yake sahihi ndani ya nyumba yake na kwa mume wake ambapo kwa kujipamba huko kuna neemesha maisha na kujenga msingi wa kwanza wa jamii sahihi nayo ni familia.
Inafahamika uwa mwanamke kufunika kichwa chake nywele zake na maeneo mengine ya mwili wake ni katika alama za utakasifu na wema, na kisha wafuasi wa dini zote wanatekeleza alama na kuizingatia ni katika alama za wema ukweli na utakasifu.
Mwenyezi Mungu amemuwekea Sharia mwanamke ya kuvaa hijabu kwenye Sharia zote za mbinguni, kwani Kitabu Kitakatifu kimekubaliana na Qur`ani Tukufu katika hilo, kwani zimekuja Aya ndani ya Kitabu Kitakatifu zinazoonesha Sharia ya mwanamke kusitiri kichwa na wema wa kujisitiri na kuchukiza kuonesha mapambo.
Katika kitabu cha Mwanzo kinasema: “Isaka akatoka ili kutafakari kondoeni wakti wa jioni; akainua macho yake akaona kuna ngamia wanakuja. Rebeka akainua macho naye alipomwona Isaka alishuka juu ya ngamia. Akamwambaia mtumishi, ni nani mtu huyu ajaye kondeni kutulaki? Mtumishi akasema, huyu ndiye bwana wangu basi akatwaa shela yake akajifunika”. 24/ 63, 64, 65 ( ).
Kujifunika kichwa hakukuwa kwa upande wa Waarabu peke yao bali kulikuwa kumeenea kwenye mataifa ya zamani huko Babel Ashuur Fursi Roma na India ( ).
Pindi jamii hizi zilipoachana na utamaduni huu mwema ndipo yakaanza kuonekana ambayo unayaona miongoni mwa maasi na madhambi makubwa, hivyo ukaja Uislamu na vazi la hijabu likiwa lipo kila sehemu likitumika kwenye Uislamu kama lilivyotumika kwenye dini zingine ikiwa ni katika mila na tamaduni zinazokubaliana na maslahi ya mwanadamu.
Pili: Uislamu ni dini inayolingania kwenye usafi wa moyo, na miongoni mwa makusudio yake ni pamoja na kulinda dini kulinda akili kulinda heshima na makusudio haya lengo ni kulinda jamii, na mwenye kudhuru heshima ya jamii katika jamii na kupelekea jamii kuharibu usafi wake na kuibuka fitina na madhambi makubwa na kuchochea mambo ya matamanio na kuibuka yaliyo haramu basi jamii hii inapinduka na kuzaliwa ndani yake matendo mengi yalio haramishwa.
Mfumo wa Uislamu wa maadili mema haufahamiki isipokuwa na kila aliyekamilikiwa, katika lengo la kulinda dini na heshima Uislamu umeweka hukumu nyingi, kiasi ambacho Mwenyezi Mungu ameamrisha usafi wa nia na akaharamisha uzinzi na anakubali ndoa na akahalalisha uwezekano wa ndoa ya wake wengi ikawa ni lazima ili kukamilika kwa Sharia kuepuka kufikia kwenye kinyume na hivyo ndipo akaharamisha mchanganyiko kati ya wanaume na wanawake kwa sura ambayo inahalalisha yaliyoharamishwa, na akaharamisha pia kukaa chemba na mwanamke si ndugu ambapo hakuna yeyote anayeweza kuingia isipokuwa kwa ruhusa, ameharamisha kumuangalia mwanamke isipokuwa kwa dharura, na akamuamrisha mwanamke kutozoea kuonesha mapambo yake kwa wanaume ili isiwe sababu ya kupotea kwao, ikawekwa Sharia ya hijabu kwa lengo la kulinda jamii kutokana na maasi, na hii ni amri ya Mola Mtukufu katika kila dini kama ilivyoelezwa.
Tatu: Muulizaji ameuliza hapa swali zuri kuwa, je hijabu ya mwanamke inamzuia mwanamme muovu kutamani? Jibu ni kuwa wanaume wapo wa aina mbili, kuna huyu mwanaume muovu ambaye anamzungumzia muulizaji, na kuna mwanamme mwingine ni msafi wa nafsi anataka kulinda nafsi yake kutokana na kumuasi Mola wake lakini fitina za wanawake ambazo zinaonekana mbele ya macho yake kila siku na kila sehemu ndio ambazo zinazuia kati yake na maasi, na hijabu ya mwanamke inamlinda mtakasifu utakasifu wake na usafi wa nafsi yake na inamtisha muovu na kumzuia kuingia kwenye kutongaza, na huu ndio ukweli.
Nne: Katika ulimwengu wetu kuna mifano ya jamii zisizozingatia utakasifu kwa mtazamo wa nje na mavazi na kuacha kwa kila mwenye kutaka kufanya kitu au jambo basi afanye pasi ya kizuwizi cha dini au mazoea au visivyokuwa hivyo na kudhani kuwa ustarabu unapingana na maadili mema pamoja na dini, na maadili pamoja na dini hazizalishi isipokuwa ukandamizaji wakafungua walipotaka matamanio hivyo haikuwa isipokuwa ni kupotea kwa Umma na kuenea majanga na maradhi na wala hawakuweza kuwa na njia ya kutoka kwenye shimo hilo ndipo wakaanza kulingania kwenye mema kwa ajili ya hali nzuri kwa Umma huu kwani wanakuta jambo hili lipo wazi hakuna shaka yeyote ndani yake.

Share this:

Related Fatwas