Muislamu Mgumu

Egypt's Dar Al-Ifta

Muislamu Mgumu

Question

Kwa nini wataalamu wanamweleza Muislamu kuwa ni mgumu au Muislamu mgumu?

Answer

Dhana hii ya Muislamu Mgumu imekuja kwa kuashiria ugumu wa kutoka Muislamu huyo katika zizi la imani isipokuwa kwa kupatikana kwa masharti matatu ambayo nadra kupatikana pamoja kwa hiyo Muislamu hahukumiwi kafiri endapo hakuthibitika kusifika kwa mambo haya matatu, ambayo ni; kuwa anakufuru kimakusudi akiwa anatambua kuwa vitendo na maneno yake huwa sababu ya kukufuru, endapo sharti mojawapo ya  masharti haya likikosekana basi ni ngumu kumhukumu Muislamu ukafiri kwa hiyo, huitwa "Muislamu Mgumu" kwa sababu ya ugumu wa kupatikana kwa masharti haya matatu pamoja, zaidi ya hayo, wataalamu wakataja maelezo zaidi kuhusu dhana hii katika vitabu vya Fiqhi na vinginevyo, ambapo walisisitiza kuwa ingawa kupatikana kwa masharti haya kwa baadhi ya Waislamu, basi hukumu ya ukafiri ni haki ya mahakama peke yake, hivyo kumhukumu Muislamu yeyote kwa ukafiri haikukubaliki isipokuwa na Kadhi aliyeteuliwa na Mtawala kwani hukumu kama hii hufuatana na mabadiliko mengi kama vile; hukumu za mali na urithi ambapo kafiri harithi muumini wala muumini harithi kafiri, pia, hukumu ya kupambanua kati ya mume na mkewe, na hukumu nyinginezo, kwa hiyo kumhukumu Muislamu kwa ukafiri ni jambo zito na fitina kubwa. 

Share this:

Related Fatwas