Utume kwa Watoto wa Isma'il na wato...

Egypt's Dar Al-Ifta

Utume kwa Watoto wa Isma'il na watoto wa Yakobu.

Question

 Imepokelewa ndani ya Qur`ani kauli ya Mwenyezi Mungu:

Answer

{Na hakika tuliwapa Wana wa Israili Kitabu na hukumu na Unabii, na tukawaruzuku vitu vizuri vizuri, na tukawafadhilisha kuliko walimwengu wote}. [AJ JATHIYAH 16]
Na kauli ya Mola Mtukufu: {Na tulimtunukia (Ibrahim) Is-haq na Yaaqub. Na tukajaalia katika kizazi chake Unabii na Kitabu, na tukampa malipo yake katika dunia; naye hakika Akhera bila ya shaka ni katika watu wema} [AL ANKABUUT 27].
Haya ni maelezo kuwa Utume ni kwa wana wa Israil bila ya wengine, na maelezo haya pia yanakubaliana na maelezo ya Taurati ambayo imetahadharisha wana wa Israil kumkubali mwenye kudai yeye ni Mtume kutoka kizazi cha Ismail, ikiwa Utume ni kutoka kwa wana wa Israil kwa mujibu wa ushahidi wa Taurati Injili na Qur`ani basi ni vipi Nabii wa Kiislamu anakuwa ni Nabii hali ya kuwa si katika kizazi cha Yakoub? Na vipi Qur`ani inasema:
{Na mtaje katika Kitabu Ismail. Bila ya shaka yeye alikuwa ni mkweli wa ahadi, na alikuwa Mtume, Nabii} [MARIAMU 54] Na wala haikusema kabisa Ismail katika wana wa Israil ili awe na Utume bali ndugu zake ndio ambao Utume haukuwa katika kizazi chake.
Na Qur`ani imeelezea ubora wa wana wa Israil kwa walimwengu wote ikasema:
{Enyi Wana wa Israili! Kumbukeni zile neema zangu nilizo kuneemesheni, na Mimi nikawatukuza zaidi ya wadamu wote} [AL BAQARAH 47]. Na Qur`ani ikataja mara kwa mara kuwa Is-haq ni mtoto wa pili wa Mzee Ibrahim, na Yakoub ni mjukuu wake wote hao wawili ni zawadi ya Mwenyezi Mungu kwa Mzee Ibrahimu bila ya kutajwa Ismail pamoja na kuwa ndio mtoto wa kwanza wa Mzee Ibrahimu.
Jibu la Shaka Hiyo:
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Kwanza Kabisa: Aya zilizotajwa hazina yanayopelekea madai hayo:
Aya hizi hazioelezei – kwa ukaribu wala kwa umbali – kuwakana watoto wa Ismail A.S wala kupinga Utume wa Mbora wa viumbe S.A.W
Kauli yake Mola Mtukufu Aliyosema:
{Na hakika tuliwapa Wana wa Israili Kitabu na hukumu na Unabii, na tukawaruzuku vitu vizuri vizuri, na tukawafadhilisha kuliko walimwengu wote} [AJ JATHIYAH 16] inatupa habari kuhusu ukubwa wa kutoa neema zake Mola Mtukufu kwa waja wake hawakulinda shukrani ya neema ya Mungu baada ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kusema: {Mwenye kutenda mema basi ni kwa ajili ya nafsi yake, na mwenye kutenda uovu ni juu yake mwenyewe. Kisha mtarudishwa kwa Mola wenu Mlezi} [AJ JATHIYAH 15]. Maneno haya yanatupatia mfano wa wale Mwenyezi Mungu aliwalipa kutokana na waliyoyafanya miongoni mwa wana wa Israil baada ya kupewa Kitabu Hekima na Utume na Mwenyezi Mungu akawaruzuku vilivyovizuri na kuwafadhilisha kwa viumbe wengine wa zama zao, huenda ukafahamu kuwa Aya Tukufu haina – kabisa – ndani yake kinachoonesha umaalumu kwao kama anavyodai mwenye kudai bali utakuta Aya mbili zinazofuata zinaashiria tofauti yao katika dini na hukumu ya hilo linarejea kwa Mwenyezi Mungu siku ya Kiyama watahesabiwa kwa matendo yao na wala Mola wako hatomdhulumu yeyote, kisha ni juu yako – ewe Nabii wa Mungu na kila mwenye kutaka haki katika dini – kulazimika na kile Mwenyezi Mungu alichokifunua kwako miongoni mwa Sharia za haki bila ya kuwageukia wale wasiojua kitu.
Soma kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu – baada ya Aya Iliyopita:
{Na tukawapa maelezo wazi ya amri. Basi hawakutafautiana ila baada ya kuwajia ujuzi, kwa ajili ya uhasidi uliyo kuwa baina yao. Hakika Mola wako Mlezi atahukumu kati yao Siku ya Kiyama katika mambo waliyo kuwa wakitafautiana * Kisha tukakuweka wewe juu ya Njia ya haya mambo, basi ifuate, wala usifuate matamanio ya wasio jua kitu * Kwa hakika hao hawatakufaa kitu mbele ya Mwenyezi Mungu. Na hakika wenye kudhulumu ni marafiki wao kwa wao. Na Mwenyezi Mungu ni rafiki wa wamchao} [AJ JATHIYAH 17-19].
Ama Aya ya pili ambayo ni kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:
{Na tulimtunukia (Ibrahim) Is-haq na Yaaqub. Na tukajaalia katika kizazi chake Unabii na Kitabu, na tukampa malipo yake katika dunia; naye hakika Akhera bila ya shaka ni katika watu wema} [AL ANKABUUT 27].
Yenyewe inaonesha kuwa hakuna kizuizi cha kutokea Utume kwenye kizazi cha Mzee Ibrahimu – na Ismail ni miongoni mwao – Aya inazungumza kuhusu zawadi ya Mwenyezi Mungu – Mtukufu – kwa Mzee Ibrahimu A.S Is-haq na Yakoub na akafanya Utume na Kitabu katika kizazi cha Mzee Ibrahimu A.S na Mzee Ibrahimu ndio Baba wa Is-haq na Ismail, vile vile Utume ni katika kizazi chake kwa watoto wote wa Is-haq na watoto wa Ismail.
Pili: Ismail ndani ya Qur`ani Tukufu:
Maelezo ya utangulizi kuhusu Ismail A.S na kutambulika Utume wake ni maelezo ya Qur`ani kwenye Aya nyingi. Mwenyezi Mungu Amesema:
{Na tukamtunukia (Ibrahim) Is-haq na Yaakub. Kila mmoja wao tulimuongoa. Na Nuhu tulimuongoa kabla. Na katika kizazi chake tuliwaongoa Daud na Suleiman na Ayyub na Yusuf na Musa na Harun. Na hivi ndivyo tunavyo walipa wafanyao wema * Na Zakaria na Yahya na Isa na Ilyas. Wote walikuwa miongoni mwa watu wema * Na Ismail, na Al-Yasaa, na Yunus, na Luut. Na wote tuliwafadhilisha zaidi ya walimwengu wote} [AL AN'AAM 84- 86].
Kisha Mola Mtukufu Akasema baada ya hayo:
{Hao ndio tulio wapa Vitabu na hukumu na Unabii. Ikiwa hawa watayakataa hayo, basi tumekwisha yawakilisha kwa watu wasio yakataa} [AL AN'AAM 89].
Na Mwenyezi Mungu Akaendelea kusema:
{Na nani atajitenga na mila ya Ibrahim isipokuwa anayeitia nafsi yake katika upumbavu? Na kwa yakini Sisi tulimteuwa yeye katika dunia; na hakika yeye Akhera atakuwa miongoni mwa watu wema * Na Mola wake Mlezi alipo mwambia: Silimu, Nyenyekea! Alinena: Nimesilimu, nimenyenyekea kwa Mola wa walimwengu wote * Na Ibrahim akawausia wanawe, na pia Yaaqub: Enyi wanangu! Hakika Mwenyezi Mungu amekuteulieni Dini hii; basi msife ila nanyi mmekuwa Waislamu, wanyenyekevu * Je! Mlikuwepo yalipo mfikia Yaaqub mauti, akawaambia wanawe: Mtamuabudu nani baada yangu? Wakasema: Tutamuabudu Mungu wako na Mungu wa baba zako, Ibrahim na Ismail na Is- hak, Mungu Mmoja tu, na sisi tunasilimu kwake} [AL BAQARAH 130-133].
Tatu: Ni kwa nini Utume haupo kwa watoto wa Ismail?
Ndani ya Kitabu Kitakatifu hakuna dalili hata moja ya kuhusishwa wana wa Israil peke yao na Utume wala pingamizi la Utume kuwa kwa watoto wa Ismail kwa sababu ni watoto wa Ismail.
Ni kwanini utenganisho huu kati ya kizazi cha Is-haq na Ismail? Je kuna kuna kosa lolote Ismail ameifanya anastahiki adhabu Yeye peke yake bali na kizazi chake? Uadilifu wa Mungu upo wapi kuwajumuisha watoto – ikiwa tutakiri kuwa Ismail amefanya makosa pamoja na kuwa hajafanya hayo makosa – hali ya kuwa hawahusiki? Au ni muendelezo wa msingi wa kurithi makosa ambayo akili haikubali yenye yakini na uadilifu pamoja huruma za Mungu kuongezea pia hata kukubalika na dini za mbinguni? Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu Anajua zaidi pale anapoweka Ujumbe wake, ikiwa atateua – naye ndio mfadhilishaji – kwishilizia Utume kwa kizazi kinachotokana na Ismail A.S basi hakuna kinachozuia uteuzi wake na matakwa yake.
Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema:
{Na kilipo wajia Kitabu kitokacho kwa Mwenyezi Mungu kinacho thibitisha waliyo nayo - na wao walikuwa wakitafutia ushindi kuwashinda makafiri - yalipo wajia yale waliyo kuwa wakiyajua waliyakanusha. Basi laana ya Mwenyezi Mungu juu ya wakanushao!} [AL BAQARAH 89].
Akaendelea kusema Mola Mtukufu:
{Na alipo wajia Mtume kutoka kwa Mwenyezi Mungu, mwenye kuthibitisha yale waliyo nayo, kundi moja miongoni mwa wale walio pewa Kitabu lilitupa Kitabu cha Mwenyezi Mungu nyuma ya migongo yao kana kwamba hawajui} [AL BAQARAH 101.
Nne: Kusudio la kufadhilishwa kwa wana wa Israil zaidi ya watu wengine:
Kufadhilishwa kwa wana wa Israil zaidi ya watu wengine – ndani ya zama zao – ni kwa sababu Mwenyezi Mungu aliwakusanyia kati ya msimamo wa dini na maadili na kati ya kujihukumu wao wenyewe kwa wenyewe, na akaeneza uadilifu wa kwanza kwao na kati ya maisha mema usalama na ustawi, wakati watu wengine walikuwa katika maisha ya kitajiri lakini kilichopungua kwao ni msimamo wa dini na maadili na baadhi yao walikosa amani kwa sababu ya uwingi wa fitina, na kusudio la walimwengu ni mataifa ya zama zao na yote hayo ni kutoa habari ya yaliyopita kuhusu wana wa Israil katika nguvu ya mambo yao na wala si kwa yale yaliyoelekewa na mambo yao baada ya kutafautiana kufifia mambo yao pamoja na kufutika Sharia zao ( ).

 

Share this:

Related Fatwas