Uke katika Idadi na Uwingi wa Kinachohesabiwa
Question
Aya ya Qur'ani:
Mola Amesema: {Na tuliwagawanya katika makabila kumi na mbili, mataifa mbalimbali} {AL-AARAF: 160}.
Mlalamikaji anasema nini?
Answer
Ilipasa idadi iwe kwa kiwakilishi jina cha kiume na kinachohesabiwa kiwe kwenye umoja, na tuseme kabila kumi na mbili ( ).
Shaka
Aya Tukufu imekuja kinyume na kanuni mbili katika kanuni za lugha katika mlango wa idadi, kanuni ya kwanza ni idadi kuwa dhamiri ya kiume kwa sababu idadi ya kiume, na idadi ya “Ithnain” mbili inakubaliana na kinachohesabiwa kiwe cha kiume au cha kike, na “Thaaniyah” mbili ni kuwa kinachohesabiwa kinapaswa kiwe katika umoja lakini Aya imekuja kwa dhamiri ya wingi.
Kuondoa shaka
Irabu ya Aya Tukufu sio kama alivyotaja muulizaji kwani “Asbaatan” kwa maana ya makabila sio upambanuzi wa idadi ya “Ithnataa Asharata” kwa maana ya kumi na mbili mpaka iwajibike kwenye idadi kuwa ya kiwakilishi jina cha kiume na katika upambanuzi wa umoja kama alivyotaja, hivyo upambanuzi wa idadi umeondoshwa ( ) kwa dalili ya kitenzi cha “Tuliwagawanya” na upambanuzi unakuja ili kuondoa kisichofahamika, na kwa ufahamu huu hakuna kisichofahamika mpaka uhitajike upambanuzi.
Miongoni mwa faida za kilugha kwenye utaratibu huu
Kwanza: Ufupisho ambapo umeondoshwa upambanuzi kwa kitenzi cha “Tumewagawanya”.
Pili: Aya Tukufu imeanza na kitenzi “Qattaanaa hum” kwa maana ya tumewagawanya kwa kutumika alama ya kukaza kwenye herufi ya Taa, na ukazaji huu unamaanisha uwingi, kwa maana uwingi wa kugawanyika na kugawa makundi, na hii inakubaliana na uwingi, na lugha ya Qur'ani ni pana sana zaidi ya kanuni za lugha na utaalamu wake wa kibalagha.
Tatu: Uwingi wa “Asbaatan” na kuelezea kwa kauli yake “Umamaa” kwa maana ya mataifa, lau neno “Asbaat” kwa maana ya makabila ni upambanuzi basi angesema: Kabila kumi na mbili, basi ingekuwa maelezo ni pungufu na haifai kwenye uandishi wa kielimu zaidi, kwa sababu jina “Sabtu” husadikiwa moja, hivyo yanakuwa makabila ya Nabii Yakoub ni watu kumi na mbili tu, na hii ni uwingi wa makabila na akasema baada ya hapo “Umamaa” kwa maana ya mataifa kwa sababu Umma ni kundi kubwa, na lilikuwa kila kundi katika makabila ya Nabii Yakoub kundi kubwa.
Nne: Na kila kundi au kabila katika makundi hayo limekuwa ni Umma, kwani Mwenyezi Mungu Amesema: {Na kumbukeni mlipokuwa wachache, naye akakufanyeni kuwa wengi} {AL-AARAF: 86} pamoja na kufahamika kwake neno makundi au makabila kwa utukuzo wao, kwa sababu makabila hapa ni makabila ya watoto wa Ishaka Ibn Ibrahimu amani ya Mwenyezi Mungu iwe kwao ( ).