Uharamisho wa Miezi Mitakatifu

Egypt's Dar Al-Ifta

Uharamisho wa Miezi Mitakatifu

Question

Shubha:
Miezi Mitakatifu ilikuwapo kabla ya Uislamu, Na dini ya Uislamu imechukua uharamisho wa miezi hiyo kutoka kwa Waarabu wa zama za Jahiliya, na Mtume Mohammad S.A.W. aliona Uharamisho huu unakinzana na utashi wake katika vita na kulipiza kisasi dhidi ya maadui zake na akapitisha Utukufu wa miezi hiyo kama ilivyotajwa katika Suratu AT TAWBAH: {Na ikisha miezi Mitukufu basi wauweni washirikina popote mwakutapo, na washikeni na wazungukeni, na wavizieni katika kila njia. Lakini wakitubu, wakashika Swala, na wakatoa Zaka, basi waachilieni. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu} [AT TAWBAH 5]
Na hakika yeye mwenyewe anakinzana na kauli yake katika Suratu AL BAQARAH pia: {Wanakuuliza juu ya kupigana vita katika Mwezi Mtakatifu. Sema: Kupigana vita wakati huo ni dhambi kubwa. [AL BAQARAH 217]
 

Answer

 Kituo cha Tafiti za Kisheria katika Ofisi ya Kutoa Fatwa ya Misri.
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Uislamu unalenga kuharamisha damu na kupinga Uadui.
Ya Kwanza: Hakika Uislamu kupitisha uharamu wa Miezi mitakatifu kulikuwa katika mlango wa kulinda maisha na kutoyateketeza bila ya haki kwani Dini hii Takatifu kwa jinsi ilivyo inalenga kulinda damu za watu – miongoni mwa wafuasi wake na wengine pia- Kuuawa bila haki hakuna ubaya ikiwa malengo yake makuu ni kuilinda nafsi. Lakini ni ipi dhana ya kwamba ikiwa Uislamu umeharamisha kuwashambulia watu kivita juu ya wafuasi wake nayo ikawashambulia? Je, inafaa ikiwa atawashambulia wasimame wakiwa wamepokonywa Utashi wao na hawawezi kujilinda? Hapana, Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema: {Mwezi Mtakatifu kwa Mwezi Mtakatifu. Na vitu vitakatifu vimewekewa kisasi. Anaye kushambulieni nanyi mshambulieni, kwa kadiri alivyo kushambulieni. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Na jueni kwamba Mwenyezi Mungu yupo pamoja na wachamngu.} [AL BAQARAH 194]
Na maana yake ni kutokana na Utukufu wa Mwezi Mtukufu haikupiganwa vita ndani yake wakalipokea hilo kwa kuutukuza Mwezi Mtukufu na wakazuia umwagaji damu za watu na waliovuka mipaka yenu wajibuni kwa kiasi cha walichokifanya na haikudhuruni nyinyi kufanya hivyo katika wakati wowote ule.
Miezi Mitakatifu imetukuzwa, lakini Utukuzo wa nafsi ni mkubwa Zaidi:
Ya Pili: Na kwa taarifa hii iliyotangulia imebainika ya kwamba hukumu ya Qur'ani Tukufu kuhusu vita ndani ya miezi Mitukufu ni moja tu. Haikutofautiana kutoka sehemu kwenda sehemu nyingie bila ya kuondosha chochote ndani yake, ukisoma Aya kama kipengele kimoja bila ya kukata sehemu yake yoyote. Na kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Wanakuuliza juu ya kupigana vita katika Mwezi Mtakatifu. Sema: Kupigana vita wakati huo ni dhambi kubwa. Lakini kuzuilia watu wasiende katika Njia ya Mwenyezi Mungu na kumkanusha Yeye, na kuzuilia watu wasiende kwenye Msikiti Mtakatifu na kuwatoa watu wake humo, ni makubwa zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu. Na fitina ni mbaya zaidi kuliko kuuwa. Wala hawataacha kupigana nanyi mpaka wakutoeni katika Dini yenu kama wakiweza. Na yeyote katika nyinyi akiacha Dini yake akafa naye ni kafiri, basi hao ndio ambao a'mali zao zimeharibika duniani na Akhera. Na hao ndio watu wa Motoni; humo watadumu} [AL BAQARAH 217].
Basi Aya inasimulia swali na jibu; swali kuhusu Mwezi Mtakatifu, Na jibu linatosheleza utukuzaji kosa la kuua ndani yake lakini atakayeshambulia na akamwaga damu au akavishambulia vitakatifu vya Nyumba ya Mwenyezi Mungu na kuwatoa watu wake humo kosa lake ni kubwa mno mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. Yaani {Wanakuuliza} juu ya kupigana vita katika Mwezi Mtakatifu, {Sema: Kupigana vita wakati huo ni dhambi kubwa}, lakini kuzuia njia ya Mwenyezi Mungu na kuzuia Msikiti Mtukufu na Kuufanyia ukafiri ni kukubwa kuliko hayo mapigano. {Wala hawataacha kupigana nanyi mpaka wakutoeni katika Dini yenu kama wakiweza}, Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu amebainisha kwamba lengo lao kutoka katika swali hilo ni kupigana na Waislamu, halafu Mwenyezi Mungu Mtukufu ameteremsha baada ya hayo kauli yake: {{Mwezi Mtakatifu kwa Mwezi Mtakatifu. Na vitu vitakatifu vimewekewa kisasi. Anaye kushambulieni nanyi mshambulieni, kwa kadiri alivyo kushambulieni}, Kwa hivyo, ametaja katika Aya hiyo kwamba mapigano ni kwa lengo la kuwalinda watu na mali na uhalali wake. [Tazama kitabu cha: Mafatehu Al Ghaibu 30/6].
Msimamo wa Uislamu kutoka katika Mila na Desturi za watu na Tamaduni zao:
Ya Tatu: Je, ni lazima kwa Uislamu kuharamisha kila desturi – nzuri au mbaya – iliyokuwepo kabla ya Ujumbe wa Mtume S.A.W? Je huko sio kutoka katika Njia sahihi sisi kuja na Mila na Desturi za watu na tamaduni zao ambazo hazina madhara yoyote bali zinaweza kuleta faida za kibinadamu, tukaziharamisha na kuzitia makosani? Hakika Uislamu unatufundisha sisi kuyapitisha na kuyakubali waliokuwa nayo Waarabu katika kuifanya Miezi hii kuwa Mitakatifu, tuikiri Haki hata kama chanzo chake ni kutoka kwa wengine, na tusimame pamoja na haki hata kama haikuwa upande wetu, na tunufaike na kila jaribio (zoezi) la kibinadamu lenye manufaa bila kumjali mtendaji.
Ya Nne: Utukufu wa Miezi mitakatifu haukuwepo wakati wa Waarabu tu bali ulikuwepo pia katika Sharia ya Ibrahim A.S, na uliendelea kuwepo mpaka ulipokuja Uislamu Wenye Dini ya kumtakasia Mwenyezi Mungu Mtukufu ikaupitisha na kuharamisha ukiukwaji wa aina mbalimbali kama walivyofanya Waarabu.

Share this:

Related Fatwas