Adhabu ya Firauni kwa Watu wa Musa

Egypt's Dar Al-Ifta

Adhabu ya Firauni kwa Watu wa Musa

Question

 Andiko lenye Shaka:
Ndani ya Qur`ani Tukufu Aya zimekuja:
{Wakasema waheshimiwa katika watu wa Firauni: Unamuacha Musa na watu wake walete uharibifu katika nchi na wakuache wewe na miungu yako? Akasema: Tutawauwa watoto wao wa kiume, na tutawaacha hai watoto wao wa kike. Na bila ya shaka sisi ni wenye nguvu kwao} [AL-A'ARAF: 127].
Na kauli yake Mola Mtukufu:
{Hakika Firauni alifanya kiburi katika nchi, na akawagawa wananchi makundi mbali mbali. Akalidhoofisha taifa moja miongoni mwao, akiwachinja watoto wao wa kiume na akiwaacha watoto wao wa kike. Hakika yeye alikuwa katika mafisadi * Na tukataka kuwafadhili walio dhoofishwa katika nchi hiyo na kuwafanya wawe viongozi na kuwafanya ni warithi * Na kuwapa nguvu katika nchi, na kutokana na wao kuwaonesha kina Firauni na Hamana na majeshi yao mambo yale waliyo kuwa wakiyaogopa * Tulimfunulia mama yake Musa kwa kumwambia: Mnyonyeshe. Na utakapo mhofia basi mtie mtoni, na usihofu wala usihuzunike. Hakika Sisi tutamrudisha kwako na tutamfanya miongoni mwa Mitume} [AL-QASAS: 4 – 7].
Katika Suratul-Aaraf Sura inasema kuwa Wamisri walilalamika kwa Firauni kutokana na vitendo vya Musa, hivyo Farauni akachukuwa uamuzi wa kuuwa watoto wa changa wa kiume wa Kiibrania na kuwaacha hai watoto wachanga wa kike, na katika Suratul-Qasas inamzungumzia Firauni kabla ya kuzaliwa kwa Musa kuwa aliamrisha kuchinjwa kwa watoto wachanga wa kiume na kuachwa hai watoto wachanga wa kike mpaka mama wa Musa akafikwa na hali ya wasi wasi mkubwa kuhusu mtoto wake wa kiume ambaye ni Musa mwisho akaamua kumficha kwenye kisanduku ( ) mpaka akaokotwa na kuchukuliwa na familia ya Firauni.
Na kwa maelezo haya Aya hizi mbili zinagongana, kwa sababu Aya ya kwanza inasema Firauni aliwaahidi watu wake kuwa atauwa watoto wachanga wa kiume wa wana wa Israil na kuwaacha hai watoto wao wachanga wa kike baada ya Musa A.S kupewa Utume na kuonekana mambo yake na kuwa na wafuasi wake, wakati Aya ya pili inasema kuwa hayo yametokea kabla ya kuzaliwa kwa Musa A.S na huu ni mgongano.

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Hakuna mgangano kati ya Aya hizi mbili, kwa sababu hii imerudia kwa Firauni katika hali zote mbili na hakuna jambo la ajabu katika hilo, kwani Aya zote mbili zilizopo hapa zimekusanya ahadi ya Firauni kwa Musa na watu wake, kwani kauli ya Aya ya kwanza: {Tutawauwa watoto wao wa kiume…} na kauli ya Aya ya pili: {Akalidhoofisha taifa moja miongoni mwao, akiwachinja watoto wao wa kiume na akiwaacha hai watoto wao wa kike…} lakini ahadi hii ilikuwa na hali mbili tofauti, kwani kwenye Aya ya kwanza: Ilikuwa ni baada ya kuonekana wito wa Musa A.S na baadhi ya wana wa Israil kuanza kumuamini, na Aya ya pili ilikuwa ni kabla ya kuzaliwa kwa Musa A.S kwa muda mdogo tu au wakati wa kuzaliwa kwake, na hii inafahamika kutokana na muundo wa Aya, na ahadi mbili ni aina moja, na inafahamika hili ni kwa vile Firauni alikuwa akifanya vitendo vya aina hii kwa nyakati tofauti, kwani alifanya kabla ya kuzaliwa kwa Musa A.S ili kujiridhisha kumuuwa huyo kijana ambaye Firauni alifahamu kuwa huenda atachukuwa ufalme wake, alipofanikiwa kuuwa watoto wengi ni kana kwamba alijiridhisha kuwa atakuwa ameshamuuwa huyo mtoto na akaamua kuacha adhabu hii ambayo watu wa Musa walikuwa wanaionja, kisha alipozaliwa Nabii Musa S.A na Mwenyezi Mungu Mtukufu akapanga kumuokoa na kifo hiki na akampa Utume na kudhihirisha wazi ulinganiaji wake ndipo alipostukizwa Firauni jambo hili limemtoka mikononi mwake hivyo akaanza kuweka mipango ya kumaliza tatizo hili kwa kurudia tena adhabu zake za kuuwa, na hii ndio kauli ya Jamhuri ya Wanachuoni wa Tafasiri.
 

Share this:

Related Fatwas