Qaruun.

Egypt's Dar Al-Ifta

Qaruun.

Question

 Andiko lenye Shaka:
Ndani ya Qur`ani Tukufu imekuja:
Hadi kwenye kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:
{Hakika Qaruni alikuwa katika watu wa Musa, lakini aliwafanyia dhuluma. Na tulimpa hazina ambazo funguo zake zinawatopeza watu wenye nguvu kuzichukua. Walipo mwambia watu wake: Usijigambe! Hakika Mwenyezi Mungu hawapendi wanao jigamba…… Basi tukamdidimiza yeye na nyumba yake katika ardhi; wala halikuwepo kundi lolote la kumnusuru kwa Mwenyezi Mungu, wala hakuwa miongoni mwa wanaojitetea} [AL QASAS: 76: 81].
Inafahamika kuwa Qarun aliyetajwa ndani ya Qur`ani ni Croesus, mfalme wa Lydia 546 – 560 BC naye ni alama ya utajiri kwa Waarabu na wasiokuwa Waarabu, wala hakuna kinachoelezea kuchanganyika kwake na Sores ambaye ametajwa ndani ya Taurat, hakuna uhusiano wa Qar`ani na Sores ambaye kwa kushirikiana na Dathan na Abiram walilipiza kisasi dhidi ya Musa ndipo ardhi ikafungua mdomo wake na kuwameza.
Ni wazi kuwa Qur`ani Tukufu imechanganya bila ya sababu yeyote kati ya Qarun ambaye ndio Croesus na Sores ambaye alishirikiana na Dathan pamoja na Abiram kumfanyia kisasi Musa.

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Kisa ambacho kimetajwa na Aya za Qur`ani ni kisa cha Qarun ambaye amekuwa ni alama ya utajiri mwenye kiburi asiyetoa haki ya Mwenyezi Mungu katika mali yake, bali anafanya jitihada ya kueneza uharibifu kwenye ardhi, na kugawanyika watu pembezoni mwake, kisha Mwenyezi Mungu akamfanya alama kwa watu wake na kwa ulimwengu mpaka siku ya Kiyama, na kubainisha kuwa maisha ya Akhera na mwisho mwema vimeandaliwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa ajili ya wacha-Mungu, na Qur`ani imetosheka kwa kutaja jina la Qarun tu.
Ama Croesus aliyetajwa nyinyi mnasema kuwa yeye ni alama ya utajiri, huyo sio kusudio la Aya bali kusudio la Aya ni kuwa mtu alikuwa tajiri na wakati huo huo alikuwa mwingi wa kibri, hivyo Mwenyezi Mungu akamzamisha kwenye ardhi.
Ama kauli kuwa jina lake ni Sores kuna uwezekano kuwa ni Sores aliyetajwa ndani ya Taurat, na inawezekana kuwa jina la mtu mwingine, na hii inakuwa ni katika mfanano wa majina, na Wanachuoni wamesema: Jina la Qarun ni jina la Kiarabu, na katika lugha ya Kiibrania ni Sores, na ikatokea kwenye kulifanya la Kiarabu mabadiliko ya baadhi ya herufi zake kwa lengo la kurahisisha, na ukafanyika wizani wake kwa muundo wa wizani wa Kiarabu kama vile jina la Twaluut na Jaalut ( ).

Share this:

Related Fatwas