Kisa cha Nabii Musa na Khidiri

Egypt's Dar Al-Ifta

Kisa cha Nabii Musa na Khidiri

Question

 Ndani ya Qur`ani Tukufu imekuja kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:
{Na pale Musa alipo mwambia kijana wake: Sitoacha kuendelea mpaka nifike zinapo kutana bahari mbili, au nitaendelea kwa muda mrefu……. Wala Mimi sikutenda hayo kwa amri yangu. Hiyo ndiyo tafsiri ya hayo ambayo wewe hukuweza kuyasubiria} [AL-KAHF: 60 – 82].
Imekuja kwenye tafasiri ya Aya hizi kuwa: Musa Amani ya Mungu iwe kwake alisafiri akiwa na mtoto wake Joshua Ibn Nun mpaka wakafika kwenye jiwe wakiwa na samaki wa kuchoma, wakati wapo kwenye lile jiwe Joshua alitawadha mara yule samaki wa kuchoma akadondokewa na matone ya maji ya kutawadha yule samaki akarudi kuwa hai na kuingia majini na kuondoka, wakati Nabii Musa alipoulizia samaki ili apate kula hakumpata, walipoamua kurudi ile sehemu ya jiwe ndipo walipomkuta Khidhri naye ni Nabii Eliya, waliondoka pamoja kisha wakapanda chombo Khidhri akakiharibu, kisha akamuua mtoto, kisha akajenga ukuta uliokuwa unataka kudondoka, na ukuta huu ulikuwa ni wa watoto wawili yatima, ulijengwa na baba yao kwa ajili yao ili watakapo kuwa wakubwa wakute chini ya huo ukuta dhahabu iliyohifadhiwa, na dhahabu hizo zilikuwa zimeandikwa baadhi ya maneno ya hekima, miongoni mwa maneno hayo ni pamoja na neno: “Hakuna mola wa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu. Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu” na hiyo ilikuwa ndani ya zama za Iskandar Zul-Qarnayn.
Kisa hiki kinaweka wazi kuwa Qur`ani Tukufu imekwenda kinyume na matukio ya historia, kwa sababu Musa aliishi nchini Misri mwaka 1500 BC, na Eliya – ambaye anaitwa Khidhri – aliishi nchini Palestina mwaka 900 BC, na Iskandar Mkubwa aliishi nchini Ugiriki mwaka 332 BC, hivyo upo wapi ushahidi wa hawa kwa Muhammd ambaye alitokea ndani ya nchi ya Kiarabu wakati wa karne ya saba AB baada ya kuzaliwa kwa Nabii Isa?!!
Na vipi inawezekana kwa hawa ambao wamekulia kwenye falme tofauti na ndani ya karne zilizopishana sana wakutane ndani ya wakati mmoja na kwa upande mmoja?!!

Answer

 Kituo cha tafiti za Kisharia Ofisi ya Mufti wa Misri.
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:

Tafasiri ya kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Basi wakamkuta mja katika waja wetu} kuwa huyu mja ndio Khidhri Amani ya Mola iwe kwake ni kauli thabiti na sahihi, lakini Khidhri Amani ya Mungu iwe kwake ndio Eliya Ibn Malakan – wala sie Eliya kama ilivyotajwa – swala la Khidhri ndio Eliya si sahihi.
Ama kauli ya kuwa Zil-Qarnayn ndio Iskandar Mkubwa 324 – 356 BC, kisa hiko hakijafikiwa na uhakiki wa kihistoria…bali Wafasiri ambao wamekielezea kisa hiki wamejenga shaka kwenye ukweli wake na usahihi wake….kwa sababu uthibiti wa kihistoria ni kuwa Iskandar Al-Maqduny alikuwa ni mfalme wa kipagani, na Zul-Qarnayn alikuwa ni mtu mwema kumekuwa na tofauti kwenye Utume wake.
Ama kauli ya Wafasiri: Chini ya ukuta kulikuwa kumehifadhiwa dhahabu iliyoandikwa baadhi ya maneno ya busara na hekima miongoni mwa maneno hayo ni: “Hakuna mola wa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu. Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu” jambo hilo halina ugeni wala mshangao kwa sababu Manabii wengine walibashiri ujio wa Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W kutokana na dini yao ni moja hata kama kutakuwa na Sharia tofauti kidogo, hivyo kauli hii kama haitokuwa dhaifu kinachochukuliwa ni uwepo wa mfanano kati ya Sharia za mbinguni.
Ama kauli kuwa samaki alikuwa amechomwa hatupingi kuwepo muujiza kama huu kwa Nabii Musa Amani ya Mwenyezi Mungu iwe kwake.

Share this:

Related Fatwas