Mlezi wa Nabii Musa

Egypt's Dar Al-Ifta

Mlezi wa Nabii Musa

Question

Imekuja ndani ya Qur`ani Tukufu kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:
{Na mkewe Firauni alisema: Atakuwa kiburudisho cha macho kwangu na kwako. Msimuuwe! Huenda akatufaa, au tumpange kuwa mwenetu. Wala wao hawakutambua} [AL QASAS: 09].
Hapa tunaona tofauti kati ya Qur`ani na Kitabu Kitakatifu kuhusu mwanamke aliyemchukuwa Musa na kumlea, kwani Qur`ani hapa imekwenda kinyume na ukweli wa kihistoria uliothibitishwa na Kitabu Kitakatifu nao ni kuwa mwanamke ambaye alimchukuwa Musa Amani ya Mungu iwe kwake na kumlea ni binti wa Firauni na wala sio mke wake kama ilivyokuja ndani ya Qur`ani, na imekuja katika Kitabu Kitakatifu kuwa binti wa Firauni alikwenda mto naili kwa lengo la kuoga – kwa sababu walikuwa wanauzingatia ni mungu unawatakasa na uchafu – ndipo alipoona kisanduku kidogo tahamaki ndani yake kuna mtoto analia, ndipo binti wa Firauni alipomchukuwa yule mtoto na kuwa mtoto wake. Na Musa amesema katika Kitabu cha [Kutoka 2: 5 – 15]. Huyo ndio binti wa Firauni, na Yeye Musa ndiye anajua zaidi nani aliyemlea.
 

Answer

Kituo cha tafiti za Kisharia Ofisi Kuu ya Mufti wa Misri.
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Kuna tofauti kati ya muokotoji na mlezi. Qur`ani inasema: Muokotoji ni watu wa familia ya Firauni, na hii ni wote inakusanya mke wake na wengine, wala Qur`ani Tukufu haikusema kuwa mlezi ni binti wa Firauni au mke wa Firauni, kwani Aya Tukufu haioneshi kuwa mke wake ndiye ambaye alimlea Nabii wa Mungu Musa Amani ya Mungu iwe kwake bali Aya inaelezea kauli ya mke wa Firauni alipomuokota Musa Amani iwe kwake akasema:
{Ni kiburudisho cha macho kwangu na kwako. Msimuuwe! Huenda akatufaa, au tumpange kuwa mwenetu. Wala wao hawakutambua} hivyo Aya inakiri kuwa wao ni wenye makosa kumuokota na kutaraji watanufaika naye.
Ama kauli kuwa ambaye amemlea Musa ni binti wa Firauni ni hoja inayohitaji uthibitisho wa kihistoria, na ni jambo gumu kuthibitisha kwake, hivyo basi ni jambo linalokadiriwa, na kutokana na hili hakuna mgongano wala mpishano kati ya Qur`ani na yaliyotajwa ndani ya Kitabu Kitakatifu kuhusu maudhui hii.

 

Share this:

Related Fatwas