Vipi Shetani Amchome Mtume S.A.W.?!...

Egypt's Dar Al-Ifta

Vipi Shetani Amchome Mtume S.A.W.?!

Question

Matni yenye shaka
Imekuja katika Qur`ani neno lake Mwenyezi Mtukufu: {Na uchochezi wa Shet'ani ukikuchochea basi omba ulinzi wa Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye ni Msikizi, Mjuzi. Hakika wale wamchao Mungu, zinapowagusa pepesi za shetani, mara huzindukana na hapo huwa wenye kuiona haki. Na ndugu zao wanawavutia kwenye upotofu, kisha wao hawaachi} [AL A'RAAF: 200-202].
 

Answer

 Na imekuja Hadithi: “kila mwanadamu anapozaliwa shetani humchoma katika ubavu wake, basi hupiga kelele isipokuwa mtoto ya Maryam {Isa bin Maryam} alikuja kumchoma akachoma kwenye pazia”.
Nasi tunauliza: Ibilisi anamfuata Mtume wa Uislamu S.A.W. na anamchoma, basi vipi anakuwa Mtume?! Tofauti iliyoje kati yake na Masih ambaye Hadithi inakiri kuwa shetani alipokuja kumchoma akachoma pazia, na aliyoyasema Petro mtume: “Yeye alikwenda huko na huko akitenda mema na kuwaponya wote waliokuwa wamevamiwa na Ibilisi” {Matendo 10:34}.
Kuondoa shaka;
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Je! Shetani anaweza kuwatawala Mitume:
Shetani hana utawala kwa mitume ambao Mwenyezi Mungu amewalinda kutokana na upotevu wake, lakini kuna tofauti kubwa kati ya kupoteza na majaribio ya kuwatia wasiwasi na uchochezi, na Aya Tukufu inazungumzia jaribio endelevu la shetani la kutia wasiwasi, na inamfundisha mtume bali inamfundisha kila anayepitiwa na wasiwasi kama huu wa shetani aundoe kwa kujilinda kwa Mwenyezi Mungu Msikivu Mjuzi.
“Shetani hakati tama katika kuwatia wasiwasi Mitume; kwa sababu hilo lipo kwenye tabia yake, na anawawinda katika maeneo yaliyojificha makusudio yake akitumaini mmoja wao aanguke, ijapokuwa anajua kwamba hawezi kuwapoteza lakini hakati tama ya kuwafanya wazembee kutekeleza wajibu wao, lakini akihisi wasiwasi huuondoa, kwa hivyo Mtume S.A.W. amefundisha kutaka msaada kwa Mwenyezi Mungu katika kujikinga na sheatani katika Aya iliyotangulia”.
Injili inazungumzia jaribio la Shetani kwa Masih Issa bin Maryam:
Na katika mlango huu ni yale yanayotuhadithia Injili kuhusiana na jaribio la Ibilisi kwa Masihi Isa bin Marayam ambapo imekuja katika Injili:
“Baada ya Yesu kufunga kwa siku arobaini mchana na usiku, akaumwa njaa sana. Mjaribu akamwendea na akasema, “Ikiwa wewe ni Mwana wa Mungu, basi yaamuru mawe haya yawe mikate. Yesu akajibu, “Maandiko yanasema, ‘Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila Neno linalotoka katika kinywa cha Mungu. Kisha Shetani alimwongoza Yesu mpaka mji mtakatifu wa Yerusalemu na akamweka juu ya mnara wa Hekalu. Akamwambia Yesu, “Ikiwa wewe ni Mwana wa Mungu, jirushe mpaka chini! Kwani Maandiko yanasema, ‘Mungu atawaamuru Malaika zake wakusaidie,
na mikono yao itakupokea, ili usije ukajikwaa mguu wako kwenye jiwe. Yesu akamjibu, “Pia, Maandiko yanasema, ‘usimjaribu Bwana Mungu wako. Kisha Shetani akamwongoza Yesu mpaka kwenye kilele cha mlima ulio mrefu sana na kumwonesha falme zote za ulimwengu na vitu vya kupendeza vilivyomo ndani. Shetani akamwambia Yesu, “Ukiinama na kuniabudu, nitakupa vitu hivi vyote.Yesu akamjibu Shetani akamwambia, “Ondoka kwangu Shetani! Kwani Maandiko yanasema, ‘Umwabudu Bwana Mungu wako na umtumikie yeye peke yake! Baada ya hayo, Shetani akamwacha. Ndipo Malaika wakaja kumhudumia” {Matayo:1-11}.
Angalia jinsi gani Ibilisi hakukata tamaa kwa Masihi?! Hii ndio maana ya uchochezi ambayo imekuja katika Qur`ani na ambayo imemsemesha Muhammad S.A.W.
Je! Masihi pekee ndiye aliyelindwa na kuchomwa na Shetani wakati wa kuzaliwa:
Hakuna Katika Hadithi iliyotangulia iliyotajwa kwenye swali kwamba Masihi hakaribiwi na wasiwasi wowote bali juhudi nyingi zimethibitisha kwa Hadithi ilitajwa kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu amejibu dua ya bibi yake Masihi aliposema kumwombea dua Maryam binti yake: {Na mimi nimemwita Maryamu. Nami namkinga kwako, yeye na uzao wake, uwalinde na Shet'ani aliyelaaniwa} [AAL IMRAAN: 36].
Na haimaanishi kwamba umaalumu huu haupo kwa Mtume S.A.W. –tukikubali mjadala kwa hilo - kwamba shetani anamwendesha na anaweza kujiepusha na hilo, kwamba baadhi ya Wanazuoni wa Kiislamu wemechagua kwamba Mitume yote wanashirikiana katika hilo.
Vilevile Hadithi hii haitufundishi kwamba Masihi ni bora kuliko Mtume Muhammad S.A.W. kwa sababu kuna Hadithi nyingi za ubora wa Mtume S.A.W. na kuwepo ubora wa Masihi A.S. kulikothibiti katika ulimi wa Mtume S.A.W. hakubatilishi mengi yaliyothibitisha ubora wake.

 

Share this:

Related Fatwas