Kiapo cha Upuuzi

Egypt's Dar Al-Ifta

Kiapo cha Upuuzi

Question

Imekuja katika Qur`ani Tukufu: {Mwenyezi Mungu hakushikeni kwa viapo vyenu vya upuuzi. Bali anakushikeni kwa yanayo chuma nyoyo zenu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe na Mpole} [AL BAQARAH: 225].
Na neno lake Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Anayemkataa Mwenyezi Mungu baada ya kuamini kwake - isipo kuwa aliye lazimishwa na hali ya kuwa moyo wake umetua juu ya Imani, lakini aliye kifungulia kifua chake kukataa - basi hao ghadhabu ya Mwenyezi Mungu ipo juu yao, na wao watapata adhabu kubwa} [AN NAHL:106].
 

Answer

Hivi Aya hizi hazifungui milango wa uongo? Je! tabia njema zinasimama katika uongo? Injili inasema: “Lakini watu waoga, wasioamini, wapotovu, wauaji, wazinzi, wachawi, waabudu sanamu, na waongo wote, mahali pao patakuwa ndani ya lile ziwa linalowaka moto na madini ya kiberiti; hicho ndicho kifo cha pili.” {Ufunuo 8:21}.
Kuondoa shaka;
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Kwanza: kiapo cha upuuzi ni kile ambacho kinakuja pasi na kukusudia:
Aya Tukufu iliyotolewa ushahidi kuhusiana na jambo la kiapo ndani yake kuna habari kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kusamehe yale yaliyotoka ulimini kwa waja wake kwa kuapa kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu bila ya kukusudia kiapo, kama maneno ya mja aliyoyazoea ulimini kwake: hapana naapa kwa Mwenyezi Mungu, au ndio naapa kwa Mwenyezi Mungu.
Pili: kushikwa kunakuwa kwa kukusudia:
Katika Aya hii na mfano wake katika Qur`ani Tukufu inajulikana kwamba kushika kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kunakuwa pale mja atakapo tamka kiapo kwa makusudi akiuahidi moyoni mwake, na kama hivyo katika Sharia ya Kiislamu, Mwenyezi Mungu hamshiki mja kwa kitu ambacho nafsi yake haikikusudia, Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Mwenyezi Mungu haikalifishi nafsi yoyote ila kwa kadiri ya iwezavyo. Faida ya iliyo yachuma ni yake, na khasara ya iliyo yachuma ni juu yake pia. (Ombeni:)Mola wetu Mlezi! Usituchukulie tukisahau au tukikosea. Mola wetu Mlezi! Usitubebeshe mzigo kama ulio wabebesha wale walio kuwa kabla yetu. Mola wetu Mlezi Usitutwike tusiyo yaweza, na utusamehe, na utughufirie, na uturehemu. Wewe ndiye Mlinzi wetu. Basi tupe ushindi tuwashinde kaumu ya makafiri } [286], na akasema: {Waiteni kwa baba zao, maana huo ndio uadilifu zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu. Na ikiwa hamwajui baba zao, basi ni ndugu zenu katika Dini, na rafiki zenu. Wala si lawama juu yenu kwa mlivyo kosea. Lakini ipo lawama katika yale ziliyo fanya nyoyo zenu kwa makusudi. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu} [AL AHZAAB:5].
Tatu: Kusamehe ni jambo la Rehema la Mwenyezi Mungu:
Nani anajua maana ya Rehema za Mwenyezi Mungu Mtukufu yeye anajua hali ya mwanadamu na yeye ndiye aliyemuumba katika hali ya udhaifu, ambapo mwanadamu hupatwa na usahaulifu wakati mwingine na kukosea pia, hamtii makosani mtu isipokuwa mtu akithibiti kukusudia katika kitendo chake, lau kama si hivyo, mwanadamu angeingia katika madhambi makubwa kwa sababu ya uanadamu wake, na tunaamini kwamba mwenye kuwapeleka kwa kuwakalifisha watu kwa wasiloliweza basi huyo anayabana yale ambayo Mwenyezi Mungu Mpole Mwenye kurehemu ameyawekea nafasi kwa rehema zake na fadhila zake.

 

Share this:

Related Fatwas