Kwa Nini Uislamu Umefanya Mirathi y...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kwa Nini Uislamu Umefanya Mirathi ya Mwanamke Muwa Nusu ya Mwanamume?

Question

Matni ya Shaka:
Imekuja Aya katika Qur`ani isemayo: {Mwenyezi Mungu Anakuusieni juu ya watoto wenu: Fungu la mwanamume ni kama fungu la wanawake wawili} [AN NISAA: 11].

Answer

Kwa nini Uislamu unampa mwanamke nusu ya fungu la mwanume pamoja na kwamba maisha yanakuwa baadhi ya nyakati magumu sana kwa mwanamke kuliko kwa mwanamume? Kumpa mwanamume mara mbili ya mwanamke ni katika ada za zama za kijinga.
Kuondoa shaka;
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Falsafa ya urithi katika Uislamu
Kwa hakika mirathi katika Uislamu ni mfumo uliojengewa misingi na vipimo ni vizuri tutavitaja hapa ili muulizaji afahamu misingi ya elimu hii; tofauti katika viwango vya warithi wakiume na wakike katika falsafa ya mirathi ya Kiislamu vinadhibitiwa na vipimo vitatu:
Kwanza: Daraja la udugu kati ya warithi awe mwanamke au mwanamume na kati ya marehemu anayerithiwa, kila daraja la udugu linavyokuwa karibu kiwango kinaongezeka katika mirathi, na kila udugu unavyokuwa mbali kiwango cha urithi kinapungua bila ya kuzingatia jinsia ya warithi.
Pili: Nafasi ya kizazi cha mrithi katika kufuatana kwa muda kwa vizazi, vizazi ambavyo vinaanza maisha na kujiandaa kubeba mzigo wa maisha kawaida fungu lake huwa kubwa katika urithi kuliko vizazi ambavyo vinayapa mgongo maisha, na mzigo wao unapungua bali huwa mzigo wake unawajibishwa kwa mwingine, na hilo bila ya kuangalia uuke au uume kwa warithi wakike na wakiume, binti wa marehemu hurithi hurithi kingi kuliko mama yake na wote ni wanawake, na binti anarithi kingi kuliko baba! Ambaye binti hurithi nusu peke yake! Vilevile mtoto wa kiume anarithi kuliko baba na wote ni wanaume. Na katika vipimo hivi vya falsafa ya Uislamu kuna hekima kubwa ya Kiungu, na makausudio makubwa ya Mola yamejificha kwa wengi, navyo ni vipimo havina uhusiano na uuke na uume hata kidogo.
Tatu: mzigo wa kifedha ambao Sharia ya Uislamu inawajibisha kwa mrithi kuubeba, na kuchukua jukumu lake kwa wengine. Na hiki ndicho kipimo pekee kinacholeta tofauti kati ya mwanamume na mwanamke - katika mantiki ya mwanamume ana majukumu mengi ya kifedha - lakini pamoja na hivyo hakupelekei dhuluma yoyote kwa kwa mwanamke au kupunguza nafasi yake, kinyume chake ni sahihi! Katika hali ya kuwa sawa daraja la udugu kwa warithi na wakawa sawa katika zama za kuzaliwa- mfano watoto wa marehemu ni wanaume na wanawake- tofauti ya mzigo wa maisha ndiyo sababu ya kutofautiana fungu la mirathi, na kwa hilo Qur`ani haijajumuisha katika utofauti kati ya mwanamke na mwanamume katika kuwajukumuisha warithi, bali imewathibiti katika hali moja pekee, Aya inasema: {Mwenyezi Mungu Anakuusieni juu ya watoto wenu: Fungu la mwanamume ni kama fungu la wanawake wawili} [AN NISAA: 11]
Na unapozama katika hali na masala ya mirathi kama ilivyokuja katika elimu ya mirathi unagundua uhakika unaowashangaza wengi katika fikra zao za awali na za makosa, katika maudhui hii ya kuchambua hali na mambo ya mirarhi unagundulika kwa uwazi:
1. Kwamba kuna hali nne tu mbazo mwanamke anarithi nusu ya mwanamume.
2. Kuna hali mara mbili ya hizi nne ambazo mwanamke anarithi sawa na mwanamume.
3. Kuna hali kumi au zaidi mwanamke anarithi zaidi ya mwanamume.
4. Na kuna hali mwanamke anarithi wala harithi mfano wake wanaume.
Kwa maana kuna zaidi ya hali thelathini ambazo mwanamke anachukua kama mwanamume au zaidi, au yeye anarithi wala harithi mfano wake mwanamume, ukilinganisha na hali nne ambazo mwanamke anarithi nusu ya mwanamume. Haya ndiyo matunda ya kusoma hali na mambo ya mirathi katika elimu ya mirathi, ambayo haikusimama katika vipimo vya uume na uke kama wadhaniavyo wengi.
Mirarhi kabla ya Uislamu
Mwanamke katika zama za ujinga alikuwa anamfuata mwanamme katika kila kitu, ameporwa haki ya kutaka, mpaka Umar bin Al-Khattab R.A. akasema: (Naapa kwa Mwenyezi Mungu hakika sisi katika zama za ujinga tulikuwa hatuhesabii chochote kwa mwanamke, mpaka Mwenyezi Mungu aliposhusha aliyoyashusha kuhusu wao, na akaapa aliyoyaapa kwao wao) ilifikia katika baadhi ya makabila kufanywa kama mali anarithiwa kama inavyorithiwa, na anahamia kwa mrithi kama inavyohama mali, na walikuwa wanamnyima haki nyingi na wanamwona kuwa hana haki, na katika vitu ambavyo ujinga ulimpora mwanamke ni urithi, kisha ukaja Uislamu ukakuta mwanamke anafanyiwa muamala huu wa kikatili, ukamwondoshea dhuluma hiyo, na ukamwekea fungu lake la mirathi, na ikashuka Qur`ani ikithibitisha haki yake katika mirathi, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Wanaume wana sehemu katika wanayo yaacha wazazi na jamaa walio karibia. Na wanawake wanayo sehemu katika waliyo yaacha wazazi na jamaa walio karibia. Ikiwa kidogo au kingi. Hizi ni sehemu zilizo faridhiwa} [AN NISAA: 7].
Mirathi kwa wasiokuwa Waislamu
Mwanamke katika dini nyingine hana mirathi, hana haki ya kurithi isipokuwa katika hali moja: Kutokuwa na ndugu wa kiume.
Imekuja katika Hesabu 27:8-11: {Kisha waambie Waisraeli kwamba mtu yeyote akifa bila kuacha mtoto wa kiume, urithi wake atapewa binti yake. Ikiwa hana binti, basi urithi huo watapewa ndugu zake wa kiume. Na ikiwa hana ndugu wa kiume, basi urithi wake utawaendea baba zake, wakubwa na wadogo. Na ikiwa baba yake hana ndugu wa kiume, basi urithi wake utakuwa wa jamaa yake wa karibu, naye ataumiliki kama mali yake. Hii itakuwa kanuni na sheria kwa Waisraeli, kama vile mimi Mwenyezi-Mungu nilivyokuamuru}
Imedhihiri kwamba kitabu kitakatifu kimeweka mirathi yote kwa mtoto wa kiume, ikiwa marehemu hana mtoto wakiume katika hali hii tu ndio anarithi mtoto wa kike.
 

Share this:

Related Fatwas