Kwanini Uislamu Umeweka Sharia ya Mume Kumwacha Mke wake?
Question
Matni ya shaka:
Imekuja Aya katika Qur`ani: {Hapana ubaya kwenu mkiwapa t'alaka wanawake} [AL BAQARAH: 236] na Qur`ani imehalalisha kwa mwanamume kwa utashi wake peke yake bila ya kurejea kwa yeyote katika anachokitaka, kuvunja familia yake na kubomoa nguzo zake na kuziparaganisha, anatoa talaka kwa mke wake.
Answer
Ni katika mambo ya kusikitisha kumwona mwanamume wa Kiislamu akigombana nje ya nyumba, anatoa talaka tatu kisha anamfukuza mke wake nyumbani kwake, si kwa sababu yoyote isipokuwa alitoa talaka katika ugomvi kwa sababu mwanamke hana uwezo wowote! Kisha anasema: “Hakika halali anayochukiza zaidi kwa Mwenyezi Mungu ni talaka” vipi Mwenyezi Mungu ahalalishe kitu anachokichukia? Je. Si sahihi kwamba anachokichukia akiharamishe?
Kuondoa shaka;
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Muulizaji amelazimisha picha ya wasiofuata mafundisho ya Dini ya Kiislamu, na akataka kuhukumu kwa picha hiyo kwa Sharia ya Kiislamu ya talaka kwa ujumla, hii ni aina ya kusingizia, na sahihi ni kuangalia sharia ya talaka katika njia yake ya mfumo wa Kiislamu.
Mwenyezi Mungu Ameweka sharia ya talaka katika Uislamu na akaiweka katika mikono ya mwanaume kwa sababu mbili:
Kwanza: Yeye ndiye anayegharamia, Mwenyezi Mungu amemlazimisha gharama za makazi kama alivyomlazimisha kuendelea kumgharamia, yeye ndiye muhitaji zaidi wa kusalia katika nyumba hii kuliko mwingine; na Uislamu kwa kujali sana kuendelea kubaki familia hii ukategemeza jambo hili kwake.
Pili: Kwamba mwanamume anadhibiti sana hisia zake kuliko mwanamke; wanawake wengi hawawezi kudhibiti hisia zao katika matukio mbalimbali, hasa matukio ya maisha ya ndoa; kwa sababu yanahitaji uzoefu mkubwa, yanahitaji aina ya fikra zinazoshinda akili sio hisia ambazo ndio sifa ya mwanamke, na mwanamke mara nyingi haelewi hilo, hivyo Mwenyezi Mungu Akaweka usimamizi katika mikono ya mwanamume.
Na si talaka zote zinavunja familia kama alivyosema muulizaji, bali talaka inaweza kuwa suluhishi pekee la kupumzika kwa pande zote mbili.
Na picha aliyoilazimisha muulizaji ya mwanamume anayegombana na mwingine kisha anatoa talaka na kumfukuza mkewe nyumbani kwake, picha hii ni ya watu wa kawaida wasiofuata dini katika Waislamu, na si sahihi kuhukumiwa kwa wasilamu wote, bali sahihi ni kwamba Waislamu wote wanajipanga katika suala la talaka wala hawafanyi haraka kama alivyosema muulizaji.
Fadhila za Talaka katika Uislamu
Mwenyezi Mungu Amehalalisha talaka ili kusuluhisha matatizo mengi ambayo yaneweza kuzuka kati ya mke na mume na yakawa hayana suluhisho isipokuwa kutengena, mwanamume anaweza kumwoa mwanamke kisha akabaini kuwa kuna tofauti kati yao katika tabia, na mwanamke anaweza akaonekana ni tasa hayafikiwi kwake makusudio ya juu ya ndoa, na yeye hapendi kuoa mke zaidi ya mmoja au hawezi, na sababu nyinginezo ambazo hazipelekei mapenzi kati ya mke na mume wala ushirikiano katika mambo ya maisha, na kusimama kwa haki za ndoa kama Alivyoamrisha Mwenyezi Mungu, kwa haya talaka inakuwa ni jambo la lazima ili kumaliza mahusiano ya ndoa ambayo haifikii makusudio yake, ambayo lau wanandoa wawili wangelazimishwa kuendelea nayo chuki zingekula nyoyo zao, na wangekaribia kila mmoja kummaliza mwenzake kwa njia awezayo, hiyo inaweza kuwa sababu ya kupetuka mipaka wote na ndio njia ya kila shari na madhambi, kwa hili Mwenyezi Mungu Ameweka sharia ya talaka kuwa njia ya kumaliza uharibifu huu na kuondoa shari hizi ili kila mmoja apate mbadala wa mwanandoa mwingine, huenda akapata alichokikosa kwa wa kwanza ikafikiwa kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na wakitengana Mwenyezi Mungu atamtosheleza kila mmoja katika wao kwa ukunjufu wake. Na Mwenyezi Mungu ni Mkunjufu Mwenye hikima} [AN NISAA: 130]
Na Uislamu ulipohalalisha talaka, umeshghulikia yote yanayotokea baada ya talaka, ukaweka malezi ya wototo wadogo kwa mama mpaka watakapokuwa wakubwa, na kuwajibisha baba kugharamia watoto wake na malipo ya malezi yake na kunyonya kwake hata kama mama ndio aneyefanya mambo hayo.
Na maana ya Hadithi ya “Hakika halali inayomchukiza zaidi Mwenyezi Mungu ni talaka” kwamba Mwenyezi Mungu Ameihalalisha na amewataka waja wake wasiharakishe hilo bali walifaje jambo la mwisho wasilifanye isipokuwa wanapalazimika.
Mwenyezi Mungu kuchukia talaka ni kuwakataza Waislamu kuharakisha hilo, na kwa hivyo ameichukia talaka katika nafsi, akasema Mtume S.A.W.: “Mwanamke yeyote anayemwomba mumewe talaka bila ya ubaya wowote basi na harufu ya Pepo ni haramu kwa mwanamke huyo” na akatahadharisha kulifanyia mzaha, akasema S.A.W.: “ Ni lipi jambo la mmoja wenu anayecheza na mipaka ya Mwenyezi Mungu, anasema, nimeacha, nimerejea”.
Na imezingatia talaka kuwa ni tiba ya mwisho ambapo haiwi sipokuwa mambo yanapokuwa yameshindikana, na tatizo kuongezaka na pale panapokuwa hapana tiba zaidi ya hiyo, na imeongoza kutumima njia nyingi kabla ya kufika kwenye talaka, imemtaka mume kuwa na subira na kuvumilia hata kama kuna vitu anavichukia kwa mke wake ili kuendelea kwa maisha ya ndoa, Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na kaeni nao kwa wema, na ikiwa mmewachukia, basi huenda mkakichukia kitu, na Mwenyezi Mungu ametia kheri nyingi ndani yake} [AN NISAA: 19], na ikamwongoza mume akigundua kuwa mke wake anatoka katika utiifu kumrekebisha kwa hatua: mawaidha kisha kumhama (kitandani) kisha kumpiga pigo lisilopetuka mpaka {Na ambao mnachelea kutoka katika ut'iifu wanasihini, muwahame katika malazi na wapigeni. Wakikut'iini msiwatafutie njia ya kuwaudhi bure. Hakika Mwenyezi Mungu ndiye aliye juu na Mkuu} [AN NISAA: 34], michakato na njia zote hii zinachukuliwa na kujaribiwa kabla ya kufikia kwenye talaka, na katika hili kunabainika kwamba mahusiano ya ndoa ni jamno kubwa kwa Mwenyezi Mungu.
Hakuwi sawa kutenganisha alichokiunganisha Mwenyezi Mungu na akakiwekea hukumu, muda wakuwa hakuna sababu za kweli na za hatari zinazowajibisha kutengana huko, wala halifikiwi hilo isipokuwa baada kutumia njia zote za kusuluhisha.
Na katika mwongozo wa Uislamu katika talaka, na kufuatilia sababu zinazopelekea talaka, kunabainika kwamba kama talaka inavyokuwa kwa masilahi ya mume, pia inakuwa kwa masilahi ya mke katika mambo mengi, inawezekana yeye ndio ametaka talaka, Uislamu haukatai maombi yake, na katika hili ni kunyanyua nafasi ya mwanamke na kumheshimu, si kumdaharau kama wanavyoadai watu, bali kumdharau ni kutosikiliza matakwa yake na kumlazimisha kujifunga na asichokipenda kinachomkera.
Talaka si kudharau utukufu wa ndoa kama wanavyodai, bali ninjia ya kupatikana ndoa sahihi na salama, ambayo inafikia maana ya ndoa na malengo yake makuu, si ndoa ya kujionesha iliokosa maana zote ndoa na makusudio yake.
Kwa sababu makusudio ya Uislamu si kuendelea kusalia mahusiano ya ndoa vyovyote yawavyo, lakini Uislamu umejalia malengo na makusudio katika mahusiano haya, hakuna budi kufikiwa, na kama hayakufikiwa basi pachukue nafasi yake yale yatakayofikia malengo hayo.