Jina la Kale la Mbao za Sharia Mbao Ngapi Zilizotumwa kwa Nabii wa Mwenyezi Mungu Musa A.S.?
Question
Matini ya shaka:
Imetajwa katika Qur'ani Tukufu: {Na tukamuandikia katika mbao kila kitu, mawaidha na maelezo ya mambo yote. (Tukamwambia): Basi yashike kwa nguvu na uwaamrishe watu wako wayashike kwa ubora wake. Nami nitakuonesheni makaazi ya wapotofu} [AL A'RAAF 145]
Answer
Na Qur'ani hapa imekanusha uhalisi, kwani kutokana na yanayojulikana ni kwamba sharia ya Musa imeandikwa katika mbao mbili na siyo mbao kadhaa, na katika mbao hizo mbili zimeandikiwa Nyasia kumi tu na siyo maelezo ya mambo yote, kama ilivyotajwa katika Qur'ani. Yatazame hayo katika Kitabu Kitakatifu [Kutoka 18-31]
Kujibu shaka:
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Aya Tukufu inayaelezea baadhi ya yaliyomkuta Mtume Musa A.S, kwani baada ya kukamilisha ahadi na Mwenyezi Mungu kumchagua aubebe Ujumbe na aweze kusema na Mwenyezi Mungu, alimwamrisha achukue vibao na kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa jambo hilo, na Mwenyezi Mungu kumwambia kuwa Vibao hivyo vimeandikwa ndani yake baadhi ya kila kitu kinachohitajiwa na Umma wake; mpaka yawe ni mawaidha tosha na uwazi wa kila kitu
Na Qur'ani haikutuainishia idadi ya vibao; na haikusema kwamba idadi yake ni vitatu au vinne au idadi nyingine. Lakini tunaposoma Kitabu Kitakatifu katika [Sehemu ya Kutoka] tunakuta kwamba zipo matini kadhaa zinazobainisha kwamba idadi ya vibao ni zaidi ya viwili. Basi amesema: "Kisha alimpa Musa alipokwisha matamko yake pamoja naye katika mlima wa Sainaa vibao viwili vya shahada, vibao vya jiwe vimeandikwa kwa vidole vya Mwenyezi Mungu" [Kutoka 18-31]
Kisa kimeeleza baada ya hayo kwamba Bwana wetu Musa A.S alivivunja vibao viwili hivyo kwa kusema: “Na alipokaribia mahali aliona ndama na mchezo, basi Musa alikasirika zaidi na akavitupa vibao viwili mikononi mwake na akavivunjika vyote viwili chini ya mlima” [Kutoka 19-32]
Kisha baada ya hayo Mwenyezi Mungu alimpatia vibao viwili vingine, na kwa hivyo anasema: Kisha Mungu akamwambia Musa tuchongee vibao viwili vya mawe kama vile vya mwanzo na uandike juu yake maneno ambayo yalikuwepo katika vibao vya mwanzo ulivyovivunja [Kutoka 34:1]
Basi kutokana na hayo inabainika kwamba idadi ya vibao ni zaidi ya vinne, na hiyo ni idadi inayoweza kuelezeka kwa wingi,
Na Maana ya kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na maelezo ya mambo yote} ni kwamba vimefafanua kila kitu kilichomo ndani ya vibao hivyo miongoni mwa hukumu mbalimbali wanazozihitaji katika dini yao, hiyo ni jumuishi inayokusudiwa umaalumu. [Kitabu cha: At Tashiil Li Ulum At Tanziil 45/2]
Na Kila kitu katika Aya hiyo - na yanayofanana nayo - Wanavyuoni wamezungumzia kwa kusema: "Katika kila maudhui ni kwa mujibu wa maudhui hiyo" na wakapigia mfano, nayo ni kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kuhusu upepo uliowaangamiza watu wa Aadi. {Unaangamiza kila kitu kwa amri ya Mola wake Mlezi. Wakawa hawaonekani ila nyumba zao tu. Hivyo ndivyo tuwalipavyo wakosefu!} [AL AHQAF 25] nao pamoja na hayo haukuangamiza mbingu na ardhi, bali umeangamiza kila kitu kinachoweza kuangamizwa, kama iivyodhihiri kutokana na muktadha wa Aya kama watu, mazao na mitende na mfano wake.