Ukinzani wa Qur'ani na Kitabu Kitak...

Egypt's Dar Al-Ifta

Ukinzani wa Qur'ani na Kitabu Kitakatifu katika Kisa cha Kujenga kwa Namruudh Ukuta Mrefu wa Babiloni.

Question

Matini ya shaka:
Imetaja katika Qur'ni Tukufu kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Walipanga vitimbi walio kuwa kabla yao, Mwenyezi Mungu akayasukua majengo yao kwenye misingi, dari zikawaporomokea juu yao, na adhabu ikawajia kutoka wasipo kujua}. [AN NAHL 26]
 

Answer

Na imepokelewa katika Tafsiri kwamba maana inayokusudiwa katika Aya hiyo ni Namruudh Bin Kanaan, hakika yeye alijenga ukuta mrefu huko Babiloni ambao upana wake ni sawa na dhiraa elfu tano ili aweze kuangalia jambo la mbinguni basi Mwenyezi Mungu Mtukufu akampelekea upepo na ukuta wake ukamporomokea yeye na watu wake na wote wakaangamia. Na hayo yanatofautiana na yaliyotajwa katika Vitabu Takatifu, basi imetajwa katika vitabu hivyo kuwa Namruudh ni Bin Kosh Bin Haam Bin Nuh A.S., na siye Bin Kan'aan [Uumbaji 10- 6-8]
Baada ya gharika hiyo watu walianza kujenga mji na majumba marefu yatakayodumisha na kuendeleza majina yao, na Mwenyezi Mungu Mtukufu akawaadhibu huku midomo yao ikibwabwaja wasijue nini wanachokisema na kushindwa kufahamiana na wakasitisha ujenzi na kwa ajili hiyo mji huo ukaitwa Babiloni: kwa sababu Mwenyezi Mungu Mtukufu aliibabaisha midomo yao [Uumbaji: 11:1 -9]
Kujibu shaka:
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Katika kuanza, hapana budi itambulike ya kwamba Wanachuoni wa Tafsiri ya Qur'ani Tukufu wanakusudia katika Vitabu vyao Ujumuishaji mtupu wa kila kinachowezekana kunufaisha katika Tafsiri ya Aya Tukufu, bila ya wao kuchunguza na kukagua, na kwa kuhamisha tu hakumaanishi kutegemea kwao kila walichokitaja, na pamoja na hayo hakika sisi tunawaona wanatanguliza kilicho bora zaidi kwao kukubalika na wanachelewesha wanayoyaona kuwa ni dhaifu. na kusudio lao katika jambo hilo ni kukusanya maelezo yote waliyonayo, kwa wale wa baada yao kuhusu Aya, na kwa hivyo, Mjadala wa kukubali au kuyarudi yaliyotajwa na Wanachuoni Wakubwa wa Qur'ani bila ya Maandiko ya Qur'ani.
Ama kwa upande wa ile Aya yenye maana inayowachanganya hiyo inawazungumzia makafiri wa Makkah na inawabainishia kwamba iliwatokea waliokuwa kabla yao katika Mataifa vitimbi kama hivyo wavifanyavyo, na adhabu waliadhibiwa hapa hapa duniani kabla ya Akhera na nyumba zao zikaharibiwa na kuwaporomokea na ikawajia adhabu kwa namna wasiyoitambua.
Na katika hiyo ni kauli mbili:
Ya Kwanza: Kwamba lengo la hayo ni uwasilishaji wa hali za namna ya kuondoshwa kwa Mataifa, na ndani yake kuna uazimaji wa maana wakilishi, nayo ni ufananishaji wa hali iliyowatokea wale waliofanya vitimbi katika kuzuia basi Mwenyezi Mungu akawachukua haraka na kuwaondoshea hicho cheo, kwa hali ya watu waliojenga jumba kubwa lenye nguzo nyingi na wakalikimbilia kwa ajili ya kujihifadhi kisha mwenyezi Mungu Mtukufu akazing’oa nguzo zake na dari lake likawaporomokea kwa mpigo na wote wakaangamia.
Na juu ya hivyo, kwa hiyo maana ya waliokuwa kabla yao inakuwa ni yenye kukusanya wafanya vitimbi wote waliobomolewa na kuporomokewa na majumba. Na hii ndio kauli iliyopitishwa na wengi miongoni mwa Wanachuoni wa Tafsiri ya Qur`ani Tukufu. [Tafsiri ya Al Qortbiy 98/10, na Tafsiri ya Al Alusiy 361/4, kitabu cha: At Tahariir wa At Tanwiir 133/14]
Ya Pili: Baadhi ya wafasiri walisema: labda inatakiwa kwa Aya Tukufu kuainisha, yaani hakika, basi inayotakiwa ni jamaa maalumu, halafu baadhi ya wafasiri walitofautiana katika jamaa hiyo, hawa ni nani? Basi walitaja kauli kadhaa kama mfano:
Ya Kwanza: Kwamba wanaotakiwa nao ni Namruudh na jamaa yake.
Ya Pili: Bikhtanser na jamaa yake.
Ya Tatu: Waliogawa amabo Mwenyezi Mungu Mtukufu aliwatajia katika Suratu Al Hijr {Kama hivyo tuliwateremshia walio gawa. Ambao wakaifanya Qur'ani vipande vipande} [AL HIJR 90-91]
Ya Nne: wakusudiao ni jamaa ya Bwana Luutw A.S.
Na miongoni mwa wanachuoni wa Tafsiri, yule ambaye hajaziangalia kauli zote lakini yeye anautaja uwezekano uliopo katika Aya Tukufu kwa maana mbili zilizotangulia – kwa maana ya uwakilishi au uainishaji.
Na Aya imebeba kisa cha Namruudh kwa umaalumu wake kutoka kwa Wanachuoni wa Tafsiri ya Qur`ani Tukufu wapo wasio ridhia wanadhoofisha kisa hiki na hasa kwa kuwa kimepokelewa ndani yake kauli ambazo akili haiwezi kuzikubali na kuziamini, kama vile kauli yao: hakika jengo alilolijenga Namruudh upana wa ukuta wake ulikuwa dhirai elfu tano, na inasemekana ni farsakh ambayo ni sawa na kilomita nne hadi sita, na alitaka kwa kufanya hivyo awe na uwezo wa kupanda mbinguni ili aweze kupambana na watu wa huko, kwa hiyo maana ya ujanja katika Aya ni ujenzi wa Ukuta kwa ajili ya kupambana na wakazi wa huko.
Kwa upande wa kauli yao: kwamba sababu ya kuuita mji huo kwa jina hilo ni kwamba watu baada ya gharika walijenga mji wao na majumba marefu marefu ili wadumishe milele jina lao, basi Mwenyezi Mungu akawaadhibu kwa kuwasababishia uzito katika ndimi zao na wakashindwa kuelewana, na wakaacha kujenga na kwa sababu hiyo mji huo uliitwa Babiloni jambo ambalo haliachwi kama lilivyo; kwa sababu wanachuoni wametaja kuwa mji wa Babiloni ulijengwa na kiongozi mwenye nguvu nyingi Purasab, na jina la mji huo linatokana na sayari ya Mushrarii; kwani neno Babiloni kwa lugha ya eneo hilo ni jina la Mushtari. [Mu'jam Al Buldaan 310/1]

 

Share this:

Related Fatwas