Miujiza ya Nabii wa Mwenyezi Mungu ...

Egypt's Dar Al-Ifta

Miujiza ya Nabii wa Mwenyezi Mungu Musa A.S.

Question

Matini ya Shaka:
Imetajwa katika Qur'ani Tukufu Kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Basi tukawapelekea tufani, na nzige, na chawa, na vyura, na damu, kuwa ni Ishara mbali mbali. Nao wakapanda kiburi, na wakawa watu wakosefu}. [AL AARAF 133] Pia imetaja Kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na kwa yakini tulimpa Musa ishara tisa zilizo wazi. Waulize Wana wa Israili alipo wafikia, na Firauni akawaambia: Hakika mimi nakuona wewe Musa umerogwa!} [AL ISRAA 101].
 

Answer

Na ni inaeleweka kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu aliwapigia wamisri juu ya mkono wa Musa mapigo kumi, na siyo matano kama ilivyotajwa katika Aya ya kwanza, na wala sio tisa kama ilivyotajwa katika Aya ya pili. Na kadhalika kwamba Tufani haikutokea Misri katika zama za Firauni, bali ilikuwa tukio mashuhuri lililowakumba jamaa wa Nuhu.
Kujibu shaka:
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Hakuna katika Aya mbili yaliyoainisha idadi ya Miujiza:
Hakuna katika Aya mbili zilizotajwa, ukinzani wowote wa kuiweka miujiza yote katika idadi maalumu, kwani Aya moja ya kwanza haina ndani yake utajo wa idadi kabisa, ukiachana na kwamba kuwa ndani yake na mzingo wa idadi maalumu, na vilevile Aya ya pili – ingawa imekuwa na utajo ndani yake wa idadi – isipokuwa Aya hiyo haikuzinga miujiza ya Musa kwa idadi hii; kwani imeamuliwa kwamba utengaji wa idadi kwa kutaja haimaanishi kukana kilichoongezeka juu yake
Miujiza ya Musa ni mingi:
Aya ambazo Mwenyezi Mungu Mtukufu akampa Musa A.S., ni nyingi. Na Imamu Ar Razi ametoa kutoka katika Aya za Qur'ani Aya kumi na sita; moja yake ni: kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu aliondosha ugumu na uzito katika ulimi wake, na muujiza wa pili: ni fimbo yake kugeuka nyoka, na wa tatu: joka lake kuyameza majoka yao yote na kwa wingi wake, na muujiza wa nne: Mkono mweupe, na wa tano: ni gharika, nzige, chawa vyura, damu na wa kumi: kuipasua bahari kama katika kauli ya Mwenyezi Mungu Mtuykufu{Na tulipo ipasua bahari kwa ajili yenu natukakuokoeni, tukawazamisha watu wa Firauni, na huku mnatazama}. [AL BAQARAH 50]
Na ya kumi na moja: Jiwe kama katika kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na Musa alipo omba maji kwa ajili ya watu wake, tulimwambia: Lipige jiwe kwa fimbo yako. Mara zikatimbuka chemchem kumi na mbili; kila kabila ikajua mahali pake pa kunywea. Tukawaambia: Kuleni na mnyweriziki ya Mwenyezi Mungu, wala msiasi katika nchi mkafanya uharibifu}. [AL BAQARAH 60],
Na ya kumi na mbili: kulinyanyua jabali; kama katika kuali ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na pale tulipo unyanyua mlima juu yao ukawa kama kwamba ni kiwingu kilicho wafunika, na wakadhani kuwa utawaangukia, (tukawaambia): Kamateni kwa nguvu tuliyo kupeni, na yakumbukeni yaliyomo ndani yake ilimpate kumcha Mungu}. [AL AARAF 171],
Na ya kumi na tatu ni kuteremsha chakula cha Manna na Salwa, na ya kumi na nne, naya kumi na tano ni: kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na hakika tuliwaadhibu watu wa Firauni kwa miaka (ya ukame) na kwa upungufu wa mazao, ili wapate kukumbuka}. [AL AARAF 130]. Na ya kumi na sita: kutoziona mali zao kama mitende, unga, vyakula, na fedha zao. [At Tafsiir Al Kabiir 64/21].
Swali: Kwanini Mwenyezi Mungu Mtukufu amezingatia kutaja miujiza hiyo tisa?
Na swali linabakia kuwa: kwanini kuna kuzitenga Aya hizi tisa kwa kutaja katika aya mbili za Qur'ani Tukufu? tunasema hii ina maana ya kwamba miongoni mwa miujiza yote imo miujiza tisa ya Musa A.S, ina sifa maalumu kinyume na mingine na kuna zaidi ya mmoja wa Mwanachuoni wa Tafsiri waliojitahidi kuainisha, na inaonekana wazi ya kwamba miujiza tisa ni: mkono kugeuka rangi na kuwa mweupe kila alipouingiza mfukoni mwake, fimbo yake kugeuka nyoka, gharika, nzige, vyura, damu,, chawa, ukame,, ugonjwa ngozi, nazo nayo imetajwa katika Suratul Aaraaf. [Tafsiri ya At Tahriir Wa At Tanwiir 225/15].
Na hizo tisa chini yake kuna ziada, na wala zenyewe haziingii katika zingine na wala haziingiliani kama ambavyo Aya hizi tisa zina sifa maalumu zinazozitofautisha na zingine ambazo Musa A.S, alipewa na Mola wake nazo ni Aya miongoni mwa Aya ambazo alizipewa ili aweze kuzitumia katika kupambana na Firauni, na hivyo kuwa sio aya ambazo Mwenyezi Mungu aliwateremshia Watoto wa Israeli.
Na inarudiarudia kutaja Aya tisa katika mahali pawili katika Qur'ani Tukufu: Aya ya Suratu Al Israa: {Na kwa yakini tulimpa Musa ishara tisa zilizowazi. Waulize Wana wa Israili alipo wafikia, na Firauni akawaambia: Hakika mimi nakuona wewe Musa umerogwa!} [AL ISRAA 101]. Na Aya ya Suratu An Naml: {Na ingiza mkono wako katika mfuko wako, utatoka mweupe bila ya maradhi. Ni katika Ishara tisa za kumpelekea Firauni na watu wake. Hakika hao walikuwa watu waovu} [AN NAML 12].
Na Aya zote mbili zina mapokezi ya suala la Firauni na watu wake. Amesema Ibnu Kathiir: Musa A.S, alipewa Aya nyingine nyingi, zikiwemo; kupiga jiwe kwa fimbo yake na kutoka kwa maji katika jiwe hilo, na pia Aya ya kuwafunika kwa kiwingu, Aya ya kuteremshwa kwa Chakula cha Manna na Salwaa, na aya nyingine nyingi walizoteremshiwa Banu Israeli baada ya kuondoka kwao Misri, na hapa zimetajwa Aya tisa tu ambazo alizishuhudia Firauni na Watu wake wa Misri zikawa hoja juu yao wote na wakazipinga na wakazibisha kwa ukafiri na upingaji. [Tafsiir Ibn Kathiir 66/3 na yanayoifuata]
Tufani (Gharika):
Ama kwa upande Gharika lililotajwa ndani ya Aya ya kwanza hilo silo lile lililotajwa na ambalo lilitokea wakati wa zama za Nuhu A.S, na jambo la kushangaza ni kwamba kuna kutajwa kwa Tufani katika kitabu cha Bibilia tufani iliyotokea Misri katika zama za Firauni, na Firauni kutaka msaada kwa Musa A.S, ili amwokoe katika Tufani hiyo! Basi muulizaji vipi anaghafilikia jambo kama hilo?
Hakika Firauni aliambiwa: Wewe ni mbishi kwa watu wangu hata usiwaache waende zao, kwa hiyo wakati kama huu nitaleta mvua kubwa ya mawe ambayo haijawahi kutokea nchini Misri, tangu mwanzo wake hadi leo, na ikateremka mvua kali na baridi, na Firauni akamuahidi Musa A.S, kwamba atawaachia kizazi cha Israeli, lakini Firauni alipoona kuwa mvua na baridi na radi vimekatika akarejea tena kukosea na akaupotosha moyo wake na ahadi yake [kutoka 9:17-35].

 

Share this:

Related Fatwas