Ukoo wa Bikira Maria

Egypt's Dar Al-Ifta

Ukoo wa Bikira Maria

Question

Matini ya Tuhuma
Imetajwa katika Qur’ani tukufu kauli yake Mwenyezi Mungu: {Akenda naye (mwanawe) kwa jamaa zake amembeba. Wakasema: Ewe Maryamu! Hakika umeleta kitu cha ajabu!(27) Ewe dada yake Harun! Baba yako hakuwa mtu muovu, wala mama yako hakuwa kahaba (28)} [MARYAM: 27:28] Vile vile kauli yake Mwenyezi Mungu: {Na Mariamu binti wa Imrani, aliye linda ubikira wake, na tukampulizia humo kutoka roho yetu, na akayasadiki maneno ya Mola wake Mlezi na Vitabu vyake, na alikuwa miongoni mwa wat'iifu} [AT TAHRIM: 12]
 

Answer

Tunauliza: Biblia inasema kwamba Bikira Mariam ni binti Haley [Luka 3:23]? Basi vipi Qur’ani inasema kuwa yeye ni binti yake Imran, Abu Musa Mtume, na kwamba yeye ni dada yake Harun, ingawa yuke na baina ya Imran, Harun na Musa miaka elfu moja na mia sita?
Jibu la Tuhuma:
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Kwanza: Kilichotajwa katika Sura hii iliyotangulia ni nasaba ya Yusuf An-Najjar Ibn Hali, sio nasaba ya Maryam binti Imran, na hili linatudhihirishia kwa uwazi mkanganyiko mwingi unaotokea kwa sababu ya ukosefu wa yakini katika upitishaji wa maarifa Luka anasema: (Na Yesu alipoanza, alikuwa na umri wa kama miaka thelathini, naye alikuwa anafikiriwa ni mwana wa Yusufu Ibn Hali) (Luka 3:23).
Kwa hiyo, hakuna ubaya kuwa Maryamu ni binti yake Imran, kama ilivyotajwa katika Qur’ani, na hakuna upingaji kuhusu hilo baina ya Qur’ani na ukweli, wala baina ya Qur’ani na Kitabu kitukufu.
Pili: Kuhusu Maryam ni dada yake Haruna, maana yake ni kuwa amenasibishwa kwa Mtume Harun, ikiwa kwa wema wake au kwa kuwa yeye ni katika kizazi chake, au ana kaka aitwaye Haruna asiyekuwa Mtume huyo. Na hii ni miongoni mwa njia zinazokubalika katika lugha, imepokelewa kutoka kwa Al-Mughirah Ibn Shu’bah, amesema: “Nilipofika Najran waliniuliza, wakasema: Mnasoma: Ewe dada yake Harun, na Musa alikuwa kabla ya Isa hivi na hivi. Nilipomjia Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W.) nilimuuliza kuhusu hilo akasema: "Walikuwa wakiitwa kwa majina ya Mitume wao na watu wema kabla yao.”
Pia inajulikana katika sura za Biblia kwamba Mariam, (A.S.), alitoka katika kabila la Haruni, kwa hiyo inawezekanaje kwamba alikuwa dada ya Haruni? Yaani: wa kizazi chake. Ilikuja mwanzoni mwa Injili ya Luka kwamba Elizabeti, mke wa Zakaria (A.S.), alikuwa wa kizazi cha Haruni kutoka kabila la Lawi, na Zakaria alikuwa wa kizazi cha Haruni wa kabila ya Lawi, akamwoa; Kwa sababu sheria yao inataka kila mmoja wa kabila lake aoe tu, na kwamba Mariam alikuwa jamaa ya Elizabeti (). Na ikithibitika kuwa yeye ni jamaa yake, basi imethibiti kuwa Mariam ni kabila la Lawi.

 

Share this:

Related Fatwas