Kuongea Kwa Nabii Isa Akiwa Mchanga...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kuongea Kwa Nabii Isa Akiwa Mchanga.

Question

Matini yenye Shaka:
Imekuja ndani ya Qur`ani Tukufu kauli ya Mwenyezi Mungu:
{Naye atazungumza na watu katika utoto wake na katika utu uzima wake, na atakuwa katika watu wema} [AAL- IMRAA: 46].
Na kauli yake Mola Mtukufu:
{Na pale Mwenyezi Mungu atapo sema: Ewe Isa bin Maryamu! Kumbuka neema yangu juu yako, na juu ya mama yako, nilipo kutia nguvu kwa Roho Takatifu, ukazungumza na watu katika utoto na utu uzimani} Al-Maidah: 110.
Na kauli yake Mola Mtukfu:
 

Answer

{Akawaashiria kwa mtoto mdogo. Wakasema: Vipi tuzungumze na mtoto mdogo aliye ndani ya mbeleko? * Mtoto akasema: Hakika mimi ni mja wa Mwenyezi Mungu. Amenipa Kitabu, na amenifanya Nabii} MARYAMU: 29: 30]. Kitabu Kitakatifu hakijazungumza kuwa Masiha alizungumza akiwa mdogo.
Jibu la Shaka:
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Kwanza: Injili haikueleza kwa kina miujiza ya Nabii Isa. Amani ya Mungu iwe juu yake.
Pili: Maelezo ya Qur`ani Tukufu kuhusu kuzungumza kwa Masihi akiwa bado mtoto mchanga peke yake yanatosha kuamini jambo hili kwani tumekuwa na dalili nyingi juu ya ukweli wa Kitabu hiki katika yale yanayotolewa muongozo, mfano wa jambo kama hili la Masihi au Nabii Isa kuzungumza katika umri huu halina masilahi yeyote kwa Waislamu kulielezea au kulificha.
Tatu: Mtume S.A.W amelitaja hilo na Qur`ani ikalisema hilo wakati wa zama za Mtume mbele ya Wakristo ndani ya Kisiwa cha Kiarabu na nje yake na wala hatuna taarifa yeyote ya kupingwa maelezo hayo na mtu yeyote, na ifahamike kuwa umuhimu wa kwanza ulikuwa ni kubatilisha ulinganiaji wa Mtume S.A.W na walimfanyia mijadala katika maudhui nyingi mfano wa: Je Maryamu Binti Imran ni dada wa Haruna? Mtume akawabainishia kuwa walikuwa wanamnasibisha kwa waja wema ndani ya watu wao na wala si ndugu yake kwa kuzaliwa, kwa maana si ndugu wa mama mmoja na baba mmoja, ikiwa wamefanya naye mjadala katika jambo kama hili hivi washindwe kujadiliana naye katika jambo muhimu zaidi ya hilo?
Nne: Lau Nabii Isa - Amani ya Mungu iwe kwake – asingezungumza alipokuwa mtoto mchanga na kumtetea mama yake basi Wayahudi wangemuhukumu mama yake kwa kuchomwa moto kwa mujibu wa sheria zao: “Na binti ya kuhani yeyote atakapojitia unajisi kwa ukahaba, amemtia unajisi baba yake; atachomwa moto” Mambo ya Walawi 21:9. Pamoja na kuwa Wayahudi hawakumchoma moto wala hawakumgusa kwa kumfanyia kero yeyote hivyo ni lazima atakuwa amekuja na kitu kilichowaondoa kwenye kutekeleza adhabu hiyo, swali ni kuwa: Ni kwanini Wayahudi walimwacha bila ya kumchoma moto? Pamoja na kuwa ni mjakazi ndani ya Hekalu?

 

Share this:

Related Fatwas