Tanwiin Haibadiliki Kisarufi

Egypt's Dar Al-Ifta

Tanwiin Haibadiliki Kisarufi

Question

Aya ya Qur`ani: Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema: {Na watapitishiwa vyombo vya fedha na vikombe vya vigae} [AL INSAAN: 15] Na akasema tena Mwenyezi Mungu: {Hakika Sisi tumewaandalia makafiri minyororo na pingu na Moto mkali} [AL INSAAN: 4] 

Answer

Nini amesema mjenga hoja?
Baada ya kutajwa Aya ya kwanza kwa kutumia alama ya Tanwiin pamoja na kwamba haipaswi kuleta alama ya Tanwiin kwa vile kawaida huwa inazuilika na kubadilika kisarufi, na akasema tena baada ya kutajwa Aya ya pili hivyo ni kwanini amesema minyororo kwa kutumia alama ya Tanwiin pamoja na kuwa haikupaswa alama ya Tanwiin kwa kuzuilika kwake na kubadilika kisarufi? ( ).
Kuondoa Shaka:
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
1. Maneno haya si maneno yanayokubali kubadilika kisarufi kama alivyosema muulizaji kwa upande wa mfumo wa usomaji wa Hafswi An Aswim, bali yenyewe hayakubali kubadilika kisafuri kwa maana ya kukubali alama ya Tanwiin ( ) ambayo ndio iliyosababisha mchanganyiko wa mambo kwa uwepo wa herufi ya alifu, lakini husomwa bila ya alama ya Tanwiin kwa sababu ya kuzuilika na mabadiliko ya kisarufi, na sababu ya kuzuilika kwake ni muundo wenye kumalizikia na uwingi.
2. Muulizaji ameshindwa kuelewa kuwa katika lugha za Waarabu hawasemi kwa kuzuiliwa kubadilika kisarufi, na kutokana na hilo maneno haya yamekuja katika baadhi ya visomo kisarufi, kwa mfano Nafii amesoma na Ibn Katheer pamoja na Al-Kasaany na Jaafari “Qawaariiran” kwa alama ya Tanwiin ya kisarufi ikiwa herufi ya nuni katika sehemu mbili kwa pamoja “Qawaariiran” na “Salaasilan” upande wa sarufi kwenye maneno mawili ni kuwa baadhi ya Waarabu walikuwa wanatumia alama ya Tanwiin maneno yote, na wala hakuna katika lahaja yao maneno yenye Tanwiin na yasiyokuwa na Tanwiin bali yote ni yenye Tanwiin, na Qur`ani imeteremka kwa lugha ya Kikuraishi kisha kwa lahaja za makabila mengine ya Kiarabu ( ).

 

Share this:

Related Fatwas