Je Radi ni Malaika?

Egypt's Dar Al-Ifta

Je Radi ni Malaika?

Question

Matni Yenye Shaka:
Imepokelewa ndani ya Qur`ani kauli ya Mungu:
{Na radi inamtakasa Mwenyezi Mungu kwa kumhimidi, na Malaika pia, kwa kumhofu. Naye hupeleka mapigo ya radi yakampata amtakaye. Nao wanabishana juu ya Mwenyezi Mungu. Na Yeye ni Mwenye adhabu kali!} Ar-Raad: 13.
 

Answer

Imepokelewa katika baadhi ya Hadithi zinazonasibishwa na Nabii wa Uislamu S.A.W kuwa radi ni Malaika aliyopewa jukumu la mbingu.
Tunauliza: Ikiwa radi ni umeme unaotokana na mgongano wa mawingu, hivyo ni kwa nini anasema kuwa: Radi ni moja ya Malaika.
Kuondoa Shaka:
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Kwanza: Aya haijataja zaidi ya kusema kuwa radi inamtukuza Mwenyezi Mungu Mtukufu na viumbe kumtukuza Mwenyezi Mungu Mtukufu ni jambo linalokubalika na dini wala halipingwi na wenye akili, kisha hakuna shaka yeyote kwenye Aya bali wewe utakuta ndani ya Kitabu Kitakatifu yanayounga mkono viumbe kumtukuza Mwenyezi Mungu Mtukufu, ndani ya Kitabu cha Zaburi: 69, 34 “Mbingu na nchi zimsifu, bahari na vyote viendavyo ndani yake”. Na katika Kitabu cha Zaburi: 148 “Haleluya. Msifuni Bwana kutoka mbinguni; Msifuni kaitka mahali palipo juu * Msifuni, enyi malaika wake wote; Msifuni majeshi yake yote * Msifuni, jua na mwezi; Msifuni nyote zote zenye mwanga * Msifuni enyi mbingu za mbingu, Nanyi maji mlioko juu ya mbingu * Na vilififu jina la Bwana kwa manaa aliamuru vikaumbwa * Na vilisifu jina la Bwana kwa maana aliamuru vikaumbwa * Amefithibitisha hata milele na milele, ametoa amri wala haitapita * Msifuni Bwana kutoka nchi, enyi nyangumi na vilindi vyote * Moto na mvua ya mawe * Theluji na mvuke, Upepo wa dhoruba ulitendao neno lake * Mlima na vilima vyote. Miti yenye matunda na mierezi yote * Hayawani na wanyama wafungwao, vitambaavyo na ndege weye mbawa * Wafalme wa dunia na watu wote, wakuu na makadhi wote wa dunia * Vijana waume na wanawali wazee na watoto * Na walisifu jina la Bwana, maaa jina lake peke yake limetukuka; Adhama yake I juu ya nchi na mbingu”.
Pili: Ama maana iliyokuja ndani ya baadhi ya Hadithi ya kuunganishwa kwa radi na Malaika maana yake ni kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu ameunganisha tukio hili ambao watu wanaliona na sababau nyingine huwenda zikawa hazionekani kwa hisia zao nayo ni uwepo wa Malaika aliyepewa usimamizi wa tukio hili, na mwenye kuamini kuwa ndani ya ulimwengu kuna mambo mengi yasioonekana ambayo hayawezi fahamika na hisia hayawezi kuwekwa mbali na kukubali hilo.

 

Share this:

Related Fatwas