Je Qur'ani Inaamirisha Kutoa Msamah...

Egypt's Dar Al-Ifta

Je Qur'ani Inaamirisha Kutoa Msamaha?

Question

Matni Yenye Shaka:
Imeelezwa kuwa Qur`ani inapinga kutokana na amri yake ya kutoa msamaha ambapo imesema: {Na hakika Kiyama kitafika. Basi samehe msamaha mzuri} [AL HIJIRI: 85]
Na imekataza kutoa msamaha ambapo Mungu Anasema:
{Ewe Nabii! Pambana na makafiri na wanafiki, na wakazanie. Na makazi yao ni Jahannamu, na huo ndio mwisho mbaya} [AT TAWBAH: 73].
 

Answer

Jibu la Shaka:
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Hakuna mgongano kati ya Aya mbili, vilevile tofauti ya muda Aya ya kwanza ilikuwa mwanzoni mwa kuanza kwa Uislamu ambapo Waislamu hawakuwa na dola bali ni watu wachache wasio na uwezo wa kupambana na batili kwa nguvu.
Ama Aya ya pili yenyewe inaelezea wakati Waislamu walipokuwa na nguvu na baada ya kutengeneza dola yenye nguvu na ukawa umefika wakati wa kufikisha dini kwa uwazi na kuipambania.
Inawezekana kufahamika mfumo wa Uislamu katika kupambana na batili katika wigo wa Aya hizi mbili kuwa Muislamu katika hali ya udhaifu anafanyia kazi msingi wa kusamehe, ama katika hali ya kuwa na nguvu Muislamu anapaswa kulingania kwa uwazi na kupambania kazi hiyo hata kama atalazimika kutumia nguvu ikiwa atakutana na nguvu inayomzuia kueneza hukumu za dini yake na mafundisho ya Uislamu wake. Twahir Ibn Ashuur amesema: Kuamrisha kwake kusamehe ni katika maadili mema, na hilo linarejea kwenye ubaya wa ushirikiano wao na Mtume S.A.W na wala si sehemu ya kutaja uadui wa kikabila au kidini, wala hakuna kupingana na kauli yake katika Suratu Baraatu:
{Piganeni na wasio muamini Mwenyezi Mungu wala Siku ya Mwisho, wala hawaharamishi alivyo haramisha Mwenyezi Mungu na Mtume, wala hawashiki Dini ya Haki, miongoni mwa walio pewa Kitabu, mpaka watoe kodi kwa hiari yao, hali wametii} [AT TAWBAH: 29], kwa sababu hizo ndio hukumu kuu hivyo hakuna haja ya kusema kuwa Aya hii imefutwa na Aya iliyopo kwenye Suratu Baraatu ( ).

 

Share this:

Related Fatwas