Je Qur'ani Inalingania Kulipiza Kis...

Egypt's Dar Al-Ifta

Je Qur'ani Inalingania Kulipiza Kisasi?

Question

Matni Yenye Shaka:
Imekuja ndani ya Qur`ani kauli ya Mwenyezi Mungu:
{Anaye kushambulieni nanyi mshambulieni, kwa kadiri alivyo kushambulieni. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Na jueni kwamba Mwenyezi Mungu yu pamoja na wacha-Mungu} Al-Baqarah: 194.
 

Answer

Na sisi tunaona athari mbaya ya msingi wa kulipiza kisasi zikienea kwa sababu ya maneno haya, na askari polisi wangapi wakipata tabu kutokana na matokeo yake, na zikapaza sauti za wasomi katika kufundisha dhidi ya nadharia hii, je kulipiza uadui kwa aliyekufanyia uadui ndio tiba ya uhalifu?
Jibu la Shaka:
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Kwanza: Kusudio la kulipiza uadui kwenye Aya:
Aya imefuata mwenendo wa lugha ya Kiarabu katika kutumia mfumo wa kibalagha unaoitwa kwa jina la kuunda, nao ni kutaja kitu kwa tamko la mwingine ili kuingia kwenye urafiki japo ikiwa si sehemu ya maana yake kwa lengo la kibaragha.
Au mfano wa kauli ya mshairi inayosema: Nipikie juba na kanzu ( ), juba na kanzu huwa havipikwi, kana kwamba amesema: Nishoneeni, mfano wake kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:
{Na malipo ya uovu ni uovu mfano wa huo. Lakini mwenye kusamehe, na akasuluhisha, basi huyo malipo yake yapo kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye hawapendi wenye kudhulumu} As-Shaura: 40.
Kwa maelezo hayo ni kuwa, maana ya Aya ni kuwa mwenye kuwafanyia ubaya basi rudisheni ubaya wake na uovu wake, na zilindeni nafsi zenu, na wala hakuna kwenye Aya msukumo kwa Muislamu kufanya uadui, ni vipi na Aya ambayo kabla yake inamlingania Muislamu kudhibiti mizani ya mapigano na kuleta uadilifu, kwa vita kuwa na sababu za misingi ya kuondoa fitina wala si katika matamanio ya kulipiza kisasi na kuleta uadui, na kuhusisha kwa madhalimu kuwatisha kutokana na vitendo vya uadui, kwani Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema:
{Na piganeni nao mpaka pasiwepo fitina, na Dini iwe ya Mwenyezi Mungu tu. Na kama wakiacha basi usiweko uadui ila kwa wenye kudhulumu} [AL BAQARAH: 193].
Pili: Aya imekataza kulipiza kisasi ambapo imeamrisha adhabu sawa na ubaya wenyewe:
Kisha Aya inamkemea mtu anayelipiza kisasi ambapo kulipiza kisasi hakuna adhabu sawa na uadui, ulipizaji kisasi ni desturi za zama za ujinga zinazopelekea mtu katika watu aliyeuliwa kuuwa mtu mmoja katika watu wanaodhaniwa kuwa muuaji ni miongoni mwao pasi ya kuangalia kuwa huyo mtu ni muuaji kweli au hapana, na pasi ya kufanyika uchunguzi wowote katika hilo, hivyo Aya ikaamrisha mtu kuhakikisha kuwa adhabu iwe sawa na kosa au uharifu bila ya kuzidisha, na kusudio la mfano wake ndani ya Aya Tukufu ni mfano wake katika kiwango na hali ( ).
Usamehevu pia una nafasi:
Muulizaji hakufahamu kuwa amri ya kurejesha uadui iliyokuja katika Aya Tukufu haikusudii ulazima, bali ni jambo halali, hivyo mwenye kutaka kusamehe haki yake Sharia Takatifu inamruhusu kufanya hivyo, na katika msamaha huu ana malipo makubwa. Mwenyezi Mungu amesema kumwambia Mtume wake S.A.W wakati alipouliwa baba yake mdogo mzee Hamza:
{Na mkilipiza basi lipizeni sawa na vile mlivyoadhibiwa. Na ikiwa mtasubiri, basi hakika hivyo ni bora zaidi kwa wanao subiri} [AN NAHL: 126].
Na Akasema: {Na malipo ya uovu ni uovu mfano wa huo. Lakini mwenye kusamehe, na akasuluhisha, basi huyo malipo yake yapo kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye hawapendi wenye kudhulumu} [ASH SHURAH: 40].
Ama mtu kuwa mwenye kudhulumiwa na Sharia ikamtaka kutojifanyia maudhui hili haliendani na nafsi zengine za wanadamu, kwani ni kauli ambayo haikubaliki na watu wengi, ikiwa atalazimishwa hivyo na ukasema: Hii ni amri ya Mungu basi huo ni msiba mkubwa huenda ukawatoa watu katika dini ya Mungu makundi kwa makundi ( ).


 

Share this:

Related Fatwas