Je! Mayahudi Walitaka Kumwona Mweny...

Egypt's Dar Al-Ifta

Je! Mayahudi Walitaka Kumwona Mwenyezi Mungu?

Question

Imekuja ndani ya Qur`ani Tukufu: {Na mlipo sema: Ewe Musa! Hatutakuamini mpaka tumuone Mwenyezi Mungu wazi wazi. Ikakunyakueni radi nanyi mnaangalia * Kisha tukakufufueni baada ya kufa kwenu, ili mpate kushukuru} [AL BAQARAH: 55 – 56].
Na imekuja pia ndani ya Qur`ani Tukufu: {Watu wa Kitabu wanakutaka uwateremshie kitabu kutoka mbinguni. Na kwa hakika walikwisha mtaka Musa makubwa kuliko hayo. Walisema: Tuoneshe Mwenyezi Mungu wazi wazi. Wakapigwa na radi} [AN NISAA: 153].
 

Answer

Huu ni mgongano kati ya Qur`ani na yaliyokuja ndana ya Kitabu Kitakatifu, kwani Kitabu Kitakatifu kinasema: “Wakamwambia Musa, sema nasi wewe, nasi tutasikia, bali Mungu asiseme nasi, tusije tukafa” Kutoka 20: 19.
Huenda msukumo wa kutaja hili ndani ya Qur`ani ni kuhofisha Waarabu ambao walimtaka Muhammad kuwateremshia kitabu kutoka mbinguni.

Kuondoa shaka:
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Aya hizi zimetaja baadhi ya mapendekezo ya Mayahudi ambayo yanaonesha juu ya kukufuru kwao na ubishi wao, baada ya Mwenyezi Mungu kuwaneemesha kwa kumuangamiza Firauni, na kuwaokoa kutokana na adhabu zake, na akawateremshia vitu vizuri, na waliletewa kiwingu ili kufunikwa na kivuli eneo la jangwani, hata hivyo hawakumshukuru Mwneyezi Mungu kwa neema hiyo bali walimpinga Mola wao, na wakasema kumwambia Musa: {Wakasema: Ewe Musa! Hebu tufanyie na sisi miungu kama hawa walivyo kuwa na miungu}[AL A'ARAAF: 138], Nabii Musa akawajibu: {Musa akasema: Hakika nyinyi ni watu msio jua kitu * Hakika haya waliyo nayo watu hawa yatakuja angamia, na hayo waliyo kuwa wakiyafanya yamepotea bure}[AL A'ARAAF: 138, 139], baada ya Musa kwenda kwenye ahadi ya Mola wake ndipo Mayahudi wakachukua mapambo yao na kutengeneza ng’ombe mwenye mwili na sauti wakiwa wanamuabudia kinyume na Mwenyezi Mungu, na wala hawakutosheka na hilo bali walitaka wamuone Mungu wazi wazi ili waamini yale waliyoletewa kutoka kwake, imani zao wakazitundika mpaka pale watakapomuona Mwenyezi Mungu Mtukufu, ndipo Mwenyezi Mungu akapeleka radi kali kutoka mbinguni ikiwa ni kuwatia adabu, kisha akawarudishia tena uhai baada ya radi hii ili wapate kushukuru.
Yanazingatiwa matakwa ya kumwona Mwenyezi Mungu Mtukufu ni jambo ovu linalowajibisha kuteremka radi na adhabu, kwa sababu kumuona hakutengani na upande wa kuwa na mwili na mengine katika mapungufu, na Mwenyezi Mungu Ameepukana na hali hizo. Mwenyezi Mungu Amesema: {Macho hayamfikii bali Yeye anayafikia. Naye ni Mjuzi Mwenye habari} [AL AN'AAM: 103].
Baada ya kurudi kwenye uhai kwa maombi ya Musa A.S. walimtaka aombe yeye kumuona Mungu na sio wao, ili yeye achukue nafasi yao ya kumuona Mungu kama vile alivyochukua nafasi ya kusikia kwake ufunuo sehemu ya kusikia kwao maneno ya Mwenyezi Mungu ili wamuamini, hivyo Nabii Musa A.S. hakuwa na matokeo isipokuwa kutangulia kuomba na akasema: {Mola wangu Mlezi! Nioneshe nikutazame} akajibiwa kwa kauli yake Mola Mtukufu: {Hutoniona}.
Ama kauli yao: Waisrael walihofia Mungu wala hawakutaka wamuone, na wakasema kumwambia Musa: Wakamwambia Musa, sema nasi wewe, nasi tutasikia, bali Mungu asiseme nasi, tusije tukafa”. Tunasema: Kauli yao hii ilikuwa baada ya kutaka kwao kumuona Mwenyezi Mungu Mtukufu na kuteremkiwa na radi, kisha kurudi tena kwenye uhai baada ya maombi ya Nabii Musa A.S. kinachoingia akilini kuwa ombi la kuacha kumuona haliwi isipokuwa ni baada ya kutokea jambo kubwa wakati wa kuomba kumuona, nalo ni lililozungumziwa na Qur`ani.
Na kauli yao: Ikiwa Kitabu Kitakatifu hakikutaja haya, tunasema: Kitabu Kitakatifu hakikutaja chochote mpaka tuseme kuwa hakikutaja kisa hiki pia, kwani kuna mambo mengi yamethibiti ambayo hayakutajwa na Kitabu Kitakatifu.
Na kauli yao kumwambia Musa: sema nasi wewe, nasi tutasikia, bali Mungu asiseme nasi, tusije tukafa” ndani yake yamo yanayoonesha yaliyotokea hapo nyuma pale walipotaka kumuona Mwenyezi Mungu, na kama sio hivyo basi wasingezungumzia kifo, ni vipi walifahamu kuwa ikiwa watataka kumuona Mwenyezi Mungu adhabu yao ni kifo, isipokuwa wakiwa wametanguliwa na uzoefu wa matokeo ya ombi hili, hivi inaingia akilini kuwa hawa wanapinga kumuona Mwenyezi Mungu Mtukufu na wao wanafahamika kwa sifa zao za ubishi kwa Mitume wao na kuwataka mambo mengi ya ajabu?
Ama kauli yao: Huenda msukumo wa kutajwa hili ndani ya Qur`ani ni kuwahofisha Waarabu ambao walimtaka Muhammad awateremshie kitabu kutoka mbinguni, tunasema: Waarabu hawakumtaka Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. kuwateremshia kitabu mpaka wapate hofu, lakini waliomtaka hilo ni watu wa kitabu – kwa andiko la Aya – na Aya inambainishia Mtume S.A.W. kuwa kuitikia ombi la hawa watu hakutatatua tatizo kwani wao hawataamini, hivyo kutajwa jambo la waliowatangulia miongoni mwa Mayahudi waliotaka makubwa zaidi ya waliyotaka Waarabu, kwani walitaka kumuona Mwenyezi Mungu Mtukufu.

 

Share this:

Related Fatwas