104- Je! Starehe za Peponi ni za Ki...

Egypt's Dar Al-Ifta

104- Je! Starehe za Peponi ni za Kimwili au Kiroho?

Question

104- Je! Starehe za Peponi ni za Kimwili au Kiroho? 

Answer

 Asili ya shaka:
Ndani ya Qur`ani Tukufu imekuja wasifu wa Peponi na watu wake:{Watakuwa juu ya viti vya fahari vilivyo shonwa * Wakiviegemea wakielekeana * Wakitumikiwa na wavulana wa ujana wa milele * Kwa vikombe na mabirika na bilauri za vinywaji kutoka chemchem safi * Hawataumwa kichwa kwa vinywaji hivyo wala hawatoleweshwa * Na matunda wayapendayo * Na nyama za ndege kama wanavyo tamani * Na Mahurulaini * Walio kama mfano wa lulu zilio hifadhiwa} [AL-WAAQIA: 15 – 23].
Pepo hii inakubaliana na mapenzi ya mwili na kukubaliana kwa kupenda vitu vinavyoonekana. Badala ya jangwa wameahidiwa Peponi {Inayopita chini yake mito} [AR-RAD: 35]. Badala ya kulala kwenye mchanga wameahidiwa peponi {Humo vimo viti vilivyo nyanyuliwa} [AL-GHASHIYAH: 13]. {Wakae juu ya viti vya enzi wakiangalia} [MUTAFIFIN: 23].
Badala ya kuvaa manyoya ya ngamia peponi wameahidiwa {Watapambwa humo kwa mapambo ya mikononi ya dhahabu na lulu. Na mavazi yao humo ni hariri} [AL-HAJ: 23]. Badala ya ukame peponi wameahidiwa pepo mbili zilizojaa matunda {Imo humo miti ya matunda, na mitende na mikomamanga} [AR-RAHMAAN: 68]. {Mizabibu}[AL-NABA': 32]. Badala ya hema ambalo halisaidii kupambana na joto la kiangazi wala baridi ya kifuku, peponi wameahidiwa majumba imara: {Ghorofa zilizo jengwa juu ya ghorofa} [AZ-ZUMAR: 20]. {Hawataona humo jua kali wala baridi kali} [AL-INSAN: 13]. Badala ya wanawake wa Kibedui wameahidiwa wanawake miongoni mwa Mahuru: {Na tutawaoza mahuru-l-aini} [AT-TWUR: 20]. {Watakuwemo wanawake watulizao macho yao, hajawagusa mtu kabla yao wala jini} [AR-RAHMAN: 56]. {Vijana * Wanapendana na waume zao, hirimu moja} [AL-WAAQIA: 36 – 37].
Badala ya kukosa huduma wameaihidiwa kuhudumiwa na vijana wakiwapatia vinywaji vyenye ladha: {Wakitumikiwa na wavulana wa ujana wa milele * Kwa vikombe na mabirika na bilauri za vinywaji kutoka chemchem safi} [AL-WAAQIA: 17 – 18]. {Na watawazungukia kuwatumikia wavulana wasiopevuka, ukiwaona utafikiri lulu zilizotawanywa} [AL-INSAN: 19]. Badala ya chakula duni peponi wameahidiwa nyama {Na tutawapa matunda, na nyama kama watavyo penda} [AT-TWUR: 22]. {Na nyama za ndege kama wanavyo tamani} [AL WAAGIA: 21].
Badala ya njaa umasikini na maisha magumu wameahidiwa peponi: {Ina mito ya maji yasiyo vunda, na mito ya maziwa isiyo haribika ladha yake, na mito ya mvinyo yenye ladha kwa wanywao, na mito ya asali iliyo safishwa} [MUHAMMAD: 15].
Yapo wapi haya kwenye kauli ya Masiha: “Kwa maana katika Kiyama hawaoi wala hawaolewi, bali huwa kama malaika mbinguni” Mathayo 22: 30. Na kauli yake: “Maana ufalme wa Mungu si kula wala kunywa, bal ni haki na amani na furaha katika Roho Mtakatifu” Warumi: 14: 17.
Kuondoa shaka: Kituo cha tafiti za Kisharia Ofisi ya Mufti wa Misri.
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Kwanza: Kusudio la Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa viumbe vyake ni kumuabudu na kuujenga uliwengu, lengo hili halifikiwi isipokuwa kwa ahadi ya Mwenyezi Mungu Mtukufu ya thawabu nyingi huko Akhera ahadi inayokubaliana na vile wavitakavyo na wavipendavyo katika aina zote za neema ziwe za kimwili au kiroho, miongoni mwa neema za kimwili ni neema zote za ladha ambazo Mwenyezi Mungu amezihalalisha, na jumla ya neema za ladha ima makazi au chakula au ndoa, hivyo Mwenyezi Mungu akasifu makazi kwa kauli yake: {Mabustani yapitayo mito kati yake} [AL-BAQARAH: 25]. Chakula: {kila watapopewa matunda humo, watasema: Haya ndiyo kama tuliyo pewa mwanzo} [AL-BAQARAH: 25]. Ndoa: {Na humo watakuwa na wake walio takasika} [AL-BAQARA: 25].
Kisha vitu hivi vinapopatikana linganisha na hofu ya kwisha au kuondoka, basi Mwenyezi Mungu akabainisha kuwa hofu hii kwao haipo akasema: {Na wao humo watadumu} [AL-BAQARAH: 25]. Hivyo Aya ikawa ni yenye kuonesha ukamilifu wa neema na furaha( ).
Ikiwa miongoni mwa watu wanamuabudu Mwenyezi Mungu Mtukufu wala hawana tamaa na pepo wala malipo ya Akhera bali wanamuabudu Mwenyezi Mungu kama Yeye tu ikiwa ni upendo kwake na ikiwa ni kujibu mazuri aliyomfanyia na kuwafanyia viumbe vyengine, watu wa aina hii ni wachache sana.
Na Mtume S.A.W. anasema: “Watu ni kama ngamia mia moja hukuti anayefaa kupandwa kwa ajili ya safari( )” watu wengi hawakubali kwa Mwenyezi Mungu isipokuwa kwa matumaini ya pepo au kuondokana na moto.
Pili: Mfananisho huu muulizaji anajaribu kuunganisha kati ya dini ya Uislamu na Waarabu wa zama za ujinga pamoja na hali ya maisha yao ya jangawani, majibu ya hayo ni kusema: Malipo ya waliyoahidiwa Waumini katika Aya nyingi za Qur`ani Tukufu sio kwa watu wa Makka na Madina tu miongoni mwa Waarabu ambao sifa zao zimetajwa katika shaka iliyotajwa, bali ni kwa Waumini wote na Waislamu ambao wanaishi maeneo yote ya dunia, je Waislamu wote hawa Mtume Muhammad S.A.W. amewaahidi starehe na neema sawa na tabu waliyoipata duniani kwenye makazi chakula na vinywaji.
Tatu: Ama kauli kuwa Qur`ani haikutaja kuwa peponi kuna furaha ya kiroho huo ni uzushi tu, kwani Mwenyezi Mungu ametaja ndani ya Qur`ani Tukufu neema zote za kiroho, na huenda kilele cha neema hii ya kiroho ni kumuona Mwenyezi Mungu Mtukufu peponi wala hakuna neema ya kiroho zaidi ya hiyo. Mwenyezi Mungu amesema: {Kwa wafanyao wema ni wema na zaidi. Wala vumbi halitawafunika nyuso zao, wala madhila. Hao ndio watu wa Peponi. Humo watadumu} [YUNUS: 26]. Wanachuoni wa tafasiri wamekubaliana kuwa kusudio la neno zaidi katika Aya Tukufu ni kumuona Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Imamu Al-Aaluusy R.A. anasema: Neno ziada kusudio ni kumuangalia Mola wao Mtukufu, nayo ni tafasiri iliyopokelewa kutoka kwa Abibakri na Ally radhi za Mola ziwe kwao, na Ibn Abbas, na Hudhaifah, pamoja na Ibn Masoud, Abi Musa Al-Ash’ary na wengine, imepokelewa kutoka kwa Mtume S.A.W. kwa njia tofauti, imepokelewa na Twayaalisy, pamoja na Ahmad na Muslimu pia Tirmidhy Ibn Majah Ibn Jariir na Ibn Mundhir Ibn Aby Haatim na Ibn Khuzaimat Ibn Habban na Abu Shaikh na Dar Qutwniy katika upokezi, na Ibn Mardawy pamoja na Baihaqy katika majina na sifa kutoka kwa Swuhaib, kuwa Mtume S.A.W. alisoma Aya hii {Kwa wafanyao wema……} akasema: “Pindi watu wa peponi watakapoingia peponi na watu wa motoni watakapoingia motoni muitaji ataita. Enyi watu wa peponi munayo ahadi kwa Mwenyezi Mungu na anataka kuwakamilishieni: Watauliza ni ipi hiyo? Kwani mizani zetu za matendo mema hazikuwa nzito na nyuso zetu hazikuwa nyeupe na hatujaingia peponi na kutuepusha na adhabu ya moto? Mtume S.A.W. akasema: Wataondolewa pazia kisha watamuona Mwenyezi Mungu Mtukufu, ninaapa kwa Mwenyezi Mungu kwamba Mwenyezi Mungu hajawapa kitu kinachopendwa zaidi kwao kuliko kumuona kwa macho yao”( ).
Nne: Muulizaji amechukua dalili kinyume na sifa za peponi zilizopokelewa ndani ya Qur`ani Tukufu kwa kutumia kwake Aya hizi mbili ndani ya Kitabu Kitakatifu, na Aya hizi mbili zinabeba maelezo na ufafanuzi ya kuwa maana ya kwanza: Hakuna katika ufalme wa Mungu – kwa maana ya Kiyama – chakula na kinywa bali ni wema na amani.
Ya Pili: Siku ya Kiyama hakuna kuoa wala kuolewa kwa maana ya ndoa kama vile ya duniani, na hasa imekuja kwenye Aya hii ikielezea ugonvi kati ya wanaume saba wote wameoa mwanamke mmoja na wanauliza atakuwa ni mke wa nani huko peponi hivyo jibu linakuwa kwa maana hii( ).
Tano: Neema za peponi na adhabu za motoni ni tofauti na hali ya dunia kisha Wanachuoni Waislamu wamezuia kupima kitu kisichoonekana na kinachoonekana kwa maana kutolea ushahidi hali za duniani kwa hali za Akhera, kwa sababu ulimwengu wa Akhera si kipimo cha watu wa duniani.
Siri ya watu wa peponi kuneemeshwa vile walivyovizoea duniani.
Hakuna shaka kuwa kuneemeshwa vitu sawa na vile mwanadamu alivyovizoea duniani ni katika neema yenye nguvu zaidi kuliko kitu asichokizoea mwanadamu duniani, kwa sababu hiyo Hadithi ya mnyama aina ya kenge imekuja Mtume S.A.W. amesema: “Hapana bali hakuwa maarufu kwenye ardhi za watu wangu (Makka) na kujikuta namchukia”( ).
Sheikh Twahir Ibn Ashuur R.A. anasema: “Kilichowekwa ndani ya nafsi ni kupenda hilo ima ni kwa sababu Mwenyezi Mungu Mtukufu ameandaa neema za waja wema peponi sawa na roho zao zilivyozoea hapa ulimwenguni, kwani kwenye mazoea kunapelekea umakini wa nafsi na roho vile zilivyokuwa hapa duniani, ulimwengu wa vitu vya kuonekana na kupata maarifa ya vitu hivyo bado sisi tunahitaji vitu hivyo na kuvizingatia ni neema kubwa, kwa sababu hiyo Mwenyezi Mungu ameandaa neema za kudumu katika sura hiyo, ima ni kwa sababu Mwenyezi Mungu Mtukufu amezipendezesha roho vitu hivi duniani, na ni kwa sababu vipo kama vile vilivyozoeleka katika ulimwengu wa juu kabla ya kuteremka mwilini kwa kuzoeleka kwake hivyo katika ulimwengu wa mfano, na sababu ya kutokuwa katika maumbile ya ajabu ni kutozoeleka kwake kuwa mfano wa vilivyopo katika ulimwengu” ( ).

 

Share this:

Related Fatwas