108- Je, Mwenyezi Mungu Amehalalish...

Egypt's Dar Al-Ifta

108- Je, Mwenyezi Mungu Amehalalisha Mali za Watu?

Question

108- Je, Mwenyezi Mungu Amehalalisha Mali za Watu? 

Answer

 Matni yenye Shaka: Imekuja ndani ya Qur'ani Tukufu:
{Na jueni ya kwamba ngawira mnayo ipata, basi sehemu moja ya tano ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na Mtume, na jamaa, na mayatima, na masikini, na wasafiri, ikiwa nyinyi mmemuamini Mwenyezi Mungu na tuliyoyateremsha kwa mja wetu siku ya kipambanuo, siku yalipo kutana majeshi mawili. Na Mwenyezi Munguni Muweza wa kila kitu} [AL ANFAAL: 41].
Na kauli ya Mola Mtukufu: {Basi kuleni katika mlivyo teka, ni halali na vizuri, na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe na Mwenye kurehemu} [AL ANFAAL 69]
Jibu la Shaka:
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
1- Sharia kawaida ni yenye kufaa:
Swala la kumiliki ngawira halihusishi tu Sharia hii ya Kiislamu bali Kitabu Kitakatifu kinatuelezea kuhusu Sharia zilizotangulia kuwa watu wake walimiliki mali za ngawira ni sawa sawa walinufaika nazo au hapana, ndani ya Kitabu cha Kumbukumbu la Torati: “Pamoja na nyara za miji tuliyoitwaa…..hapakuwa na mji uliokuwa mrefu kutushinda Bwana Mungu wetu aliiweka wazi yote mbele yetu” kumbukumbu la Torati: 2: 35, 36. Na katika Kitabu cha Mwanzo kwenye sifa za Benjamini: “Asubuhi atakula mawindo na jioni atagawanya mateka” Mwanzo: 49: 27. Na ndani ya Kitabu Kitakatifu pia: “Kwa hiyo nitamgawia sehemu pamoja na wakuu, naye atagawanya nyara pamoja nao walio hodari” Isaya: 53: 12.
2- Ngawira ni sehemu ya mfumo wa Jihadi.
Tofauti ni kubwa kati ya Sharia ya Mungu ya utatuzi wa ngawira na hayo matumizi ya kishenzi ambayo yanahalalisha mali za watu na damu zao, na kwa vile ngawira ni mali wanayoipata Waislamu katika zile wanazoziacha makafiri baada ya kumalizika kwa vita, hivyo kumiliki mali hizo na njia ya kuzigawa ni sehemu ya mfumo wa Sharia za Jihadi kuu na Jihadi ndogo, na kwa vile Sharia ya Jihadi imekutana na vigezo vya ukuzaji kuepukana na kuwa kwake mapigano kwa ajili ya damu bali imepanda na kuwa ni chombo cha malezi ya mwanadamu na kuondolea dhuluma na kuleta uadilifu na uhuru, kisha Sharia ya ngawira ikaja kwa mlango huu.
3- Kulinda mali za watu na maisha yao ni makusudio ya Kiislamu hata katika vita.
Na vipi Sharia iwe ina halalisha mali za watu? Na sisi ni wenye kuamrishwa kulinda mali za watu na maisha yao wawe Waislamu au makafiri wote ni sawa, hata katika hali ya Jihadi, na kisha yakaja makatazo ya kuuwa wanyama bila ya masilahi yeyote na kuchoma moto miti, kuharibu mazao ya shambani na matunda, maji kuchafua visima na kubomoa nyumba, na je inaendana na mtu aliyeharamishiwa mambo haya wakati wa vita kusema kuwa: Unahalalisha mali za watu, hapana.
4- Ngawira Sharia nzuri ya kimalezi:
Ni pande mbili tofauti kati ya kupora mali za watu ikiwa ni vitendo vinavyofanywa na baadhi ya watu au mauaji yanayofanywa na mashetani wao na kati ya Sharia inayolea mwanadamu kudhibiti nafsi yake na kuachanisha na matamanio yake na kuirejesha kwenye kumtii Mwenyezi Mungu, na katika hilo:
- Malezi ya kuacha kutaka ngawira bila ya kutegemea yaliyopo kwa Mwenyezi Mungu:
Kutoka kwa Abi Musa Al-Ash’ary R.A amesema: Mwarabu mmoja alimuuliza Mtume S.A.W kuwa: “Mtu anayepigana kwa ajili ya ngawira, na mtu anayepigana ili kukumbusha, na mtu anayepigana ili nafsi yake ipate kuonekana, ni yupi yupo katika njia ya Mwenyezi Mungu? Mtume SAW akasema: “Mwenye kupigana kwa ajili ya neno la Mwenyezi Mungu kuwa juu zaidi huyo ndio yupo katika njia ya Mwenyezi Mungu” ( ).
Kisha Mwenyezi Mungu amewahimiza Waumini kuwa ngawira isijekuwa sababu ya mivutano kati yao, hivyo Mola Mtukufu akasema katika Aya za mwanzo za Suratul-Anfaal:
{Wanakuuliza juu ya Ngawira ( ). Sema: Ngawira ni ya Mwenyezi Mungu na Mtume. Basi mcheni Mwenyezi Mungu na suluhisheni mambo baina yenu, na mtiini Mwenyezi Mungu na Mtume wake ikiwa nyinyi ni Waumini} [AL ANFAAL 01]
- Malezi kuwa ugawaji wa ngawira unarejea kwenye Sharia Tukufu na wala si matamanio ya nafsi:
Kisha Aya Tukufu imekuja:
{Na jueni ya kwamba ngawira mnayo ipata, basi sehemu moja ya tano ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na Mtume, na jamaa, na mayatima, na masikini, na wasafiri, ikiwa nyinyi mmemuamini Mwenyezi Mungu na tuliyo yateremsha kwa mja wetu siku ya kipambanuo, siku yalipo kutana majeshi mawili. Na Mwenyezi Munguni Muweza wa kila kitu} [AL ANFAAL: 41]. Ni jambo la ugawaji wa ngawira kwa mujibu wa mfumo ambao umewekwa na Mola wa viumbe vyote na wala si mapenzi na matakwa ya mtu, kisha mwanadamu anatoka kwenye kusudio na kulingania matamanio na upuuzi na kuelekea kwenye kusudio la Mwenyezi Mungu ambalo ni kulingania maendeleo.
Hivyo limekuja pia suala la uharamu wa kuchukuwa ngawira kabla ya kugaiwa kwa mgao wa Kisharia, angalia ni vipi mwanadamu si halali kwake kumiliki alichokipata wakati wa vita mpaka Sharia imruhusu! Mola Mtukufu Amesema:
{Na haiwezekani kwa Nabii yeyote kufanya hiyana. Na atakaye fanya hiyana, atayaleta Siku ya Kiyama aliyo yafanyia hiyana, kisha kila mtu atalipwa kwa aliyoyachuma, kwa ukamilifu; wala hawatadhulumiwa * Je! Aliye yafuata ya kumridhisha Mwenyezi Mungu ni kama yule aliye stahiki hasira za Mwenyezi Mungu, na makazi yake yakawa Jahannamu? Napo ni mahala pabaya pa kurejea} [AAL IMRAAN: 161 – 162].
- Malezi ya ujenzi wa jamii na kutoharibu mali:
Hilo ni kwa njia ya kunufaika na mali ambazo zinapatikana vitani na kurejesha matumizi yake kwenye manufaa ya jamii, na wewe pindi utakapozingatia mfumo wa matumizi ya ngawira utakuta haizingatiwi kuwa ina manufaa kwa kikundi cha watu wenye kuhitaji au kusaidia ujenzi.
Na hii ndio sauti ya akili iliyosalama ambapo haingii akilini Sharia kuhukumu kupotezwa mali hizi au kuharibiwa na sisi wafuasi wa dini haipaswi kuiharibu.

Share this:

Related Fatwas