Je. Mwenyezi Mungu Anataka Kuangam...

Egypt's Dar Al-Ifta

Je. Mwenyezi Mungu Anataka Kuangamiza Watu?

Question

  Je. Mwenyezi Mungu Anataka Kuangamiza Watu?

Answer

Matni yenye Shaka:
Imekuja kauli Tukufu ya Mwenyezi Mungu ndani ya Qur'ani:
{Na pindi tukitaka kuuteketeza mji huwaamrisha wale wenye starehe, lakini wao huendelea kutenda maovu humo. Basi hapo kauli huthibiti juu ya mji huo, nasi tukauangamiza kwa maangamizo makubwa} [AL ISRAA: 16].
Je Mwenyezi Mungu anataka kuangamiza watu? Na je anawaamrisha walioneemeka kufanya vitendo viovu ili wastahiki adhabu wakiwemo na watu masikini miongoni mwao? Na je hili linakubaliana na uadilifu wa Mwenyezi Mungu Utakasifu wake na Uaminifu wake? Ni vipi Mwenyezi Mungu hunasibishwa na uovu ufasiki na dhuluma?
Na je Qur'ani inapingana kwenye hili na kauli yake:
{Wala msifuate nyayo za Shetani. Hakika yeye ni adui yenu aliye wazi * Yeye anakuamrisheni maovu na machafu, na mumsingizie Mwenyezi Mungu mambo msiyo yajua} [AL BAQARAH: 168 – 169].
Na kauli yake:
{Hakika Mwenyezi Mungu anaamrisha kufanya uadilifu, na hisani, na kuwapa jamaa; na anakataza uchafu, na uovu, na dhuluma. Anakuwaidhini ili mpate kukumbuka} [AN NAHLI: 90].
Na kauli yake Mola Mtukufu:
{Na wanapo fanya mambo machafu husema: Tumewakuta nayo baba zetu, na Mwenyezi Mungu ametuamrisha hayo. Sema: Hakika Mwenyezi Mungu haamrishi mambo machafu. Mnamzulia Mwenyezi Mungu msiyoyajua?} [AL AARAF: 28].
Kuondoa Shaka:
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Mashirikiano ya Mwenyezi Mungu kwa waja wake ni kati ya huruma na uadilifu:
Tumejifunza ndani ya Qur'ani kuwa Mwenyezi Mungu anapenda huruma kwa waja wake na uongofu, sisi kusoma kwetu tunaanza na Bismillah Rahman Rahim, kwa maana hakika Mwenyezi Mungu ameridhia kwenye Kitabu chake kuanza kukisoma kwa sifa yake ya Rahman kwa maana ya mwingi wa huruma, na maana hii inaendelea katika Aya zingine za Kitabu Kitukukfu. Mwenyezi Mungu Amesema: {Mwenyezi Mungu hakuadhibuni mkimshukuru na mkamuamini. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kupokea shukrani na ndiye Mwenye kujua} [AN NISAA: 147]. Na akasema tena:
{Mwenyezi Mungu anakutakieni yaliyo mepesi wala hakutakieni yaliyo mazito, na mtimize hiyo hesabu, na mumtukuze Mwenyezi Mungu kwa kuwa amekuongoeni ili mpate kushukuru} [AL BAQARAH: 185]. Na akasema Mola Mtukufu: {Wala Sisi hatuadhibu mpaka tumpeleke Mtume} [AL ISRAA 15]. Hii ndio hali ya Mwenyezi Mungu katika mashirikiano yake kwa waja wake.
Lakini, hivi ikiwa ndio inapelekea huruma hivyo uadilifu wa Mungu unapelekea kuwepo kwa kanuni zinazotumika kwenye mfumo wa maisha, miongoni mwa kanuni hizo – ambazo zinaitwa mfumo wa Mungu – ni kuwa waja pindi wanapozidi kushughulishwa na maisha pamoja na mapambo yake kuliko kushughulishwa na kumuabudu Muumba na kutakasa nafsi pamoja na kuijenga sayari ya ardhi basi uharibifu huu unakuwa ndio sababu ya kuangamia kwao, na haya ndio yanayoelezewa na Aya Tukufu bali yanaelezewa na Aya zingine zisizo za Qur'ani.
Inafahamika kuwa Qur'ani Tukufu inahimiza kwenye mwenendo wa Mwenyezi Mungu kwa wenye kusimamia mambo ya jamii na kutopotoka kwa kuingia kwenye tabia chafu na kuzibeba tabia hizo kwa kigezo cha kupotoka pamoja nao, ikiwa Mwenyezi Mungu atataka kuwachukuwa kwa kuwaangamiza au kuwachukuwa kwa kuwatia adabu kwa kuongozwa na matamanio yao na kupelekwa kwenye vitendo viovu au kwenda kwenye maovu ya kijamii. Mola Anasema:
{Kadhalika katika kila mji tumewajaalia wakubwa wa wakosefu wao wafanye vitimbi ndani yake. Na wala hawafanyi vitimbi isipokuwa nafsi zao, nao hawatambui} [AL AN'AAM: 123].
Na Anasema:
{Na pindi tukitaka kuuteketeza mji huwaamrisha wale wenye starehe, lakini wao huendelea kutenda maovu humo. Basi hapo kauli huthibiti juu ya mji huo, nasi tukauangamiza kwa maangamizo makubwa} [AL ISRAA: 16].
Aya hizi mbili Tukufu zimebainisha kuwa mwenendo wa Mwenyezi Mungu ambao mamlaka yake huwa ndani ya jamii kwenye hatua za kuporomoka na kuharibika hubainisha kuwa kuporomoka huko na kuharibika kunaanza na kugawanyika kwa jamii kwenye mataifa, na kuharibika huku ikiwa kutatokea hakuhusishi upande au kikundi bali hufika kwa wote, na Aya ya pili ( ) inaongeza kuwa uharibifu ndio sababu yenye nguvu na ya haraka sana na ni sababu mbaya ya mgawanyiko wa kijamii, kwa sababu kuzama kwenye matamanio na kushibisha hisia kunaua hali ya kuhisi majivuno na kuua hisia za nguvu na wivu, na kufanya maovu ni uwanja wa kushindana waovu hakuna yeyote anayeona umuhimu kuinua kichwa chake kupinga ( ).
Hakuna kati ya Aya kitu kinachopingana:
Aya za Qur'ani Tukufu kati yake hakuna kitu cha kupingana bali Aya moja inachukuwa nafasi ya nyingine ili kujenga mfumo kamili wa Qur'ani bali na kuwa Aya moja ni tafasiri ya Aya nyingine.
Miongoni mwa tafsiri hizi ambazo tunazo ni kauli ya Mwenyezi Mungu:
{Na pindi tukitaka kuuteketeza mji…..} [AL ISRAA: 16] Ni maelezo ya uadilifu ambayo Mwenyezi Mungu amejiandikia na akaamrisha waja wake katika kauli yake:
{Hakika Mwenyezi Mungu anaamrisha kufanya uadilifu na hisani…….} [AN NAHLI: 90].
Kama linavyoonekana hili katika Aya Tukufu pindi tunapoangalia – katika muundo wake – imekuja kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:
{Na pindi tukitaka kuuteketeza mji……..} [AL ISRAA: 16] mwishoni mwa kauli yake:
{Wala Sisi hatuadhibu mpaka tumpeleke Mtume} Israa: 15. Mwenyezi Mungu amesimamia kwa uadilifu wake na huruma yake kutoadhibu isipokuwa ni baada ya kuwepo hoja anatuma mtu wa kubainisha mambo ili watu wapate kwanza kufahamu sahihi katika batili na kutoangamiza waharibifu isipokuwa baada ya ufafanuzi.
Imamu Twahir anasema: “Huu ni ufafanuzi wa hukumu iliyotolewa inayokusudia kuwatisha viongozi wa washirikina na kuwabebesha matokeo ya upotoshaji wa wale ambao wamewapotosha, nayo ni kubainisha sababu za uhalali wa kuadhibiwa baada ya kupelekwa Mjumbe akachanganya ndani yake kitisho kwa waliopotea…..maana ni kuwa, kupelekwa kwa Mjumbe kunaendana na jambo la Sharia, na sababu ya kuangamia kwao baada ya kupelekwa Mjumbe ni kule kutofuata kwao yale Mwenyezi Mungu aliyowaamrisha kupitia sauti ya huyo Mjumbe ( ).
Maana ya Kauli Tukufu ya Mola: {Na pindi tukitaka kuuteketeza mji} [AL ISRAA: 16].
Pindi tunapotaka – Kupitisha kanuni ya uadilifu baada ya kufanyia kazi kanuni ya huruma – kwa kuangamiza watu wa kijiji au mji miongoni mwa walioeneza uharibifu kundi lenye kuharibu na kundi lingine halifanyi kazi ya kukataza uharibifu hatufanyi hivyo bila ya kutokea vitendo vya uovu au vya dhambi waliyoifanya bali tunawaletea hoja kubwa kuwa kupeleka kwao mtu wa kuwafikishia yale tuliyoamrisha kwake kuyafikisha lakini kwa uharibifu wao wamestahiki kauli ya kuangamizwa.
 

Share this:

Related Fatwas