Je! Mapigo ya Misri ni Tisa au Kumi...

Egypt's Dar Al-Ifta

Je! Mapigo ya Misri ni Tisa au Kumi

Question

Matni yenye shaka:

Ndani ya Qur`ani Tukufu imekuja kauli ya Mola: {Basi tukawapelekea tufani, na nzige, na chawa, na vyura, na damu, kuwa ni Ishara mbalimbali. Nao wakapanda kiburi, na wakawa watu wakosefu} [AL-AARAF: 133, kama ilivyokuja pia: {Na kwa yakini tulimpa Musa ishara tisa zilizowazi. Waulize Wana wa Israili alipo wafikia, na Firauni akawaambia: Hakika mimi nakuona wewe Musa umerogwa} [ISRAA: 101].

Answer

Inafahamika kuwa Mwenyezi Mungu aliwapiga Wamisri kupitia Musa mapigo kumi na wala sio matano kama ilivyokuja kwenye Aya ya kwanza na wala sio tisa kama ilivyokuja kwenye Aya ya pili, vilevile tofani haikutokea nchini Misri ndani ya zama za firauni bali lilikuwa ni tukio maarufu lililowandoa watu wa Nuhu.

Kuondoa Shaka:

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:

Ndani ya Aya hakuna kinachoonesha idadi maalumu ya miujiza:

Ndani ya Aya mbili zilizotajwa hakuna kinachoelezea idadi maalumu ya miujiza, kwani Aya ya kwanza haikutaja kabisa idadi kuongezea pia ndani yake kuna idadi ya miujiza, kama vile Aya ya pili – hata kama kutakuwa na idadi – lakini haikuainisha ni idadi ngapi ya miujiza ya Nabii Musa A.S. ambapo imeonesha kuwa kuhusisha kutaja idadi hakumaanishi kukanusha ongezeko la idadi ya miujiza.

Miujiza ya Nabii Musa ni mingi

Ishara ambazo Mwenyezi Mungu alimpa Nabii Musa ni nyingi amezielezea Imamu Ar-Razy kutokana na Aya za Qur`ani Tukufu ni kumi na sita:

Ya kwanza yake: Ni Mwenyezi Mungu Alimwondolea kitata kwenye ulimi wake. Ya pili: Fimbo kugeuka nyoka. Ya tatu: Nyoka kumeza kamba zao na fimbo zao pamoja na uwingi wake. Ya nne: Mkono mweupe. Tano zingine ni: Tufani nzige kunguni vyura na damu. Ya kumi: Kupasuka bahari, nayo ni kauli yake Mola: {Na pindi tulipoitenganisha bahari}. Ya kumi na moja: Jiwe, nayo ni kauli yake Mola: {Piga jiwe kwa fimbo yako}. Ya kumi na mbili: Mlima kuufanya kama kiwingu, ni kauli yake Mola: {Na pale tulipo unyanyua mlima juu yao ukawa kama kiwingu kilicho wafunika}. Ya kumi na tatu: Kumteremshia Manna na Salwa kwake na kwa watu wake, nazo ni vyakula vitokavyo Peponi. Ya kumi na nne na kumi na tano: Ni kuali yake Mola: {Na hakika tuliwaadhibu watu wa Firauni kwa miyaka ya ukame na kwa upungufu wa mazao}. Ya kumi na sita: Kuondolewa mali zao miongoni mwa mitende ngano vyakula sarafu za Dinar na Dananiir([1]).

Kwa nini Mwenyezi Mungu amehusisha Ishara Tisa?

Swali linabakia ni kwanini zimetajwa Ishara tisa ndani ya Aya mbili za Qur`ani Tukufu? Tunasema, hii ina maanisha kuwa miongoni mwa miujiza tisa ya Musa ni yenye sifa maalumu kwake tu na si kwa mwingine yeyote, baadhi ya Wanachuoni wa Tafasiri wamefanya jitihada za kuziainisha na kuonekana kuwa “Miujiza tisa ni weupe wa mkono” fimbo kugeuka nyoka, tufani, nzige, kunguni, vyura, damu mchanga, ukame na upungufu wa mazao, nayo yametajwa ndani ya Suratul-Aaraaf”([2]).

Na hii miujiza tisa inayoingia ndani yake mingine inayozidia wala yenyewe haingii kwenye miujiza mingine wala yenyewe kwa yenyewe haingiliani, kama vile miujiza hii tisa ina sifa ya pekee ya miujiza mingine ambayo Musa A.S. alipewa, nayo ni katika miujiza ambayo alipewa ili kupambana na firauni, na hiyo tofauti na ishara ambazo Mwenyezi Mungu alizituma kwa Wana wa Israel, kutajwa kwa miujiza tisa kumejirudia ndani ya Qur`ani sehemu mbili, sehemu ya kwanza ndani ya Aya ya Suratul-Israa: {Na kwa yakini tulimpa Musa ishara tisa zilizowazi. Waulize Wana wa Israili alipo wafikia, na Firauni akawaambia: Hakika mimi nakuona wewe Musa umerogwa} [ISRAA: 101].

Na sehemu ya pili ni Aya ndani ya Suratul-Namli: {Na ingiza mkono wako katika mfuko wako, utatoka mweupe bila ya maradhi. Ni katika Ishara tisa za kumpelekea firauni na watu wake. Hakika hao walikuwa watu waovu} An-Namli: 12.

Na Aya zote mbili zimekuja zikionesha majadiliano ya firauni watu wake na Nabii Musa A.S.

Ibn Kathiir anasema: “Nabii Musa A.S. alipewa Ishara zingine nyingi miongoni mwazo ni kupiga bahari kwa fimbo, kutoa maji, kufunikwa na kiwingu, kuteremshiwa vyakula vya aina ya Manna na Salwa na zisizokuwa Ishara hizo miongoni mwa zile walizopewa watu wa Israel baada ya kuondoka kwao nchini Misri, lakini hapa kutajwa Ishara tisa ambazo aliziona firauni na watu wake miongoni mwa wananchi wa Misri kwa macho yao, hivyo ikawa ni hoja kwao wakapingana nayo na kuzishambulia kwa kukufuru na kupinga([3]).

Tufani

Ama tufani iliyotajwa ndani ya Aya ya kwanza ni sehemu na wala sio tufani ambayo iliondoa ardhi ndani ya zama za Nabii Nuhu A.S. jambo la ajabu ni kuwa ndani ya Kitabu Kitakatifu umekuja utajo wa tufani ambayo ilitokea Misri ndani ya zama za firauni na firauni akataka msaada kwa Nabii Musa A.S. ili kuondoka kwa hii tufani, ni namna gani muulizaji anajisahau kwenye jambo kama hili?

Aliambiwa firauni: “Nawe je! hata sasa wajitukuza juu ya watu wangu, usiwape ruhusa waende zao? Tazama kesho wakati kuma huu, nitanyesha mvua ya mawe nzito sana, ambayo mfano wake haujawahi kutokea huko Misri tangu siku ile ilipoanza kuwa mpaka hivi sasa” Kutoka: 17 – 34.

 

([1]) Tafsiir Al-Kabiir 21/64.

([2]) Tafsiir Tahriir wa Tanwiir 15/ 225.

([3]) Tafasiri ya Ibn Katheer 3/66 na kuendelea, nalo ni jambo lisilojificha kwa mwenye akili.

Share this:

Related Fatwas