Maneno ya Upuuzi

Egypt's Dar Al-Ifta

Maneno ya Upuuzi

Question

Aya ya Qur'ani:

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Alif Laam Raa} ([1]).

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Alif Laam Mmiim} ([2]).

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Alif Laam Mmiim Raa}([3]).

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema tena: {Alif Laam Mmiim Swaad} ([4]).

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema tena: {Haa Miim}([5]).

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema tena: {Haa Miim A’ain Siin Qaaf} ([6]).

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema tena: {Swaad} ([7]).

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema tena: {Twaa Siin} ([8]).

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu Ameendelea kusema: {Twaa Siin Miim} ([9]).

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu Ameendelea kusema: {Twaahah} ([10])

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema tena: {Qaaf} ([11]).

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema tena: {Kaaf Haa Yaa A’in Swaad} ([12]).

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema tena: {Nuun} ([13]).

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema tena: {Yaasiin} ([14]).

 

[1] Yunus, Huud, Yusuf, Ibrahim, Hijri Aya za kwanza.

[2] Al-Baqarah. Aal-Imraan, Al-Ankabuut, Luqmaan, Sajdah. Aya za kwanza.

[3] Ar-Raad Aya ya kwanza.

[4] Al-Aaraaf Aya ya kwanza.

[5] Ghaafir, Fusswiat, Zughruf, Dukhaan, Jaathiyah na Al-Ahkaaf Aya za kwanza.

[6] As-Shuuraa Aya ya kwanza na ya pili.

[7] Swaad Aya ya kwanza.

[8] An-Namli Aya ya kwanza.

[9] As-Shauaraa Aya ya kwanza.

[10] Twaha Aya kwanza.

[11] Qaaf Aya ya kwanza.

[12] Maryamu Aya ya kwanza.

[13] Al-Qalam Aya ya kwanza.

[14] Yaasiin Aya ya kwanza.

Answer

Madai ya mwenye shaka:

Katika ufunguzi wa Sura 29 za Qur'ani Tukufu zimeanza na herufi za kipuuzi hazifahamiki maana yake, sisi tunauliza: Ikiwa herufi hizi hakuna anayefahamu maana yake isipokuwa Mwenyezi Mungu “Kama wanavyosema” basi kwetu sisi faida yake ipo wapi? Kwa hakika Mwenyezi Mungu hateremshi ufunuo isipokuwa wenye faida, na maneno ya Mwenyezi Mungu ni ufikishaji na ubainifu lakini pia ni uongofu kwa watu ([1]).

Shaka:

Ndani ya Qur'ani Tukufu kuna maneno hayafahamiki na muulizaji anayaita meneno ya upuuzi ambayo hayana maana kabisa.

Historia ya Shaka:

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:

Imamu Razy ametaja kuwa baadhi ya wapinga dini wa zama zake walikuwa wanapinga Qur'ani Tukufu kwa kuwa ndani yake kuna mambo yenye kuleta shaka miongoni mwa hayo ni pamoja na hizi herufi za kukata za mwanzoni mwa Sura akasema: Miongoni mwa wapinga Mungu wapo waliopinga yaliyomo ndani ya Qur'ani kwa sababu ya kukusanya kwake mambo yanayoleta shaka, akasema: Nyinyi munasema: Amri za Muumba zinafungamana na hii Qur'ani mpaka siku ya Kiyama, kisha sisi tunaona kila mwenye madhehebu anashikamana na madhehebu yake.

Baadhi ya wasomi wanaojihusisha na elimu ya watu wa Mashariki wamezungumzia herufi za kukata zilizopo mwanzoni mwa Sura za Qur'ani Tukufu na wakapinga yaliyomo ndani ya Qur'ani wakasema zenyewe zilikuwa ni alama za majina ya wenye Misahafu miongoni mwa Maswahaba Watukufu, kisha wakazingatia kwa njia ya makosa kuwa ni Qur'ani, hivyo zikaongezwa kuandikwa kwenye Msahafu. Miongoni mwao wapo waliosema kuwa: Herufi hizi zimetokana na Tasawufi ya Kiyahudi pindi Mtume alipojiweka karibu na Wayahudi, miongoni mwa wasomi hawa akiwemo Lotte na pia Noldeke ambaye alisema kuwa: Herufi hizi ni ishara na alama zilikuwa zinamilikiwa na wale wenye misahafu ambazo Zaidi Ibn Thabit R.A alizikusanya baadaye na kuzitumia katika kutengenezea chapa yake ya msahafu ambayo alipewa jukumu la kukusanya, kwa mfano alama ya Zubeir Ibn Al-Awam ilikuwa ni {Alif Laam} na {Alif Laam Miim Raa} ni alama ya Mughiirah Ibn Shuubah, na alama ya {Haa Miim} ilikuwa ya Abdurahman, mtazamo huu umeelezewa pia na Hirschfeld ([2]).

Kitabu cha Ukweli wa Uislamu kilijibu shaka hizi katika kupambana na shaka za wenye kuleta shaka ([3]).

Juhudi za Wanachuoni katika kuondoa shaka:

Ama kuhusu hizi herufi ambazo zimeanza mwanzoni mwa baadhi ya Sura za Qur'ani, umma ulioteremshiwa Qur'ani kwa lugha yake ya Kiarabu umefahamu maana zaidi ya ishirini ya hizo herufi ([4]), na bado tafiti mpya za Qur'ani zinaongeza mapya kwenye maana ya hizo herufi ambazo zimezingatiwa na watu wa zamani, lau zingelikuwa za “Kipuuzi” kama anavyodai mgonvi wa Uislamu basi hakuna yeyote angelifahamu maana hata moja ([5]).

Na Imamu Zamakhshary anaona kuwa katika herufi hizi kuna siri ya ndani sana miongoni mwa siri za muujiza mkali wa Qur'ani, na ufipi wa mtazamo wake tunauelezea kama ifuatavyo:

“Fahamu kuwa ikiwa utazingatia kwa kina zile herufi alizozileta Mwenyezi Mungu Mtukufu mwanzoni mwa baadhi ya Sura za Qur'ani basi utakuta nusu ya herufi za kamusi ni sawa sawa herufi kumi na nne, nazo ni: Alifu Laam Miim Swaad Raa Kaaf Haa Yaa Ain Twaa Siin Haa Qaaf na Nuun, ndani ya Sura ishirini na tisa sawa na herufi za kamusi”.

Kisha ikiwa utaangalia katika hizi kumi na nne utazikuta zimekusanya usawa wa aina za herufi, ufafanuzi wa hilo ni kuwa: Miongoni mwa zisizo za sauti nusu yake ni: “Swaad Kaaf Haa Siin na Khaa”.

Na miongoni mwa herufi za sauti nusu yake ni: Alif Laam Miim Raa Ain Twaa Qaaf Yaa na Nuun.

Na miongoni za kukaza nusu yake ni: Alif, Kaaf, Twaa na Qaaf. Na miongoni za kulegeza nusu yake ni: Laam, Miim, Raa, Swaad, Haa, Ain, Siin, Haa, Yaa na Nun. Na miongoni zenye kufanyiwa kazi nusu yake ni: Swaad na Twaa. Na zilizofunguka nusu yake ni: Alif, Laam, Miim, Raa, Kaaf, Haa, Ain, Siin, Haa, Qaaf, Yaa na Nun. Na miongoni zenye sifa ya juu nusu yake ni: Qaaf, Swaad na Twaa. Na miongoni zenye sifa ya kupungua nusu yake ni: Alif, Laam, Miim, Raa, Kaaf, Haa, Yaa, Ain, Siin, Haa na Nun. Na katika herufi za kugonga nusu yake ni: Qaaf na Twaa.

Anataka kusema: Herufi hizi zilizotajwa zinazingatiwa mazingatio mawili ya kimiujiza:

Zingatio la Kwanza: Ni kwa upande wa idadi ya herufi za Kiarabu, nazo ni herufi ishirini na nane, herufi hizi zilizotajwa mwanzoni mwa funguzi za Sura ni sawa sawa na nusu ya herufi za Kiarabu, kwa maana herufi zilizotajwa ni herufi kumi na nne na ambazo hazikutajwa ni kumi na nne: 14+14=28, ndio idadi ya herufi za Kiarabu.

Zingatio la Pili: Ni kwa upande wa sifa za herufi ambazo: Ukimya mkabala wa sauti, za kukaza mkabala zilizo laini, kutekelezwa mkabala za uwazi, zilizo juu mkabala zilizochini, za kugonga mkabala na zengine. Tunakuta herufi hizi zilizotajwa mwanzoni mwa ufunguzi wa baadhi ya Sura za Qur'ani ni sawa sawa na nusu ya herufi kila sifa miongoni mwa sifa saba zilizotajwa, na sifa hizi na yanayozingatiwa miongoni mwa kuendana kwa kina kati ya zilizotajwa na zilizoachwa, haipatikani isipokuwa katika maneno ya Mwenyezi Mungu yaliyoteremshwa kwa Muhammad S.A.W nazo ni zenye muujiza mkubwa kwa wenye ufahamu, hivyo tunaona Imamu Zamakhshary anasema akielezea ujuzi huu wenye hekima: Ametakasika yule ambaye ameboresha kila kitu kwa hekima zake kwa kina, nayo ni yenye kufanya kazi kwa kundi la walioteremshiwa, kana kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu jina lake sawa na idadi ya herufi za Kiarabu ambazo miongoni mwake mpandano wa maneno yao, ikiwa ni ishara ya yaliyotajwa miongoni mwa mafokeo kwao na kulazimisha hoja zao, na kuna siri za kundi lingine amelitaja Imamu Zamakhshary, na Shairf katika kitabu chake ambacho amekiweka kwenye tafsiri ya Kashaaf basi na arejee huko.

Kuondoa shaka:

Kwanza: Hakuna katika maneno ya Mwenyezi Mungu wala ndani ya Kitabu cha Mwenyezi Mungu maneno ya upuuzi yasiyo na maana lakini kila herufi za Kitabu cha Mwenyezi Mungu zina maana. Mtume S.A.W alisema kutoka kwa Abdillah Ibn Masoud anasema: Mtume S.A.W amesema:

 “Mwenye kusoma herufi moja ya Kitabu cha Mwenyezi Mungu basi kwa herufi hiyo amefanya jambo jema na jambo jema moja lina thawabu kumi sisemi Alifu Laam Miim ni herufi moja bali Alifu herufi Laam herufi na Miim herufi([6]).

Pili: Wanachuoni wa Sharia wamekubaliana kuwa haifai Mwenyezi Mungu azungumze kitu kisicho na maana yeyote, dalili ya hilo ni kuwa kuzungumza bila ya kuwa na faida ni kuchanganyikiwa na kuchanganyikiwa ni sifa pungufu na upungufu kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu ni kitu kisichowezekana ([7]).

Tatu: Mwenyezi Mungu Mtukufu ameielezea Qur'anii Tukufu kuwa ni uongofu ponyo na ufafanuzi hivyo haiwezi kuwa na kitu kisichofahamika maana yake. Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema:

{Sema: Hii Qur'ani ni uwongofu na poza kwa wenye kuamini. Na wasio amini umo uziwi katika masikio yao, nayo kwao imezibwa hawaioni. Hao wanaitwa nao wako pahala mbali} ([8]).

Mola Mtukufu Mtukufu Amesema tena:

{Enyi watu! Umekufikieni ushahidi kutoka kwa Mola wenu Mlezi. Na tumekuteremshieni Nuru iliyowazi} ([9]).

Mwenyezi Mungu amesema tena:

{Enyi watu! Yamekujieni mawaidha kutoka kwa Mola wenu Mlezi, na poza kuponesha yaliyomo vifuani, na uwongofu, na rehema kwa Waumini} ([10]).

Nne: Wanachuoni wamekubaliana kuwa ufunguzi huu kwa hizi herufi kuna maana yenye kuzingatiwa lakini miongoni mwazo wamesema kuwa maana hii haifahamiki kwa watu hata Wanachuoni miongoni mwao, na hilo  la  kufahamika kwa watu ni kiwango kidogo cha maarifa. Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema: {Nanyi hamkupewa  katika ilimu ila kidogo tu}([11]).

hii si sifa mbaya kwa mwanadamu wala si kuonekana ni viumbe wajinga na wala si kuzungumzishwa kwa jambo lisilo na faida bali ni lenye faida hata kwa muundo huu ambao unaonekana kuwa maana ya herufi hizi umejihusisha kwake Mwenyezi Mungu Mtukufu na elimu yake, faida hii ni kufikiwa kwa imani ya mambo yasiyoonekana na imani kwa Mwenyezi Mungu na kwa Sifa zake Tukufu.

Tano: Jopo la Wanachuoni wamekubaliana kuwa zenyewe zina maana yenye kufahamika na kuzingatiwa Mwenyezi Mungu anaifungua maana hiyo kwa mtu amtakaye katika waja wake kutokana na Mwenyezi Mungu kuwa mbali na kuwaambia waja wake kitu wasichakifahamu, kisha Wanachuoni wakatoa maelekezo mbali mbali kwenye funguzi hizi miongoni mwa maelekezo hayo:

  • Kuwa ni majina ya Sura.
  • Ni herufi zimekuja ili kuleta tahadhari, zenyewe ni sauti zenye kuleta mazingatio kwa wasikilizaji…..hivyo baadhi ya wasomaji wa herufi hizi za katika funguzi za Sura huita “Mdundo” ([12]).
  • Wengine wamesema zenyewe ni kwa ajili ya kiapo.
  • Na wengine wamesema ni mafupisho ya maneno ndani ya Qur'ani Tukufu.
  • Na wengine wamesema zenyewe ni kwa ajili ya kutenganisha kati ya sura.
  • Na wengine wamesema ni Majina ya Mwenyezi Mungu Mtukufu mfano kama vile “Alif Laam Miim” na “Alif laam Raa” na “Alifu Laam Miim Swaad” zinaashiria miujiza ya Qur'ani kuwa yenyewe imetungwa kutokana na herufi ambazo Waarabu wamezifahamu na wakatengenezea maneno na wakatengeneza kutokana na maneno hayo miundo, na Qur'ani haikubadilisha chochote asili ya lugha na mada zake, pamoja na hayo Qur'ani imekuwa ni muujiza, si kwa sababu yenyewe imeteremka kwa lugha inayobadilisha lugha yao bali ni kwa sababu imeteremka kwa elimu ya Mwenyezi Mungu Mtukufu ([13]) haikuwa isipokuwa ni kuthibitisha kushindwa kana kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu anataka kuonesha kwa waja wake kuwa Qur'ani hii ambayo ipo mikononi mwao imetungwa kutokana na maneno yao wanayotungia, lakini pamoja na hivyo hawawezi kuleta mfano wake, na mwenye kuizingatia atakuta kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu ameifanya ya kudumu.
  • Wengine wamesema kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu ameitamka akiwa si mwenye kujua kusoma wala kuandika na hii inaleta ukweli wake ambapo asiyejua kusoma na kuandika hajui majina ya herufi bali anajua kuita kwake katika maneno nalo ni jambo linalofanana na kauli ya kushindwa.

Mwenye kuzingatia kauli hizi atakuta kuwa ni katika tofauti za kiaina na wala si tofauti za kinyume inawezekana kuzikusanya kati yake kwa sababu ni katika mlango wa alama na alama hazisongamani nayo ndio tunaona mapito mazuri zaidi na bora kukubalika. Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kujua zaidi.

Sita: Lau herufi hizi ni katika maneno ya upuuzi Waarabu wapinga ulinganiaji katika zama za kuteremka Qur'ani wasingeziacha, na wao ni mashahidi kwao wa ufasihi, na uwezo wa ufafanuzi wa Inshaa na uchambuzi, kwa kiwango cha upingaji wao wa Qur'ani lakini haijathibiti kwao kuwa wamezikosoa herufi hizi za ufunguzi wa baadhi ya Sura nao ni wajuzi katika eneo hili, wapo wapi wale ambao hivi sasa wanazuia kuichambua Qur'ani miongoni mwa wale ambao walikuwa wajuzi wakubwa wa sifa ya maneno na kasoro zake?

Qur'ani yenyewe imetaja upingaji wao ndani ya Qur'ani, wala haikutaja kuwa wao wamechukua kwenye Qur'ani uchukuwaji wowote ule, si katika maneno yake moja moja wala kwenye jumla zake, si katika muundo wake bali kinyume wamejisalimisha kwa kuitanguliza kwenye upande huu, na baadhi ya Waarabu wasiowaislamu wamesifu mfumo huu wa Qur'ani na wakauinua zaidi kuliko maneno ya watu na majini[14].

Na kwa athari yake kubwa kwenye nafsi wametosheka na kuusiana kati yao kutoisikiliza na kuifanyia fujo Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema:

{Na walio kufuru walisema: Msiisikilize Qur'ani hii na itimulieni zogo, huenda mkashinda} ([15]).

 

 

 

[1] Ukurasa wa 175 kitabu cha je Quran haina makosa?

[2] Quran Tukufu katika mtazamo wa wasomi wa Kimagharibi, utafiti chambuzi Dr. Muhammad Muhammad  Abu Lailah, chapa ya kwanza 2002, maktaba ya Dar An-Nashri Misri: Ukurasa wa 225 na kuendelea kwa ufupi sana.

[3] Kitabu cha Ukweli wa Uislamu ukurasa wa 60 na kuendelea.

[4] Tafasiri ya Imamu Razy 2/3 na kuendelea.

[5] Maneno ya Shaikh Ally kuhusu herufi za kukata zilizopo mwanzoni mwa Sura.

[6] Sunan Tirmidhy kitabu cha ubora wa Quran, mlango unaoelezea mwenye kusoma herufi moja ya Quran ana alipo. Hadithi nambari 2910, 5/175.

[7] Kitabu chaMahsuul Fii Elmu Al-Usuulul-Fiqh 1/169.

[8] Fussilat: 44.

[9] An-Nisaa: 174.

[10] Yunus: 57.

[11] Al-Israa: 85.

[12] Kusudio la mdondo, ni kupigia ardhini ikiwa ni kumzindua msikilizaji. Nukuu kutoka kitabu cha Hakaaik Al-Islaam 61.

[13] Hakaaik Al-Islaam 60.

[14] Miongoni mwa hayo yaliyopokelewa kwenye Hadithi 3872 kutoka kwa Akrama kutoka kwa Ibn Abbas Mwenyezi Mungu awawie radhi kuwa: Waliid Ibn Mughiirah alikuja kwa Mtume S.A.W akamsomea Qurani, taarifa hizi zikamfikia Aba Jahli akamuendea na kumuambia: Ewe ndugu yangu watu wako wanaona wakukusanyie mali, akauliza kwa nini? Akasema: Ili wakupe, kwani wewe umekwenda kwa Muahammad ili kumuelezea yaliyokuwa kabla yake, akasema: Makuraishi wanafahamu kuwa mimi ni mwenye mali nyingi, akamwambia: Toa kauli ya kuwafikishia watu wako kuwa wewe unampinga au unamchukia, akasema: Kitu niseme, kwani ninaapa kwa Mwenyezi Mungu hakuna miongoni mwetu mtu yeyote anayejua zaidi mashairi zaidi ya mimi wala kujua kuimba kaswida zaidi ya mimi, ninaapa kwa Mwenyezi Mungu hakuna mfanano wowote wa haya ambayo anayoyasema, kwani maneno yake ni matamu yenye haiba na yenye faida juu yake na chini yake, ni meneno yaliyojuu ya maneno yote, akasema: Watu wako hawatakuridhia mpaka useme hayo maneno, akasema: Basi nipe muda ili nifikiri, baada ya kufikiri akasema: Haya si chochote bali ni uchawi wa kunukuliwa kutoka kwenye uchawi mwengine, ndipo ikateramka kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: ذرني و من خلقت وحيدا {Niache peke yangu na niliyemuumba}. Imamu Al-Hakim amesema Hadithi hii ni upokezi sahihi kwa sharti la bukhary, kitabu cha tafasiri mlango wa tafasiri ya Suratul-Muddaththir. Hadithi nambari 3872 ukurasa wa 2/550. 

[15] Fussilat: 26.

Share this:

Related Fatwas