Kuwakataa kwa watu wenye msimamo mk...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kuwakataa kwa watu wenye msimamo mkali kuhusu elimu na akili ambayo Waislamu waliiingiza katika elimu zao na uhusiano wake na msimamo wao mkali na ukosefu wa ufahamu wao kwa dini.

Question

Je, kukataa kwa watu wenye misimamo mikali juu ya elimu na fikra ambayo Waislamu waliiingiza katika elimu zao kunaathiri msimamo wao mkali na kutofahamu kwao dini?

Answer

Kuwakataa kwa watu wenye msimamo mkali kwa elimu nafikra kuna athari kubwa katika msimamo wao mkali na ukosefu wa ufahamu wao kwa dini. Sayansi ya kiakili, kama vile sayansi ya mantiki, kwa mfano, ni kanuni zinazolinda akili dhidi ya kufikiri vibaya, kupuuza kanuni hizi husababisha kupotoka katika kuelewa matini za kisheria na kutambua ukweli, mambo ambayo yote mawili yana athari kubwa juu ya uwasilishaji sahihi wa hukumu ya kisheria. Kutokutambua tofauti kati ya asili ya ukweli ambamo matini iliteremshwa na asili ya ukweli wa sasa husababisha upotovu mwingi wa kiakili ambao ndio utangulizi muhimu zaidi wa fikra zenye misimamo mikali, na kama walivyotaja katika vitabu vya sayansi ya kimantiki: Kuhukumu jambo ni tawi la utambuzi wake, kwa hivyo ikiwa utambuzi ni wa makosa, basi hukumu hiyo ni potofu. Wanazuoni wa Kiislamu wamefanya kazi kwa karne nyingi kuzisafisha elimu za fikra kutokana na uchafu wake, na kisha kunufaika nazo katika kuimarisha muundo wa elimu zao. Na kama ilivyoelezwa katika Hadithi: “Hekima ni mali iliyopotea ya Muumini, huichukua popote anapoikuta”.

Share this:

Related Fatwas