Udanganyifu katika bidhaa waliokuba...

Egypt's Dar Al-Ifta

Udanganyifu katika bidhaa waliokubaliana kulipia

Question

Ni ipi hukumu ya udanganyifu katika bidhaa waliyokubaliana kulipia katika zabuni?

Answer

Udanganyifu katika bidhaa waliyokubaliana kulipia katika zabuni na mfano wake ni haramu Kisharia, ni kula mali kwa njia batili, na Uislamu umeharamisha kufanya udanganyifu na uwongo, Mtume S.A.W amesema:

 “Mwenye kutufanyia udanganyifu huyo si katika sisi”. Imepokewa na Imamu Muslimu.

Uislamu umewaamrisha Waumini kujipamba na sifa ya ukweli na wawe pamoja na watu wa kheri. Mwenyezi Mungu Mtukufu Akasema:

{Enyi mlio amini! Mcheni Mwenyezi Mungu, na kuweni pamoja na wakweli} Attawbah: 119.

Ukaamrisha kutekeleza masharti yaliyomo kwenye makubaliano. Mtume S.A.W akasema:

 “Waislamu wanatekeleza makubaliano yao isipokuwa ikiwa makubaliano yanayoharamisha halali au kuhalalisha haramu”. Imepokewa na Daaruqutwny.

Mwenyezi Mungu Anajua Zaidi.

Share this:

Related Fatwas