Mtazamo wa Kiislamu kwa nchi za uli...

Egypt's Dar Al-Ifta

Mtazamo wa Kiislamu kwa nchi za ulimwengu.

Question

Upi mtazamo wa Kiislamu kwenye zama za sasa kuhusu nchi za ulimwengu? Je ni mtazamo wa kiuadui kwa kila kisichokuwa cha Kiislamu?

Answer

Jibu:

Hivi sasa hali ya Kimataifa ikiwa pamoja na Mashirika na makubaliano ya Kimataifa, yameshiriki katika kuasisi hizi nchi na kuzipa uanachama pamoja na kutambua nchi zote za Kiislamu na kukubalika na Wanachuoni wa Umma na Majopo yao ya Kisharia, yote hayo yanalazimu mtazamo wa Ulimwengu kuwa ni nchi za amani na makubaliano, katika hayo ni pamoja na uwepo wa masilahi ya Waislamu mmoja mmoja na jamii, kwani wanasafiri Mashariki mwa dunia na Magharibi yake kwa usalama na amani, baadhi yao wakiwa wanaishi ndani ya nchi hazina hukumu za Uislamu lakini wanaishi wakifanya ibada kwa uhuru.

Mtume S.A.W. amesisitiza juu ya kuheshimu mwenye makubaliano naye – pamoja na kutokuwa Muislamu – damu yake na mali yake, akasema: “Fahamu mwenye kumdhulumu mtu mwenye makubaliano naye na kumpa jukumu la zaidi ya uwezo wake au akachukua kwake kitu bila ya ridhaa yake, basi mimi siku ya Kiyama mtetezi wake (mdhulumiwa), fahamu mwenye kumuuwa mtu mwenye makubaliano naye mwenye ulinzi wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake, Mwenyezi Mungu amemuharamishia hata harufu ya Pepo, na harufu yake inapatikana kwa mwendo wa miaka sibini” imepokewa na Baihaqy.

Masuala ya kukufurisha wengine – ni sawa sawa iwe watu jamii au nchi – kunapaswa kuwepo tahadhari, wala hakuwi isipokuwa kupitia Wanachuoni wenye weledi au mwenye mamlaka ya utoaji Fatwa na kunakuwa kwa kutolewa hukumu ya Kadhi anayetambulika, Imamu Ibn Hajar amesema: “Inapaswa kwa Mufti kuwa na tahadhari inayowezekana katika kukufurisha kutokana na ukubwa wa hatari yake na uwezekano mkubwa wa kutokusudia”.

Mwenye kupinga hili na kugeuza maisha ya watu basi huyo yupo nje ya mfumo wa Uislamu na Waislamu.

Share this:

Related Fatwas