Tafsiri ya kisayansi ya Qur’ani

Egypt's Dar Al-Ifta

Tafsiri ya kisayansi ya Qur’ani

Question

Ni ipi hukumu ya mtu anayesema: Nataka tafsiri ya kisayansi ya Qur’ani Tukufu?

Answer

Qur’ani Tukufu ni muujiza wa kiungu ambao unajitokeza upya kila baada ya muda, na tafsiri ya kisayansi ya Qur’ani Tukufu ina maana nyingi. Ikiwa imekusudiwa kuzifasiri Aya zake kwa njia na vidhibiti vinavyotambulika kisayansi, basi hivi ndivyo walivyofanya Waislamu katika zama zote, na kwa hiyo wakabainisha ulinganifu baina ya vitabu viwili vya Mwenyezi Mungu Mtukufu, vinavyoonekana na vilivyoandikwa.

Lakini ikiwa tafsiri ya kisayansi ya Qur’ani inakusudiwa kuiweka chini ya njia isiyoamini ghaibu, basi huku ni kutumia njia iliyo kinyume na imani katika kuamiliana na Qur’ani Tukufu.

Ama katika kuzitafiti

Aya za Qur'ani Tukufu ili kuwakusanya watu kutafuta hazina iliyofichwa humo katika zama zote, na kuthibitisha kuwa inavuka mipaka ya kiakili ya kila zama, ikiwa ni pamoja na zama za maendeleo ya kiteknolojia, hili ni jambo tunaloliona huku wakizingatia vidhibiti vilivyowekwa vya kushughulikia maneno na muktadha wake kwa mujibu wa Wanazuoni wa Kiislamu.

Kinachoenezwa chini ya jina (muujiza wa kisayansi) ni umbali na mzigo wa maneno ambayo wakati mwingine hayawezi kuvumiliwa, na hii ni jambo la kuhitajika juu yake. Kwa sababu Qur’ani ni kitabu cha mwongozo na nasaha, si kitabu cha sayansi ya majaribio, bali mambo haya yanakuja ndani yake kama marejeo na matokeo, si nia au asili.

Share this:

Related Fatwas