Watu kuchapisha maelezo ya maisha yao kwenye mitandao ya kijamii.
Question
Ipi hukumu ya watu kuchapisha historia ya maisha yao kwenye mitandao ya Kijamii?
Answer
Uchapishaji na urushaji “You Tube” video zinazoelezea historia ya maisha yao binafsi kwao na familia zao, ikiwa kwa kawaida ni video zenye aibu kuangaliwa na wengine au video chafu kama vile za uchi na mfano wa hayo, kuzirusha ni jambo lisilofaa Kisharia na ni jinai kisharia, kutokana na kueneza uovu katika jamii.
Ikiwa ni video zenye picha zinazofaa kuangaliwa na mwingine na urushaji wake ukawa ni kwa makusudio sahihi – kama vile kutoa uzoefu au majaribio ya jambo au kuelekezwa kwenye mlango miongoni mwa milango yak kheiri – basi hakuna kizuizi Kisharia, pamoja na kuzingatia kawaida na mazoea ya jamii katika hilo, na mrushaji awe ni mtu mwenye weledi katika anayoyazungumza na kuyarusha kwa watu.