Hukumu ya Swala pamoja na kupaka ku...

Egypt's Dar Al-Ifta

Hukumu ya Swala pamoja na kupaka kucha rangi

Question

Je ni haramu kuswali hali ya kuwa umepaka rangi za kucha?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema ni zake, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, Masahaba wake na wafuasi wake. Na baada ya hayo:

Ikiwa rangi ya kucha imewekwa baada ya kutawadha na twahara haijavunjika, basi swala ni sahihi. Lakini iwapo twahara inahitajika, basi asili yake ni kwamba rangi hiyo inapaswa kuondolewa ili twahara iwezekane.

Lakini ikiwa kuiondoa ni jambo gumu ambalo litasababisha mtu kuacha kuswali au kuchelewesha Swala hadi itoke nje ya wakati wake, basi inaruhusiwa kutia udhu huku rangi ikiwa bado ipo, kwa sababu kushikamana na ruhusa hii - hata ikiwa ni dhaifu - ni bora zaidi kuliko kuacha Swala au kuichelewesha nje ya wakati wake.

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.

Share this:

Related Fatwas