Kwenda Msikitini na Watoto

Egypt's Dar Al-Ifta

Kwenda Msikitini na Watoto

Question

Ni ipi Hukumu ya Kwenda Msikitini na Watoto

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, Maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:

Hakuna kizuizi kisharia Kwenda Msikitini na watoto, bali hilo linapendeza wakiwa wana ufahamu, ili kuwazoesha Swala na kuwakuza katika kupenda mazingira ya Imani ambayo yanawakusanya Waislamu katika kumwabudu Mwenyezi Mungu Mtukufu ili hili liwe sehemu ya kujenga utu wao hapo baadaye, na hii ni pamoja na kuchunga kuwafundisha adabu na kuwakataza kuwashughulisha wanaoswali au kucheza Msikitini. Kwa sharti kuwa hilo kwa upole na huruma, na kuamiliana na mtoto kwa upole wa hali ya juu na kumkunjulia kifua bila ya kumtia hofu na kumtisha; kwa sababu vitendo vya ukatili kwa watoto vinaweza kuwasababishia hofu na kutopenda sehemu hii tukufu, na asili ni mtoto kulelewa kwa kupenda sehemu hii na moyo wake ufungamane na nyumba ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, kama ilivyokuja Hadithi ya watu saba ambao Mwenyezi Mungu Atawapa kivuli chake. “Na mtu ambaye moyo wake una mapenzi na Msikiti”. Na Msikiti umejaa rehema na baraka.

Wanazuoni wametoa dalili ya kujuzu kwenda Msikitini na watoto kwa Hadithi nyingi, miongoni mwazo ni:

Hadithi iliyopokelewa na Bukhri na Muslim katika Sahihi zao, kutoka kwa Abu Qatadah Allah R.A. “Kwamba Mtume S.A.W. alikuwa anaswali akiwa amembeba Umama bint Zaynab binti wa Mtume S.A.W”

Al-Hafidh bin Hajar amesema: “Hadithi hii imetolewa dalili ya kujuzu kuingia Msikitini na watoto” ([1]).

Na Imamu Ahmad na Abu Dawoud na At-Tirmdhy na An-Nasaaiy na Ibnu Majah na Ibn Hibban na Al-Hakim wametoa kutoka kwa Barida RA. amesema: “Mtume S.A.W. alikuwa akihutubu, akaingia Hassan na Hussein Allah Awawie radhi wakiwa wamevaa kanzu nyekundu, wanatembea na wanajikwaa, Mtume akashuka juu ya membari akawabeba mmoja bega la kulia na mwengine bega la kushoto, kisha akapanda juu ya membari akasema: Amesema kweli Mwenyezi Mungu: {Hakika si vingine Mali zenu na Watoto wenu ni fitna} mimi nilipowatazama watoto hawa wakitembea na kujikwaa sikusubiri nikakata maneno yangu na nikashuka kuwafuata”.

Na katika Hadithi hizi mbili na nyinginezo Wanazuoni wamechukua kujuzu Kwenda Msikitini na watoto, na wakawatoa wale ambao hawaachi fujo hata wakikatazwa, pamoja na hilo lazima nasaha zao ziwe kwa upole.

Naye Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi

 

 


([1]) Fat-h Al-Bary, 1/592.

Share this:

Related Fatwas