Kuvunja Sheria ya Ukazi baada ya K...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kuvunja Sheria ya Ukazi baada ya Kutekeleza Ibada ya Umra nchini Saudia Arabia

Question

Ipi hukumu ya anayekwenda Makka kutekeleza Ibada ya Umra katika mwezi wa Ramadhani kisha akavunja sheria ya ukazi ili atekeleze Ibada ya Hija akijificha asionekane na polisi; kwa sababu mamlaka zinakataza kufanya hivyo, na miongoni mwa watu hawa wapo wanaodai kwamba wamepata Fatwa kutoka kwa baadhi ya Mashekhe kuwa hilo linajuzu?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, Maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:

Swali linaonesha kwamba hawa wanaofanya Umra wameingia kwa visa ya Umra, na sheria za nchi hiyo zinalazimisha kuondoka baada ya kumaliza Ibada ya Umra, na hawaruhusiwi kuendelea kubaki mpaka wakati wa Hija, na kwamba kuendelea kuishi humo katika hali hiyo ni kuvunja sheria za nchi. Ikiwa hivyo, basi hukumu ya jambo hili ni hakujuzu kufanya hivyo, kutokana na yafuatayo:

Kwanza: Katika kufanya hivyo kuna kuvunja amri ya kiongozi, na kuvunja amri ya kiongozi kwa kuwa haikuwa katika Haramu hakujuzu; kwa sababu Mwenyezi Mungu Amewajibisha kumtii kiongozi; Mwenyezi Mungu Anasema: {Enyi mlioamini! Mtiini Mwenyezi Mungu, na mtiini Mtume na wenye madaraka katika nyinyi}[An-Nisaai: 59]. Na imekuja kutoka kwa wapokezi sita wakubwa, kutoka kwa Ibnu Umar Allah Amuie radhi yeye na baba yake, kutoka kwa Mtume S.A.W. amesema: “Kusikiliza na utiifu kwa mtu Muislamu katika analolipenda na analolichukia, muda wa kuwa hajaamrishwa maasi, akiamrishwa maasi, hakuna kusikia wala kutii”. Na dalili ya hili ni nyingi, na kumtii kiongozi ndiyo sababu ya umoja na maisha kwenda sawa, hivyo hapana budi kwa watu kuwa na marejeo wanayofuata amri zake ili kuondosha mzozo na mgawanyiko, kinyume na hiyvo kutaenea fujo na uharibifu mkubwa utawapata watu katika Dini yao na dunia yao, na Ijmaa ya Wanazuoni wamekubaliana hilo.

Na kiongozi ana haki ya kuweka sheria anazoziona zinaweza kufikia masilahi ya waja; kwa sababu anayoyafanya kiongozi kwa raia yanategemezwa na masilahi, na wajibu wa raia kumtii kiongozi na kumtetea. Na mwenye kuingia katika nchi ya Saudia Arabia, basi anapaswa kufuata sheria zake, na ni haramu kwake kuvunja sheria, kiongozi ameamrisha watu kuondoka baada ya Ibada ya Umra, basi ni wajibu kumtii haraka, na hakujuzu kukaa mpaka wakati wa Hija, na hili linasisitizwa pia ikiwa tutasema Hija ni wajibu kwa nafasi (uwezo)kwa rai ya Madhehebu ya Imamu Shafii.

Pili: Matokeo ya jambo hilo ni madhara ambayo yanawakuta wengine, na kilichofikiwa katika kanuni za kisharia ni kwamba madhara huondoshwa; na Imamu Ahamd amepokea kutoka kwa Ibn Majah kutoka kwa Abbas na Ubada bin Samit Allah Awawie radhi, na Malik bin Yahya Al-Mazny R.A. kwamba Mtume S.A.W. amesema: “Usidhuru wala usijidhuru”. Na lengo ya sharia zinazofungamana na kudhibiti idadi ya Mahujaji sawasawa ndani ya Makka au kutoka nje limewekwa kwa masilahi tu ya Waislamu, na kuwarahisishia kutekeleza Ibada hiyo tukufu, na kupunguza madhara yatakayotokana na idadi ya Mahujaji kuwa kubwa kuzidi na ile iliyowekwa na mamlaka, madhara ambayo yanaweza kufikia vifo. Na hapa kuna mgongano wa masilahi mawili, moja ni masilahi ya mtu ambalo ni Hija ya mtu aliyevunja sharia baada ya Umra, na lingine ni masilahi ya Waislamu wote haya patikani isipokuwa kwa kudhibiti idadi yao, na ikiwa yamegongana, yanatangulizwa masilahi ya wengi kabla ya masilahi ya mtu mmoja.

Na Masilahi ambayo hupotea kwa ibada tukufu kama hizi; kutanguliza ibada ya Hija kwa mtu aliyevunja sharia baada ya Umra, pia Wanazuoni wamechunga katika masilahi yale yaliyokuwa chini kuliko hayo, wakaeleza kwamba kutanguliza kulinda mali za Mahujaji kabla ya Hija, kukiwa na gharama kubwa za safari, kama alivyosema Al-Qarafy katika Al-Furouqat.

Tatu: Yanayompata mvunja sheria katika kudhalilika anapogundulika, ikiwemo kufukuzwa, na watu huwatazama wanaofukuzwa dunia nzima kuwa si watu wazuri, na Muislamu hatakiwi kujidhalilisha; Mtume S.A.W. amesema katika Hadithi iliyotolewa na At-Tirmidhy na Ibn Majah na Ahmad katika Hadithi za Hudhayfa R.A.: “Haitakikani kwa muumini kujidhalilisha”. Na ikiwa Muislamu halazimiki kukubali kupewa thamani ya maji anayoyahitaji kwa ajili ya Udhu wake, na Wanazuoni wa Fiqhi wametoa sababu ya hilo kuwa ni yale maneno ya kusimanga, na Sharia tukufu imechunga jambo hili – hivyo  basi kutopasa Hija kwa Muislamu kwa njia hii ya Haramu ni bora, pia jambo linakuwa kubwa katika hali hii; kwani jambo hili madhara yake hayaishii kwa mvunja sharia peke yake, bali huvuka na kuabisha watu wa nchi yake pia, na huenda hilo litapelekea kuwekwa sharia maalumu kwa nchi yake ikiwa vitendo hivyo vinajirudia kufanywa na raia wa nchi hiyo.

Nne: Wajibu hauwachwi isipokuwa kwa wajibu, kama ilivvyo katika kanuni za Fiqhi, hapa kiongozi ameamrisha kuondoka baada ya Ibada ya Umra, na kumtii ni wajibu, na Hija ambayo amevunja sheria kwa ajili yake si wajibu katika Hali hii; kwa kukosekana uwezo wa kuitekeleza isipokuwa kwa kuvunja sheria.

Tano: Yale yanayotokea kwa baadhi ya wavunja sheria katika mambo ambayo huwachafua na kuzichafua nchi zao, kama kuomba omba, na kulala barabarani, jambo ambalo linasababisha madhara makubwa kila msimu wa Hija ikiwemo kukanyagwa na mahujaji na kudondokeana, na wapo miongoni mwao dhaifu au wagonjwa au wazee, na hatari inakuwa kubwa ikiwa na mizigo mizito waliyonayo, pamoja na msongamano, jambo hili linapelekea kuzuka majeraha makubwa ambayo yanaweza kusababisha vifo.

Ikiwa wakisema: kwamba baadhi ya watu wametoa Fatwa ya kujuzu kuvunja sheria ya ukazi baada ya Umra  ili kutekeleza Ibada ya Hija, jibu ni: Hao walitoa Fatwa hiyo, ima wawe wale ambao wanajuzu kutoa Fatwa kwa watu au laa, ikiwa haijuzu kwao kutoa Fatwa, basi jambo liko wazi; wao hawapo katika Daraja la kuzingatiwa, na wakiwa katika wale ambao kauli zao zinazingatiwa, basi haijuzu kufuata Fatwa yao; kwa sababu tukikadiria masuala haya kuwa ni kuhitilafiana, basi hukumu ya kiongozi katika masuala ya hitilafu inalinyanyua, na hapa kiongozi amezuia hilo.

Naye Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi

Share this:

Related Fatwas