Atakapofariki Mchumba Zawadi za Uchumba Zinakuwa za nani?
Question
Muulizaji anasema: Binti yake amechumbiwa na kijana mmoja miaka miwili iliyopita, na amempa zawadi za uchumba na baadhi ya zawadi, na amefanya sherehe ya uchumba na ametoa gharama zote, na kijana huyu amefariki, naomba kujua hukumu ya kisharia katika zawadi za uchumba?
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, Maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Uchumba, kukubaliwa mahari na zawadi za uchumba ni katika vitangulizi vya ndoa, na ni katika aina za ahadi muda wa kuwa ndoa haijafungwa kwa nguzo zake na sharti zake za kisharia, na kilichopitishwa kisharia ni kwamba mahari inakuwa katika dhima ya mume baada ya kufunga ndoa, ikiwa ndoa haijafungwa basi mchumba hana haki ya kitu chochote, na mchumba au warithi wake wana haki ya kuomba kurudishiwa mahari yao, ama zawadi za uchumba, hizi ni zawadi zinazochukua hukumu ya kitu kinachotolewa bure katika Fiqhi ya Madhehebu ya Hanafi, na yaliyoelezwa katika Madhehebu haya ni kwamba , kunakatazwa kurudisha kitu kilichotolewa bure kwa kifo cha alietoa kitu hicho au aliepewa, hivyo hakujuzu kwa warithi wa mchumba kuomba kurudishiwa zawadi za uchumba, sawasawa kilikuwa kitu au pesa; kwa sababu kufa kwa mchumba alietoa zawadi vitu vyote vimekuwa haki ya aliyechumbiwa kisharia.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi
Arabic
Englsh
French
Deutsch
Urdu
Pashto
Hausa
