Kufunga Ndoa kwa Njia ya Simu

Egypt's Dar Al-Ifta

Kufunga Ndoa kwa Njia ya Simu

Question

Nini maoni yako kuhusu ile inayoitwa “Kufunga ndoa kwa njia ya simu” ambayo imeenea kwa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu siku hizi?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:

Hakuna kitu kinachoitwa kufunga ndoa kwa njia ya simu katika sharia ya Kiislamu. Ndoa ya halali ni ile ambayo ina nguzo na masharti yake yote, ikiwa ni pamoja na mlezi halali wa mwanamke, uhiari na kukubali kati ya mwanamume na mwanamke, ushahidi wa mashahidi, mahari, na utangazaji. Ikiwa nguzo na masharti haya yatafikiwa katika mkataba wa ndoa, basi ni halali; vinginevyo, ni batili kwa mujibu wa wengi wa Wanachuoni wa Fiqhi.

Katika suala la swali na kwa kuzingatia yaliyotanguliwa hapo juu: kinachojulikana kama ndoa kwa njia ya simu sio halali kwa mujibu wa sharia ya Kiislamu kwa sababu nguzo na masharti ya mkataba wa ndoa haipatikani. Vijana katika Chuo Kikuu wanapaswa kuepuka zoea hili kwa sababu ni ukiukaji wa utakatifu wa Mwenyezi Mungu na ufisadi katika jamii. Jambo kama hilo likitokea, inachukuliwa kuwa uzinzi.

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi

Share this:

Related Fatwas