Kumkalifisha Mke Kufanya Kazi za Ny...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kumkalifisha Mke Kufanya Kazi za Nyumbani

Question

Ningependa kujua kama sharia ya Kiislamu inawalazimisha wanawake kufanya kazi za nyumbani. Ahsante.

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:

Ukweli kwamba mke hakalifishwi kwa kazi za nyumbani pia inalingana na ukweli kwamba mume hatakiwi kumlipa mkunga katika Madhehebu ya Imamu Shafi, tofauti na Madhehebu ya Imamu Malik. Haya ni iwapo kutatokea mzozo baina ya mume na mke, na hukumu ni kwa masharti yake mbele ya hakimu. Hata hivyo, katika elimu ya maisha na maadili mema ambayo Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W) alitufundisha, ambayo yameenea miongoni mwa watu, mume hugharamia matibabu ya mke wake na hulipa ada ya mkunga, na wala mkewe hataki malipo kutoka kwake kwa ajili ya kunyonyesha na kutunza nyumba – hata kama si wajibu kwake- Wala asiombe ada kwa hayo. Ni mila nzuri ambayo wanawake wa Kiislamu wameifuata, Mashariki na Magharibi, zamani na sasa. Kuchukua kile kilicho katika hukumu kwenye uhalisia wa maisha sio sawa. Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema: {Yeye humpa hikima amtakaye; na aliye pewa hikima bila ya shaka amepewa kheri nyingi}. [Al-Baqarah: 269]

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi

Share this:

Related Fatwas