Hukumu ya Vipodozi (Make up) na kut...

Egypt's Dar Al-Ifta

Hukumu ya Vipodozi (Make up) na kutengeneza Nyusi

Question

Je, kutengeneza nyusi ni halali au haramu? Na Vipodozi ni halali au haramu?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, Maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:

Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W.) amesema: "Mwenyezi Mungu amewalaani wanawake wanaochora tatuu na wanaojichora, wanaonyoa nyusi na wanaojinyoa nyusi, na wanaotengeneza mwanya kwa ajili ya uzuri, wale wanaobadilisha maumbile ya Mwenyezi Mungu"

An-naamisah ni mwanamke anayeondoa nyusi kwa kuzinyoa au kuzipunguza kwa ajili ya urembo.

Imepokelewa na At-Tabari kupitia Abu Ishaq kutoka kwa mkewe, kwamba mkewe aliingia kwa Aisha (R.A.) naye alikuwa mwanamke kijana anaependa urembo, akamwuliza: "Je, mwanamke anaweza kutengeneza sehemu ya juu ya uso wake (nyusi) kwa ajili ya mumewe?" Aisha akajibu: "Ondoa uchafu kadri uwezavyo."

Kwa msingi huo: kupunguza nyusi au kuziondoa kabisa, au kuzichora kwa kutumia kalamu au rangi ni haramu kisharia. Hata hivyo, inajuzu kutengeneza nyusi kwa kiasi katika hali ya mwanamke kujipamba kwa ajili ya mumewe, au iwapo kuna nywele nyingi kupita kiasi ambazo humsumbua mwanamke; katika hali hizo, hakuna ubaya kuondoa nywele za ziada.

Kuhusu vipodozi vya urembo au mapambo (Make-Up): Ikiwa vipodozi vinatumiwa kwa kiasi na kwa namna kama vile wanja kwenye macho au hina mikononi, basi hakuna tatizo, lakini iwapo vipodozi vinatumiwa kwa ajili ya kuonyesha uzuri wa fitna, kuchochea matamanio na kuvutia (wanaume), basi jambo hilo ni haramu.

Kwa yaliyotajwa hapo juu, jibu la swali limebainika iwapo hali ni kama ilivyoelezwa.

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi

Share this:

Related Fatwas