Baba kumlazimisha binti yake kuvaa Hijabu.
Question
Je, baba ana haki ya kumlazimisha binti yake kuvaa Hijabu, kumzuia asitoke nje ya nyumba, kumlazimisha kuacha kazi yake kwa sababu ya kutovaa Hijabu, na yote haya kuyafanya sharti ya kuvaa Hijabu? Pamoja na hayo, anafanya hili ndio sharti katika maisha yake ya kila siku?
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, Maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Baba ana wajibu wa kuendelea kumshauri binti yake katika kumtii Mola wake Mtukufu. Hijabu ni faradhi ya lazima kwa mwanamke wa Kiislamu aliyebaleghe, nayo ni kuvaa nguo zinazositiri mwili wake wote isipokuwa uso na viganja vya mikono yake, bila kujali nguo. lakini, hii haiathiri kumgharamikia binti yake kifedha akiwa yuko chini ya usamimizi wake. Maasi hayazuii matumizi. pia kutovaa kwake Hijabu sio sababu kwake ya kumzuia kuishi maisha ya kawaida, isipokuwa kama akijua kuwa kupotoka kwake. Katika hali hiyo, lazima atumie mamlaka yake kumzuia kutopotoka kadiri awezavyo.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi.
Arabic
Englsh
French
Deutsch
Urdu
Pashto
Hausa
