Kazi ya Mwanamke katika Saluni
Question
Mfanyakazi wa serikali mwenye kipato kidogo anasaidia familia ya watu saba. Mapato yake hayatoshi kukidhi mahitaji ya kimsingi ya maisha, kwa hivyo mke wake anafanya kazi ya kutengeneza nywele saluni, na kuwapamba wanawake nyumbani. Anauliza hukumu ya Kiislamu juu ya hili.
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, Maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Kazi ya mwanamke ya urembo na pambo kwa wanawake wengine haikatazwi na wala haina pingamizi. Uislamu umewatendea haki wanawake, umewaheshimu, na kuwafanya kuwa msingi wa jamii ya haki. Mwanamke ana haki ya kufurahia uzuri na mapambo yake. Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema: {Sema: Ni nani aliye harimisha pambo la Mwenyezi Mungu alilo watolea waja wake, na vilivyo vizuri katika riziki} [Al-Aaraf: 32] Mapambo yenyewe hayakatazwi na sheria ya Kiislamu. Uislamu ni dini ya usafi na uzuri. Uislamu ulifanya usafi kuwa msingi wa imani na ukahimiza kuwa kipengele kizuri cha imani na sifa bainifu ya Muislamu. Mtume (S.A.W) amesema: “Hakika Mwenyezi Mungu ni mwema na anapenda wema. Yeye ni msafi na anapenda usafi. Yeye ni mkarimu na anapenda ukarimu. Yeye ni mpole na anapenda fadhila. Basi safisheni baraza zenu wala msifanane na Mayahudi.”. Imepokelewa kutoka kwa Al-Tirmidhiy. Kwa hiyo, hakuna ubaya kwa mwanamke kutia urembo wanawake wenzake, lakini kwa sharti kwamba urembo huo uwe wa wastani na kwa madhumuni ya halali, na mbali na ubadhirifu na utiaji kupita kiasi, jambo ambalo linapingana na maadili ya sheria ya Kiislamu na linachukiwa na dini yetu ya kweli. Kwa mtazamo huu, tunawausia wanawake wa Kiislamu wajipambe kwa kiasi katika mapambo yao na wasizidishe, wasije wakajumuishwa miongoni mwa waliolaaniwa na kufukuzwa na rehema ya Mwenyezi Mungu. Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W) amewataja wanawake hao pale aliposema: “Mwenyezi Mungu amewalaani waunganishaji nywele kwa nywele na waunganishwaji nywele kwa nywele, Wenye kuchora watu tatu) na wachorwaji tatuu, Wenye kunyoa nyusi na kinyozi wa nyusi, na wenye kuchonga mianya (mwanya) ya meno yao mdomoni; ambao wanageuze maumbile ya Mwenyezi Mungu.”
.” Imepokelewa na Al-Bukhari na Muslim kutoka kwa Ibn Mas`ud.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi.
Arabic
Englsh
French
Deutsch
Urdu
Pashto
Hausa
