Uvutaji wa sigara

Egypt's Dar Al-Ifta

Uvutaji wa sigara

Question

Ni ipi hukumu ya kisharia kuhusu uvutaji wa sigara?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, Maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:

Uislamu umeharamisha kwa mwanadamu kila kitu chenye kudhuru mwili wake — kimwili au kiroho. Na Mola wetu Mtukufu amesema:{Na anawahalalishia vilivyo vizuri na anawaharimishia vile vibaya (viovu)} [Al-A'raf: 157]

Hivyo, kilicho kizuri ni kila kitu chenye manufaa kwa mwanadamu kimwili au kiroho, na kilichi kibaya ni kila chenye kumdhuru mwanadamu kimwili au kiroho.

Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {wala msijitie kwa mikono yenu katika maangamizo} [Al-Baqarah: 195].

Na imepokelewa na Ahmad, Ibn Majah na at-Tabarani kutoka kwa Ibn Abbas (Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao) kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehema na Amani ziwe juu yake) amesema: "Hakuna kudhuru wala kudhuriana."

Na pia amepokea Ibn Majah na al-Bayhaqi kutoka kwa ‘Ubadah bin Samit (Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake), na pia amepokea at-Tabarani na Abu Nu’aym kutoka kwa Thalabah bin Abi Malik al-Quradhi (Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake).

Na imethibitika kisayansi kuwa uvutaji sigara kwa aina zake zote — iwe sigara, shisha au vinginevyo — inadhuru afya na mwili wa mwanadamu. Na jambo hili limeamuliwa na Shirika la Afya Duniani, pamoja na Taasisi ya Kiislamu ya Sayansi za Tiba. Na pia imethibitika kuwa husababisha madhara moja kwa moja kwa mwenye kuvuta, na kwa njia isiyo ya moja kwa moja (uvutaji usio wa moja kwa moja) na uchafuzi wa mazingira.

Kwa hiyo, huwa haramu. Na mwenye kusaidia katika haramu nayo ni haramu, kwani njia hukumu yake hufuata makusudio. Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na saidianeni katika wema na uchamungu, wala msisaidiane katika dhambi na uadui} [Al-Ma’idah: 2]

 

Kwa hivyo, uvutaji sigara kwa aina zake zote ni haramu.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi.
Share this:

Related Fatwas