Kuwanakilia vitabu wanafunzi ili kufanya udanganyifu katika mtihani
Question
Ninamiliki duka la vifaa ya ofisi na mashine ya kutolea nakala karibu na Chuo Kikuu, wanafuzni wanakuja dukani kwangu na maduka kama yangu ili kudogesha karatazi na kuwapesishia kufanya udanganyifu katika mtihani, na sisi tunajua hilo, lakini hatuwahamishi kugelezea wala hatuwamrishi kufanya hivyo, na wao wanasema: Hali ya Chuo inaruhusu, na jambo hilo limezoeleka katika vyumba vya mItihani wala halikemewi. Je, inafaa kwetu kuwatolea nakala na kudogesha karatasi kwa lengo hili?
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, Maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Mwenyezi Mungu Anasema: {Na saidianeni katika wema na uchamngu. Wala msisaidiane katika dhambi na uadui. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu}. [Al-Maida:2] Na Mtume S.A.W. anasema: “Mwenye kufanya udanganyifu si katika sisi” Imepokelewa na Muslim na wengineo kutoka kwa Abu Hurayra R.A.
Hivyo basi kutokana na uhalisia wa swali, hakika kudogesha vitabu na kurasa na vinavyofanana na hivyo kwa hawa wanafunzi ni haramu kisharia, na jambo baya kitabia na halikubaliki kimaumbile, na kunatosha kuwa ni kumsaidia mwanafunzi kufanya udanyanyifu kwa kufanya hivyo, na hakuna mfumo wa Chuo Kikuu unaoruhusu kufanya udanganyifu, jambo hili ni batili kisharia, na hata tukisema kuwa linafaa; kuruhusu mtu au mamlaka jambo la haramu hakulifanyi kuwa halali; kwani anayeharamisha na kuhalalisha ni Mwenyezi Mungu, si mtu mmoja mmoja au mamlaka hata kama iwe kubwa kiasi gani.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi
Arabic
Englsh
French
Deutsch
Urdu
Pashto
Hausa
