Watoto wa kike kula chakula pamoja na watoto wa kiume
Question
Naombeni Fatwa kuhusu Binti yangu mwenye umri wa miaka kumi na moja bado hajavunja ungo, kutokana na matukio yaliyomtokea shuleni kwao, wanafunzi wavulana na wasichana wa darasani kwake wenye rika moja walikusanyika na kula chakula pamoja takriban wanafunzi ishirini wa kike na wakiume, na yeye alikaa karibu na mwanafunzi mwenzake wa kiume, wenzake wakamtuhumu kuwa amefanya jambo la haramu, kwa kuruhusu kwake kukaa karibu na mtoto wa kiume, kukiwa kuna nafasi kati yao nusu mita takriban, kwa mujibu wa maneno yake katika ya mkusanyiko huu mkubwa wakila chakula.
Tuhuma hizi zimemuathiri kiasi kikubwa binti yangu, wakati yeye mwenyewe anajichunga na haramu tangu mdogo hata bila ya kuambiwa ili kujizoeza, na kwa kweli anajitahidi kujichunga katika mambo yake yote, na anajifaharisha na hilo na anajinasibisha na Mtume S.A.W.; hivyo nimeona niombe Fatwa kwenu katika jambo hili ili nafsi yake na rafiki yake zitulie haraka iwezekanavyo Inshaa Allah. Na natanguliza shukrani.
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, Maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Makubalino ya Waislamu wa zamani na wasasa ni kwamba uwepo tu wa wanaume na wanawake sehemu moja si haramu, uharamu unakuwa katika aina ya uwepo huo katika mkusanyiko ikiwa unapingana na Sharia Tukufu; kama kukusanyika katika jambo la haramu, au faragha iliyoharamishwa. Na Wanachuoni wameeleza kwamba kuchanganyika kuliko haramu ni kugusana na kushikana, si mkusanyiko tu wa wanawake na wanaume sehemu moja.
Hili limeelezwa na Hadithi tukufu, imekuja katika sahihi mbili kutoka kwa Sahali bin Saada R.A amesema: “Abu As’ad Al Saaidy alipofanya harusi, alimualika Mtume S.A.W. na Masahaba zake, alipowapikia chakula alikipeleka mke wake Mama Asyad”. Boukhary ameifasiri kwa kauli yake: “Mlango wa mwanamke kusimama mbele ya wanaume katika harusi na kuwahudmia”. Al-Qurtuby amesema katika kutafsiri: “Wanazuoni wetu wamesema: katika Hadithi hii kunajuzu bibi Harusi kumuhudumia mume wake na marafiki zake katika harusi yake”.
Ibn Battal amesmea katika sherehe yake Bukhari: “Katika Hadithi tunapata kwamba kutenganisha wanawake na wanaume katika sehemu au katika muamala wa moja kwa moja si faradhi kwa wanawake wa Waumini, bali ni maalumu tu kwa wake wa Mtume S.A.W., pia hili amelitaja Mwenyezi Mungu katika Qurani Tukufu kwa kauli yake: {Na mnapo wauliza wakeze haja waulizeni nyuma ya mapazia} [Al Ahzab:53]”.
Hafidh Bin Hajar amesema katika Fat’hi Al bary: “katika Hadithi hii kunajuzu mwanamke kumuhudumia mume wake na aliowaalika, na hakufichiki kwamba sehemu ya hili ni pale kunapokuwa na uhakika wa kutokuwepo fitina na kuchunga yanayopasa kustiri, na kujuzu mwanamume kumtumia mke wake katika jambo kama hilo”.
Na katika sahihi mbili kutoka kwa Abu Juhayfa R.A. amesema: “Mtume S.A.W. aliwaunga undugu Salman na Abu Dardaa, Salman akamtembelea Abu Dardaa, akamuona Mama Dardaa amevaa nguo chakavu, akamuuliza: una nini? Akasema: ndugu yako Abu Dardaa hana haja na dunia. Akaja Abu Dardaa akampikia chakula…” mpaka mwisho wa Hadithi.
Al Hafidh bin Hajar amesema katika Fat’h Al Bary: katika Hadithi kuna faida… kujuzu kuzungumza na mwanamke wa kando na kumuuliza yenye masilahi”.
Hivyo basi hakuna ubaya mwanamume kukaa na mwanamke sehemu moja kukiwa hakuna shaka na kukawa hakuna faragha, nayo: mwanamke na mwanamume kujitenga na mwanamke mmoja katika sehemu kwa namna hawezi mtu kuingia sehemu yao, Imamu ibn Daqiq Al-Eid amesema katika Ahkam Al- Ihkam katika sherehe ya Umda Al Ahkam : akisherehesha kauli ya Mtume S.A.W.: “Jihadharini na kuingia kwa wanawake” hii ni maalumu kwa wasiokuwa mahrimu, na inakusanya wasiokuwa mahrimu, na Hapana budi kuzingatia jambo lingine nalo ni kuwa kuingia kunakuwa katika faragha, ama kukiwa si faragha basi hakukatazwi”.
Pia si kila kujitenga na kukaa faragha ni haramu; imepokewa Hadithi kutoka kwa Bukhari na Muslim na wengineo, kutoka kwa Anas bin Malik R.A. amesema: “Alikuja mwanamke wa Madina kwa Mtume S.A.W. akakaa naye faragha, akasema: naapa kwa Mwenyezi Mungu hakika nyinyi ni watu ninaowapendeza zaidi…” katika baadhi ya riwaya: “akakaa naye faragha katika baadhi ya njia, au katika baadhi ya Barabara”, Imamu Bukhari akaitengeneza mlango kauli hii kwa kuiita: “Mlango wa yanayojuzu mwanamume kukaa faragha na mwanamke mbele za watu”.
Al Hafidhi bin Hajar amesema katika Fath’hul Bary: “Katika Hadithi hii kuna dalili kwamba kuzungmza na mwanamke mtu kando kwa siri hakukatazwi katika Dini kukiwa na hakuna fitina”.
Mula Ally Al Qary amesema katika Mirqaty Al Mafatih: “katika Hadithi hii kuna kutanabahisha kuwa kukaa faragha na mwanamke katika vichochoro si katika sehemu ya kukaa naye faragha katika nyumba”.
Na kidhibiti cha faragha iliyoharamishwa kama alivyosema shekhe Al Shabramalsy Ashafy katika sherehe yake katika Nihayat Al Muhtaj: “Kukutana ambako kunakuwa na shaka ndani yake kikawaida, kinyume lau kama kutaondoka kikawaida, hakuhesabiwi kuwa ni faragha”.
Ama kuhusu kula chakula pamoja wanaume na wanawake, Imekuja kutoka katika sahihi mbili kutoka kwa Abu Hurayra R.A katika kisa cha Talha Al Ansary katika kulisha kwake wageni: “Walijifanya waonekane kama wanakula, ilhali walilala na njaa’ katika riwaya nyingine ya Ibn Abi Dunia katika Qira Al Dayf katika Hadithi ya Anas R.A: “Kwamba mtu mmoja alimwambia mke wake: Ujaze nyama mkate huu kisha utie samli kisha ulete, na mwambie mtumishi azime taa, na wakawa wanatafuna tafuna yeye na mke wake ili mgeni aone kuwa wanakula”. Na hali ilivyo ni kwamba wao wamekusanyika sehemu katika Sahani moja.
Kwa hiyo Imamu An-Nawawy anasema katika kufafanua Hadithi hii: “Hadithi hii imekusanya faida nyingi … miongoni mwazo kudanganya katika kumkirimu mgeni akiwa anakataa kwa kuwahurumia wakazi wa nyumba hiyo; kwa kauli yake: “zima taa na muoneshe kama tunakula” kwani lau kama angeona uchache wa chakula, na kwamba wao hawali naye angekataa kula”.
Mtume S.A.W. amesma: “Mwenyezi Mungu amependezwa na mlichokifanya kwa mgeni wenu usiku”. Na ikashuka katika tukio hili Aya hii: {bali wanawapendelea kuliko nafsi zao, ingawa wao wenyewe ni wahitaji} [Al-Hashri:9]
Na imetolewa Hadithi na Bukhari katika Al Adab Mufrad, na Annasaaiy katika Al Sunan Kubraa, na Ibn Hatim katika At-Taisir, na wengineo kutoka kwa Aisha R.A. amesema: “Nilikuwa ninakula chakula na Mtume S.A.W. katika chombo, akapita Omar, akamwita, akala, kidole chake kikagusa kidole changu, Omar kasema: Lo! lau ningesikilizwa msingeonekana na mtu” ikashuka Aya ya Hijabu. Al Hafidh Al- Suyut ameifanya kuwa sahihi katika Al Dar Al Manthour.
Qadhy al Ayadh anasema: “Faradhi ya hijabu ni katika mambo ambayo ni maalumu tu kwa wake wa Mtume S.A.W.; hii ni faradhi kwao isipokuwa uso na viganja”. Kauli kama hii imetangulia kutoka kwa Ibn Batuta Allah amrehemu, na hili linafanya kujuzu hilo kwa wasiokuwa wao, na si makusudio ya hijabu iliyofaradhishwa kwa wake wa Mtume S.A.W. kutodhihirisha utu wao kabisa hata kama wamejistiri, bali wameruhusiwa kutoka kukidhi mahitaji yao, ili kuondoa uzito na taabu, kama alivyobainisha hilo Al Hafidh bin Hajar katika fathul Bary akitolea dalili yaliyopo katika Bukhari katika mlango wa (Tawaf ya wanawake pamoja na wanaume) kutoka kwa Ibn Jurayj amesema: “Ataa amenieleza Ibn Hisham alipowazuia wanawake kutufu pamoja na wanaume, akasema vipi awazuie hali ya kuwa wake wa Mtume wametufu pamoja na wanaume? Nikasema: Baada ya Hijabu au kabla? Akasema: Naapa nimeidiriki baada ya hijabu, nikasema: vipi wanawake wachanganyike na wanaume! akasema: hawakuwa wakichanganyika; Bi. Aisha R.A. alikuwa akitufu na kundi la wanaume linatufu na hawachanganyiki nao”.
Ushahidi wa hilo Hadithi iliyopokelewa na Imamu Abu Dawoud katika Sunna zake “Kwamba Bi. Aisha rehema za Mwenyezi Mungu zimfikie alipita mwombaji akampa kipande cha mkate, na akapita mtu mwenye haiba, akamkaribisha akae na akala, akaulizwa kuhusu hilo, akasema: Mtume S.A.W. amesema Wawekeni watu sehemu zao”, Imamu Muslim ameitaja katika utangulizi wa sahihi yake, na Ibn Khuzayma na Hakim na wengineo wameifanya kuwa ni Hadithi sahihi, na Al Hafidh Al Sakhawy ameifanya kuwa Hadithi sahihi katika Al Maqasid na muktadha wake ni kwamba mtu mwenye haiba amekaa na amekula pamoja naye R.A., kama ilivyokuja katika ufafanuzi wake katika riwaya ya Al-Bayhaqiy katika mafungu ya Imani katika Al Adab: “akamwita, akakaa nae”.
Imamu Malik R.A. ameelezea kujuzu mwanamke kula na mwanamume mtu kando kwa sharti ya kutokaa naye faragha; imekuja katika Muwataa: “Amesema Yahyaa: Malik aliulizwa: je, mwanamke anaweza kula na mtu ambaye si mahrimu au pamoja na kijana wake? Akasema: hakuna ubaya katika hilo; ikiwa jambo hilo ni kawaida kwa mwanamke kula na wanaume, akasema na anaweza kula mwanamke na mumewe na watu wengineo ambao hula nao, au Pamoja na kaka yake kwa mfano wa hilo, na kunachukiza mwanamke kukaa faragha na mwanamume ambaye si mahram” ([1]).
Wake wa Mtume S.A.W. walikuwa wakifundisha elimu na Dini, na hizi ni diwani za sunna katika riwaya zilizopokelewa kutoka kwao, pia kutoka matabaka ya wanawake waliokuja baada yao ambao wanaume wamepokea kutoka kwao Hadithi na kuchukua elimu, Al Hafidh bin Hajar Al Asqalany amewataja katika kitabu chake cha Al Isabah fee tamayyuz al sahaba peke yake wanawake elfu moja miatano arubaini na tatu, miongoni mwao kuna wasomi wa Fiqhi, Hadithi na Fasihi.
Mwanamke wa Kiislamu alikuwa anashirikiana na wanaume katika Maisha ya jamii, pamoja na kudumu na vazi lake la kisharia na kulinda mipaka ya amani na adabu zake; mpaka kulikuwa na wanawake wa Masahaba walioshika wadhifa wa uhasibu, katika hili ni Hadithi iliyopokelewa na At-Tabarany katika Al-Muujam Al-Kabir kwa Sanadi ya watu wake waaminifu, kutoka kwa Abu Balh Yahaya bin Abii Sleem, amesema: “Nimemwona Samraa bin Naheek na alikuwa amemuwahi Mtume S.A.W. na masahaba zake, akiwa na ngao ngumu na mtandio mkubwa mkononi mwake anawapiga watu na kuamrisha mema na kukataza mabaya”.
Kwa haya, basi hakuna nafasi kwa yeyote kukemea hali hii thabiti katika Hadithi za Mtume tukufu na historia ya Uislamu, wala hakusihi kufanya mila na desturi zilizorithiwa hapo zamani au sehemu yoyote kuwa ndiyo msaidizi wa kuhukumu katika Dini na Sharia, bali Sharia inakuwa juu wala haiwi chini ya chochote, wala hakujuzu kwa mtu anayefuata njia ya kujichunga kuwalazimisha watu katika njia hiyo au kuwabebesha, au kufanya ugumu au kubana katika yale ambayo Mwenyezi Mungu Ameyafanya kuwa na wepesi ndani yake.
Kutokana na haya na swali lilivyo: Kula chakula wanawake na wanaume ni jambo linalojuzu kisharia muda wakuwa lipo katika hali ya adabu za kisharia zinazochungwa, na wanawake kujistiri na mavazi yao ya kisharia ikiwa tu hakuna kugusana kati ya wawili hawa, na wala kutoka nje ya kuamailina au maneno mabaya, kukipatikana hilo kati ya wanawake na wanaume wasiofikia baleghe basi hilo linajuzu, Pamoja na kuchunga kuwafundisha adabu za kisharia na kuwazoesha kujipamba na adabu za Kiislamu ili wazizoee watakapobaleghe.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi
([1]) Al Muwataa, mlango wa sifa za Mtume S.A.W. sura ya yaliyokuja katika chakula na vinywaji, 4/367.
Arabic
Englsh
French
Deutsch
Urdu
Pashto
Hausa
