Hukumu ya kuchanganyika wanafunzi k...

Egypt's Dar Al-Ifta

Hukumu ya kuchanganyika wanafunzi katika masomo

Question

Nimemuombea mwanangu masomo katika moja ya shule za kisasa, kisha nikagundua kuwa mwanangu anapenda sana kuhifadhi Qur`ani Tukufu, na nimemhamaisisha katika hilo, na amehifadhi Qur`ani Tukufu yote akiwa darasa la sita, Alhamdulillah, isipokuwa nimegundua kuwa shule yao kuanzia Sekondari mpaka Elimu ya juu, wanafunzi wa kike na wakiume wanasoma pamoja, pamoja na hatari ya umri huu kwa wavulana na wasichana, pia nimegundua  kwamba idara ya shule na wasimamizi wanasumbuliwa sana na jambo hili, na kwamba idara ya shule inafanya juhudi kubwa kwa wanafunzi wa kiume au wa kike kutatua matatizo yanayoibuka kati ya wanafunzi wa kike na wakiume katika awamu hii, hasa kwa kuchanganyika.

Juhudi hizi zinaathiri moja kwa moja juhudi ambazo zinaweza kutolewa katika masilahi ya elimu; ikiwa Hadithi tukufu zinatuamrisha kuwatengenisha kati ya kaka na dada wanapofikia Baleghe katika vyumba au vitanda, inakuwaje kwa Watoto wa shule katika hatua hii ngumu? Hasa kwamba kuna uwezekano wa kuwatengenisha; kwa kuwepo shule nyingine iliyo chini ya idara hiyo ambayo moja inaweza kufanywa shule ya wavulana na nyingine ya wasichana, na watu wa idara wanatamani kuwatengenisha.

Naombe mnipe Fatwa, Dini inasemaje kuhusu kuchanganyika huku, naomba mnipatie kwa haraka ikiwezekana ili niweze kulifikisha katika Idara, ili wachukue maamuzi sahihi ambayo yanaendana na msimamo wa Dini Tukufu ya Kiislamu.

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, Maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:

Kuchanganyika kati ya wanaume na wanawake katika shule na Vyuo Vikuu na sehemu nyiginezo hakukatazwi kisharia, muda wa kuwa katika mipaka ya adabu na mafundisho ya Kiislamu, na mwanamke akawa amejihifadhi katika mavazi yake, amevaa mavazi mapana hayaonyeshi kilicho ndani ya mwili wake wala kudhihirisha, akiwa anainamisha macho yake na anajiweka mbali na faragha kwa hali na sababu yoyote, Mwenyezi Mungu Anasema: {Waambie Waumini wanaume wainamishe macho yao, na wazilinde tupu zao. Hili ni takaso bora kwao. Hakika Mwenyezi Mungu Anazo khabari za wanayo yafanya} [Anour:30]

Na kama Alivyosema Mwenyezi Mungu: {Na waambie Waumini wanawake wainamishe macho yao, na wazilinde tupu zao, wala wasionyeshe uzuri wao isipo kuwa unaodhihirika} [Anour:31].

Ikiwa mwanamke na mwanaume hawakufuata yale aliyoyaamrisha Mwenyezi Mungu, basi kuchanganyika huku kunakuwa ni njia ya Haramu, na hapo kunapasa kuwatengenisha, ama kukiwezekana hilo kama ilivyokuja katika swali basi wajibu wa kuwatenganisha unaongezeka kukiwezekana kutekeleza hilo.

Naye Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi

Share this:

Related Fatwas