Nyimbo na Muziki.
Question
Ni nini hukumu ya Kisharia katika nyimbo, muziki, ala za muziki, na uimbaji wa wanawake na wanaume au peke yao? Na kigezo gani cha kutofautisha baina ya kile kinachoruhusiwa na kilichoharamishwa, kizuri na kibaya, na kuwekwa wazi kwa dalili na ushahidi kutoka katika Qur’ani Tukufu, Sunna, na Athar? Na athari ya hilo kwa watu na jamii kwa ujumla?
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, Maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Muziki: ni elimu inayoshughulika na hali ya toni na mdundo, jinsi ya kutunga nyimbo, na uundaji wa ala. Sauti inayotolewa na ala za muziki pia huitwa muziki.
Suala la kusikiliza muziki ni suala lenye tofauti za Kifiqhi, si kutokana na misingi ya Akida, na si katika mambo ya kidharura katika dini,na Waislamu hawapaswi kutuhumiana kwa ufasiki au kukemeana wao kwa wao kwa ajili ya masuala hayo yenye tofauti; kwani hali ilivyo Hukemewa lenye kukubaliana wala halikemewi lenye kutofautiana, na muda wa kuwa kuna miongoni mwa Wanachuoni wamehalalisha muziki - na hawa wanazingatiwa katika kauli yao na inajuzu kuwafuata – basi haijuzu kuugawanya Umma kwa sababu ya masuala yenye tofauti hiyo, na hasa kwa kuwa hakuna matini sahihi na za wazi katika Sheria zinazoharamisha muziki, kwa ajili hiyo kuna tofauti. Na hoja ya waliosema kwa kuharimisha muziki ni maana ya Dhahiri kutokana baadhi ya Aya za Qur`ani Tukufu ambazo wafasiri walizichukua kama ni uimbaji na muziki, kama kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na miongoni mwa watu wapo wanaonunua maneno ya upuuzi, ili wawapoteze watu na njia ya Mwenyezi Mungu pasipo kujua, na wanaichukulia ni maskhara} [LUQMAAN 6], na kauli yake: {Na ambao hujiepusha na mambo ya upuuzi} [AL MUMINUN 3], na kauli yake: {Na wachochee uwawezao katika wao kwa sauti yako}[AL ISRAA 64], na katika Sunna Hadithi ya Abu-Amir au Abu-Malik Al-Ashari R.A kutokana na Mtume S.A.W amesema: "Watakuwa kutokana na Umma wangu watu wanaohalalisha uzinifu, nguo za hariri, (kwa mwanaume) pombe na vyombo vya muziki" na Imamu Al-Bukhariy katika sahihi yake, na kadhalika kutokana na Hadithi zilizokuwa na maana hiyo.
Na wenye elimu wengi miongoni mwa Masahaba na waliowafuata walisema kwamba kupiga muziki na vyombo vyake si chochote ila ni sauti tu: nzuri yake ni nzuri na na mbaya yake ni mbaya, na Aya za Qur`ani Tukufu hazina katazo wazi juu ya muziki na vyombo vyake mashuhuri, na katazo katika Hadithi ya Imamu Bukhari ni kwa baadhi sio kwa zote kwa maana zote zilizokatazwa katika Hadithi zilijumuisha pamoja katika Sura moja, Uzinifu, na Hariri iliyoharamishwa juu kwa mwanaume; na makusudio ni kukataza maisha ya anasa si muziki hasa hasa, na misingi ya elimu ya Usuul ilikiri kwamba kuambatana si hoja; na kutajwa kwa muziki baada uzinifu si hoja kuharimisha muziki, na Hadithi zingine kutokana na hizo si sahihi au inahusisha miziki inayowasahaulisha juu ya Dhikri na ibada ya Mwenyezi Mungu au inasabibisha maovu na mambo ya haramu; na Hadithi sahihi kutokana na Hadithi hizo si kwa maana Dhahiri na iliyo na maana Dhahiri si sahihi. Na hii rai ya madhehebu ya watu wa Madinah, na iliyopokelewa na kundi la Masahaba kama Abdullah Ibn Az-Zubair na Hassan Ibn Thabit na Muawiya na Amr Ibn Al-Aas R.A na kutokana na waliofuata Al-Kadhi Shuraih na Said Ibn Al-Mosaiyab na Attaa Ibn Abi Rabah na Al-Zuhariy na Al-Shaabiy na Saad Ibn Ibrahim Ibn Abd Ar-Rahman Ibn Auf –Na alikuwa hazungumzi mazungumzo ila kwa kupiga udi– na wengineo; na Imamu wa Haram mbili (Makka na Madinah) alisema katika kitabu cha: [Al-Nihaya] "Ilipokelewa kwa uthabiti kutoka kwa wanahistoria kwamba Abdullah Ibn Az-Zubair R.A alikuwa na wajakazi waliopiga udi (aina ya gitaa) na Ibn Omar R.A aliingia na pembeni mwake kuna gitaa, na akasema: Kitu gani hicho Ewe, sahiba wa Mtume S.A.W? kisha akaichukua, na Ibn Omar aliiangali na kusema: Hii ni mizani ya Shamu, Ibn Az-Zubai alijibu: Akili hupimwa nayo" mwisho.
Na wanaokubaliana na Madhehebu hii ni Ibn Hazm na watu wa Dhahiri na baadhi ya wafuasi wa Shafi na miongoni mwao Ustadh Abu Eshak Ash-Shirazi na Al-Mawardimna Al- na Ruyani na Abu Mansur Al-Baghdadi na Al-Rafiy na Hoja ya Uislamu Al-Ghazali na Abu Al-Fadl Ibn Tahir Al-Kisarani na Imamu Ezul-Din Ibn Absul-Salam na Shekhe wa Uislamu Takiy Al- Din Ibn Dakik Al-Eid na Abd Al-Ghani Al-Nabulsi Al-Hanafi… na wengineo.
Na waliosema wazi juu ya uhalali wa muziki na vyombo vyake kundi la maulamaa kama: Ibn Hazm Al-Dhahiri katika risala yake ya “Al-ssamaiy”, na Ibn Al-Kisarani katika kitabu chake " Al-Samaiy" "", na Al-Edfiwiy katika "Al-Imtaii Bi Ahkam Al-Samaiy", na Abu Al-Mawahib Al-Shazliy Al-Malikiy katika "Farah Al-Asmaiy Bi Rukhs Al-Samaiy", na wengineo wengi.
Na miongoni walieleza wazi juu ya uhalali wa vyombo vya muziki Hoja ya Uislamu Al-Ghazaly –R.A- aliposema katika kitabu chake Ihyaa Uloum Al Deen: " Pumbao linasaidia juu ya kufanya bidii, na kufanya bidii hakuwezekani kusubiriwa juu yake ila kwa nafsi za Mitume A.S, na pumbao ni dawa ya moyo kutokana na taabu na uchovu, basi kunatakikana kuwa ni halali, lakini sio kwa kukithirisha, kama ilivyokuwa haifai kukithirisha dawa, basi pumbao kwa nia hii inakuwa heri, haya ni kwa wale ambao hawakutikiswa na Samaiy (Muziki( kutoka katika nyoyo zao lakini hawezi kuhisi na pumbao ila kwa ladha na raha tupu tu, na kunatakikana kufanya hivyo ili kupata makusudio yaliyotajwa, ndiyo hii ni dalili ya upungufu juu ya sifa ya ukamilifu; na ukamilifu ni sifa ya aliyekuwa hahitaji pumbao au raha pasi na haki, kwani mazuri ya watu wema ni mabaya ya wanaojikurubisha kwa Mwenyezi Mungu/wachamungu. Na mjuzi zaidi wa elimu ya utabibu wa nyoyo na jinsi ya kuiliwaza, ili kuiendesha kwenye haki na wema alijua moja kwa moja kwamba pumbao lake kwa mambo kama hayo ni dawa iliyo bora" [Ihiau Ulum Al-Din, Imam Al-Ghazaly, 2/226, chapa ya Al-Matbaa Al-Azharia].
Pia Sultani wa maulama Al-Ezz Ibn Abd As-Salam alisema kwamba Muziki na vyombo vya muziki na visivyokuwa hivyo vinaweza kuwa sababu ya kuboresha nyoyo, akasema: "Njia ya kurekebisha nyoyo inakuwa kwa sababu za kutoka nje; kama kusikiliza Qur`ani Tukufu na hiyo ni bora zaidi kwa wasikilizaji waadhi na ukumbusho, na inakuwa kwa wimbo kwa maana kusikilizia mashairi ya kidini, au kwa uimbaji kwa kutumia vyombo vya muziki na katika kuusikiliza aliyehalalisha kusikia vyombo hivyo anapaswa kusikia mema na kuacha maasi kwa kusikiliza waliotofautiana katika mambo yanayosikilizwa" [Al-Taj wa Al-Iklil, Abd Rabiy Al-Malikiy, 2/62, Dar Al-Fikr].
Na Shekhe Ibn Kamah amesema: Shekhe Ezz Al-Din Ibn Abd As-Salam alipoulizwa juu ya vyombo vyote, akasema: Mubaha -yaani halali- na Sheikh Sharaf Al-Din At-Tilmisani alisema: Ibn Abd As-Salam alitaka kusema kwamba hakuna dalili sahihi katika Sunna inayoviharamisha, akiwaambia maneno hayo watu wa Misri- Na Shekhe Ezz Ibn Abd As-Salam alimsikia maneno yake na alimjibu: Hapana, nimekusudia kusema hayo ni halali.[kutoka Farah Al-Asmaiy Bi Rukhs Al-Samaiy, Abu Al-Mawahib Al-Shazly].
Na Al-Kurtubiy amenukuu katika " Al-Jamii Li Ahkam Al-Quran" kauli ya Al-Kushiriy: Muziki ulipigwa mbele ya Mtume S.A.W siku ya kuingia Madinah na Abu Bakr akakemea hayo lakini Mtume S.A.W akasema: "Waacheni Ewe Abu Bakr; ili Mayahudu wajue kwamba dini yetu ni pana" na wanawake wa Madina walikuwa wakipiga muziki na kuimba: Sisi ni mabinti wa Al-Najar, na Muhamad ni jirani bora zaidi, kisha Kurtubiy akasema: "Imesemekana kwamba ngoma katika ndoa ni kama dufu, na pia vyombo vya muziki vinavyoitangaza ndoa inajuzu kuvitumia kwa maneno yaliyo mazuri na si maneno machafu" [Tafsiri Al-Kurtubiy, 14/54].
Na Al-Shaukaniy amenukuu kauli ya walioharamisha muziki na waliohalalisha na aliashiria juu ya dalili za makundi yote mawili katika "Nailu Al-Awtwar" Katika mlango wa yaliyokuja katika vyombo vya pumbazo, na alitoa maoni yake juu ya Hadithi: "Kila kinachompumbaza muumini ni batili isipokuwa vitu vitatu kucheza na famili yake, kumfunza farasi wake na kulenga kwa upinde wake " Kwa kauli ya Al-Ghazaly: “Tumesema kwamba kauli yake S.A.W "Ni Batili" haimaanisha ni haramu; bali inamaanisha hakuna faida , kisha Al-Shaukaniy akaema: "Na hilo ni jawabu sahihi; kwani yasiyo na faida ni katika mlango wa mubaha" na alitoa dalili nyingine juu ya kuhalalisha muziki kama Hadithi ya mwanamke aliyeweka nadhiri ya kupiga dufu mbele ya Mtume S.A.W Mwenyezi Mungu akimrudisha salama katika vita miongoni mwa vita na Mtume S.A.W alitoa ruhusa kwake ili kutekeleza nadhiri na dufu ikapigwa. Imepokelewa na kusahihishwa na At-Tirmiziy kutoka Hadithi ya Buraida R.A, na ruhusu yake ilimaanisha kwamba kutenda kwake si maasia katika msimamo kama huo. Na Al-Shaukani aliashiria kwenye risala yake kwa anwani" Ibtal Daawa Al-Ijmaa ala Tahrim Mutlak As-Samaiy" (kubatilisha madai ya kuwa kuna Ijmaii katika suala la kuharamisha kusikilizia muziki kwa ujumla). [Nail Al-Autwar 8/118].
Na Ibn Hazm amesema: "Kwamba Mtume S.A.W alisema: Matendo hutegemea nia, na kila mtu atalipwa kwa nia yake" na aliyenuia kusikia wimbo ili kumwasi Mwenyezi Mungu basi yeye ni fasiki, na pia kila kitu sio uimbaji tu, kilichosaidia mtu kumwasi Mwenyezi Mungu mwenye kukitenda ni fasiki, na aliyenuia kutokana na wimbo kuburudisha nafsi yake ili apate nguvu za kumcha Mwenyezi Mungu na kuchangamsha nafsi yake ili kufanya wema basi yeye ni mtiifu mwenye vizuri na kitendo chake ni haki, na asiye nuia utii au maasia kitendo chake hakina maana ni chenye kusamehewa, kama mtu kutoka kwenda kuitembelea bustani yake na kukaa kwake mbele ya mlango wa nyumba yake na kutizama". [Al-Mahali, Ibn Hazm (7/567)].
Na kutokana na yaliyotangulia tunakuta kwamba uimbaji kwa kutumia chombo cha muziki au kutotumia chombo cha muziki ni suala lililokuwa na majadiliano mengi na mazungumzo kati ya Wanazuoni wa kiislamu tangu zama za awali; waliafikiana katika maudhui na kutofautiana katika maudhui nyingine. Waliafikiana kwamba wimbo ukiwa na maneno machafu ni haramu au ufasiki au kuchochea maasia; kwa maana wimbo ni maneno tu: Uzuri wake ni uzuri na ubaya wake ni ubaya, na kila kauli yenye mambo ya haramu ni haramu. Basi ni nini fikira yako katika hali ya mkusanyiko wa mizani, wimbo na Athar?
Na wameafikiana kutokana na hayo uimbaji wa kimaumbile uliokuwa hauna vyombo na uchocheo/ ushawishi, na hayo ni katika minasaba ya furaha iliyo halali kama Arusi, na kurejea aliyekuwa mbali, siku za Eid, na kadhalika, na wamehitalifiana katika uimbaji kwa kutumia vyombo vya muziki.
Na kauli tulioichagua ni kuruhusu kutumia vyombo vya muziki na kusikiliza kwa sharti ya kuchagua nzuri na kutoshughulishwa na yanayomuweka mbali juu ya kumtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu au yanayosabibisha ufisadi na hayaambatani na sheria tukufu; kwani hakuna yaliyohukumu na kukataza kusikia sauti nzuri zenye mizani pamoja na chombo cha muziki katika Qur`ani Tukufu na Sunna ya Mtume S.A.W au Qiyasi au kupata dalili za kisheria kutokana na vyanzo. Na maumbile safi yanahisi sauti nzuri na yanapenda, hata inasemekana kwamba sababu ya hayo ni tamko la Mwenyezi Mungu kwa wanadamu katika ulimwengu kabla ya kuanza uumbaji alipowaleta wanadamu kutoka migongoni mwao kizazi chao na akawashuhudisha juu ya nafsi zao, akawaambia: Je, Mimi si Mola Mlezi wenu? , na hii ndiyo tunayoona inaafikiana kwa wakati wetu.
Na kunatakikana katika hali hii kuonya juu ya mambo yafuatayo:
Inajuzu kuchagua baina ya Madhehebu ya wenye kujitahidi na Maimamu wanaofuatwa: kwani masuala ya kisharia ni pande mbili: Upande ulio na makubaliano kutoka kwa maulama (Ijmaa) na ikajulikana kama ni udharura katika dini na upande huu haijuzu kutofautiana nao; kwani inamaanisha dhati ya Uislamu, na kutia shaka ni kama kuitilia shaka misingi ya dini. Upande mwingine ni: hayo Maswala waliyohitilafiana katika hukumu yake Maulama na hakuna Ijmaa kati yake; na jambo lake ni pana , na tofauti juu yake ni rehema, na Muislamu ana hiari kuchagua rai yeyote katika kauli za Maulama kuhusu maswala hayo.
Ukemeaji unakuwa katika yenye Ijmaa: Al-Suyuti katika kitabu cha: [Al-Ashbah wa Al- Nadhair] Alitaja kwanba: "Yaliyo na tofauti hayakemewi, lakini yaliyo na Ijmaa yanakemewa" na hii inamaanisha kwamba suala likiwa na tofauti kwa kwenye Madhehebu mbalimbali za Kifiqhi haijuzu kwa watu wa Madhehebu nyingine kukemea rai za watu wa Madhehebu mengine katika suala hilo; kwani kuna tofauti kati yao.
Kutofautisha baina ya mpaka wa Fiqhi na hukumu ya mpaka wa kujichunga: Na Maulama waliafikiana juu ya mpaka wa kujichunga kuwa ni mpana zaidi kuliko mpaka wa hukumu za Kifiqhi; na hiyo ni kwa sababu Mwislamu anaweza kuacha mambo mengi ya halali kwa kujichunga, na hii haina maana ya kumlazimisha mwingine mambo hayo kama ni wajibu kisharia, ataingia katika kuharamisha halali, na pia hapaswi kutumia hukumu za dhana zenye hitilafu kama hukumu zisizo na shaka ya ijmaa na ataingia katika hali ya Bidaa kwa kuyabana aliyoyapanua Mwenyezi Mungu Mtukufu na Mtume wake S.A.W, bali anapaswa kutumia maadili mema katika hali ya hitilafu kama katika mwenendo wa Al-Salaf katika maswala yenye hitilafu na ya jitihada.
Na kwa mujibu wa hayo na katika jibu la swali hilo: Hakuna kizuizi kinachokuzuia kusikiliza vyombo vya muziki muda wa kuwa muziki huo sio njia ya kukupelekea katika kufanya vitendo vya haramu au haukushughulishi mpaka ukaacha ya wajibu.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi.
Arabic
Englsh
French
Deutsch
Urdu
Pashto
Hausa
