Kutungika picha na masanamu, bima n...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kutungika picha na masanamu, bima na kuweka akiba benki

Question

Ni ipi hukumu ya kisharia katika kutungika picha au masanamu katika nyumba au ofisi?

Ni ipi hukumu ya kisharia katika kuanzisha mfuko wa bima au kuweka pesa benki kwa ajili ya kusomesha watoto au kuwaozesha?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, Maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:

Kwanza: Hakuna kizuizi kutungika picha; kwa sababu ni kivuli na hakuna kufanana na Alichokiumba Mwenyezi Mungu, bali makusudio ya picha iliyokatazwa katika Hadithi tukufu: Masanamu ambayo yanaelezea uumbaji wa Mwenyezi Mungu, hakujuzu kuyaweka majumbani au ofisini isipokuwa yakiwa pungufu,kama kuwepo mwili bila ya kichwa au kichwa bila ya mwili, au kuwa na vitobo kwa namna hakuwezekani kwa mnyama kuendelea kuwa hai katika hali kama hii, au yawe yanafanana na michezo ya watoto, baadhi ya Wanazuoni wamejuzisha kuweka masanamu ikiwa lengo lake si kufananisha na uumbaji wa Mwenyezi Mungu.

Pili: Hakuna kizuizi kuanzisha mfuko wa bima au kuweka akiba benki na kuchukua faida yake; mambo yote haya mawili ni katika miamala ya kisasa ambayo Wanazuoni wametofautiana kuhusu mambo haya, na ambalo tunatolea Fatwa sisi ni kujuzu yote mawili; hakuna ubaya kwa Muislamu kufanya miamala na chochote kati ya viwili hivi.

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi

Share this:

Related Fatwas