Hukumu ya Swala ya Mwanamke akiwa n...

Egypt's Dar Al-Ifta

Hukumu ya Swala ya Mwanamke akiwa na damu ya hedhi

Question

Je, mwanamke anasitisha kuswali akiona damu ya hedhi ya rangi ya kahawia ama asubiri mpaka damu ikawa nyekundu au nyeusi?

Answer

Mwanamke akiona damu kabla ya haijatimia siku kumi na tano tangu hedhi iliyopita, basi damu hii si damu ya hedhi, bali ni chini yake; yaani; Istihada.

Lakini akiona damu baada ya kupita siku kumi na tano au zaidi tangu hedhi yake ya mwisho, basi ni damu ya hedhi, sawa ikiendelea kwa muda sawa na muda wa hedhi yake ya kawaida au zaidi au chini, sharti muda isizidi siku kumi na tano, wala haijuzu kwake kuswali ndani ya muda hii.

Na muda wa kushuka damu ikizidi siku kumi na tano, basi anatwaharika, na inawajibika kwake kuswali wakati huo; kwa sababu damu inayoshuka ni damu ya istihadha, si damu ya hedhi.

Maelezo

Kama ilivyo thibitishwa katika Sharia, Swala ndiyo nguzo ya Uislamu na nguzo ya pili baada ya Shahada mbili, kwa mujibu wa kauli ya Mwenyezi Mungu (S.W.): {Na simamisheni sala na itoeni zakati na rukueni pamoja na wanaoruku} [Al-Baqara: 43], na Akasema: {Hakika sala imekuwa juu ya waumini kitabu kilichowekwa wakati} [An-Nisaa: 103]. Na kutoka kwa Abdullah bin Umar radhi za Mungu ziwe juu yake na baba yake, alisema: Mtume (S.A.W.) alisema: «Uislamu umejengwa juu ya nguzo tano: kushuhudia kwamba hapana Mungu ila Mwenyezi Mungu na kwamba Muhammad ni Mtume wa Mungu, na kusimamisha sala, na kutoa zaka, na kuhiji nyumba, na kufunga Ramadhani» (Imepokelewa na Al-Bukhari).

Swala ni faradhi kwa kila Muislamu mkubwa mwenye akili, lakini inahitaji utakaso (twahara) kutoka uchafu mdogo na mkubwa ili iwe sahihi. Haijuzu kwa mwanamke kuswali wakati wa damu ya hedhi au damu ya nifasi, kama katika Hadithi ya Abu Sa'id Al-Khudri (R.A.): Mtume (S.A.W.) alisema: «Je, si kwamba ikiwa anapata hedhi haombi wala hafungi?» (Imepokelewa na Al-Bukhari).

Damu inayotoka kwa mwanamke ina aina tatu kuu:

Damu ya Nifasi (nifas): Damu inayotoka baada ya kujifungua, na inaweza kuendelea hadi siku arobaini. Kutoka kwa Umm Salama (R.A.): «Wanawake waliokuwa wakipata nifasi wakati wa Mtume wa Mungu (S.A.W.) walikuwa wakikaa baada ya nifasi yao siku arobaini» (Imepokelewa na Abu Daud).

Damu ya hedhi (haydh): Damu inayotoka kila mwezi kwa kawaida, na kiwango chake cha juu ni siku kumi na tano (kwa wengi wa Wanachuoni wa Fiqhi)[1]. Na sifa yake kama Mtume (S.A.W.) alivyoieleza katika Hadithi iliyosimuliwa na Abu Umama Al-Bahily aliposema: Mtume alisema: «Damu ya hedhi ni nyeusi iliyoganda na ina wekundu juu yake, na damu ya mwenye istihadha ni ya manjano nyepesi»[2]

Damu ya istihadha (istihadha): Damu inayotoka baada ya kukamilika kwa damu ya nifasi au baada ya kumalizika kwa muda wa hedhi.

Kuhusu hukumu ya mwanamke kuswali wakati wa damu:

Kwanza: Haijuzu kuswali wakati wa damu ya hedhi au nifasi bila kujali rangi yake (nyekundu, nyeusi, kahawia[3] n.k.), kama katika Hadithi ya Fatma bint Abi Hubaysh (R.A.) ambaye alikuwa anapata istihadha, Mtume (S.A.W.) akamwambia: «Ikiwa ni damu ya hedhi basi ni damu nyeusi inayojulikana, basi acha Swala; na ikiwa ni nyingine basi tia udhuu, kwani hiyo ni damu ya mshipa[4]»[5] (Nasa'i).

Pili: Wakati wa damu ya istihadha, inawajibika kufanya udhu kwa kila Swala ya faradhi baada ya kuingia kwa wakati wake, kisha aswali faradhi hiyo na Sunna anazozitaka.

Tunapata faida kutokana na yaliyotangulia:

Mwanamke akiona damu kabla ya kupita siku kumi na tano (15) tangu utakaso wake kutoka hedhi yake iliyopita, basi hiyo si damu ya hedhi, bali ni damu ya istihadha.

Ikiwa mwanamke ameona damu na kupita siku kumi na tano (15) au zaidi tangu utakaso wake, basi hiyo ni damu ya hedhi; bila kujali kama muda wa hedhi hii ni kawaida yake au zaidi au chini, sharti isi zidi siku kumi na tano. Na haijuzu kwake kuswali katika muda huo.

Ikiwa muda wa kushuka damu ukizidi siku kumi na tano (15), basi atajitwaharisha, na inawajibika kwake kuswali wakati huo; kwa sababu damu inayoshuka ni damu ya istihadha, si damu ya hedhi.

 

[1] “Al-Majmu’u cha Al-Nawawy (2/376), na Mughni Al-Muhtaj cha Al-Khatib Al-Sherbeiny (1/278)”

[2] Imepokelewa na Al-Daraqutny katika kitabu chake cha Sunan (1/405)

[3] “Al-Majmu’u” cha Al-Nawawy (2/391)

[4] Maana yake ni damu ya mshipa si damu ya hedhi.

[5] Imepokelewa na Al-Nasaiy

Share this:

Related Fatwas