Kujiamini na kutokuwa na kiburi
Question
Mwanamume anasifika vipi na kujiamini?
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, Maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Kujiamini hakumaanishi kiburi, lakini kunamaanisha kuwa mwanadamu anajitambua na kujua uwezo wake, anaimani na anachokifanya hatetereshwi na mtu; akifuata katika yote hayo kuwa Mwenyezi Mungu Amemtukuza kama mwanadamu na Amemuumba kwa mkono wake, na sifa zake zimedhihiri kwake, na Akamfanya kuwa Muislamu katika wafuasi wa kipenzi cha Mwenyezi Mungu Mtume S.A.W., akifuata katika hilo kauli ya Mwenyezi Mungu: {Basi mtegemee Mweneyezi Mungu; hakika wewe uko juu ya Haki iliyo wazi } [An-Naml: 79].
Utashi wake wa nguvu unatokana na kusifika kwake kwa sifa za ukamilifu ambazo Mwenyezi Mungu Amezitaka kwa mwanadamu kujipamba nazo; kama ilivyokuja katika Hadithi: “Jipambeni kwa tabia za Mwenyezi Mungu” na maaana hii inahitaji unyenyekevu si kiburi, kwa sababu inapelekea katika rehema kwa walio pembeni yake, na kuwapenda viumbe wa Mwenyezi Mungu; kwa Imani yake kwamba Mwenyezi Mungu ndiye ambaye Amemuumba, hakuna sababu ya kiburi kwa viumbe wa Mwenyezi Mungu.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi.
Arabic
Englsh
French
Deutsch
Urdu
Pashto
Hausa
